Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Zao la vitunguu swaumu ni zao ambalo linaonekana limesahaulika japo linalipa sana,
Nilikua manyara mwaka jana nilipata jifunza haya yafuatayo:
/zao hili haliitaji maji meng kama ilivo vitunguu maji huitaji maji mengi mara moja kwa mwezi
/ zao hili huchukua mieZ 4 hadi 5 kuweza kua tayari kuingia sokoni
/ zao hili haliuzwi kimagunia wala kimadebe ni bei sana hivo linauzwa kwa neti ( net moja ni sawa na beseni moja na nusu) ambayo bei ya neti moja n shillingi elfu 56.
/ bei ya mbegu mara nyingi huwa wakulima wazao hili wananunua kwa mabeseni ambapo beseni moja la mbegu ni shillingi elfu 35
/ zao hili huna haja ya kubeba na kupeleka sokoni wanunuzi wanakufata wenyewe na mafuso yao japo ukienda navyo mombasa au sudani pia uganda ni ghari sana huuzwa huko.
/ mahali ambapo zao hili hustawi n katika udongo wa pemben mwa mabonde udongo ambao sio mgumu sana mtanisamehe aina ya udongo sijui ila mabonden lakn maji yawe yanazuiwa na kuruhusiwa mara moja kwa mwezi au hata mara mbili cio mbaya ila yawe kwa wingi yaende chini,
/ mikoa ya manyara , singida morogoro na baadh ya mikoa ya kusimi yanasupport sana

Mkuu vp dodoma kitu swaumu kinaweza kubali?
 
Kiranga Mtanzania anaogopa fursa za kilimo ndo maana ardhi imekuwa ugomvi na nchi jirani. Wenzetu wanajua kuichezea ardhi vizur.
 
Kwa dodoma linakubali hata wilaya zile ambazo zinapakana na manyara hili Zao linapenda mabonden kwa ajili ya upatikanaj wa unyevu nyevu na maji (ardhi oevu) kwa sumbawanga sijajua hali ya hewa ya huko ila nadhan Zao hili halina condition ngumu sema ardhi utakapo lika pasiwe pagumu na paweze kutunza unhevu nyevu na ndo mana linapenda mabondeni ( udongo wenye tabia ya kijaruba)
 
Pilipili Mtama je?
Unamaanisha pilipili manga? (Black pepper?)
images
images
images
images
 
Mkuu Babalao 2 kama unamaanisha pili pili zenye picha hapo juu, zao hili nimeliona likilimwa sana wilaya ya Morogoro vijijini ndani ya milima ya Uluguru. Kuanzia Kiroka, Mkuyuni hadi unamaliza Matombo yote zao linastawi. Kwa hiyo maeneo yote yenye hali ya hewa yenye kulingana na mazingira hayo kwa aliyewahi kufika huko yanafaa kwa kilimo hicho. Ilivyozoeleka kikwetu hili zao hupandwa chini ya miti maana ni zao linalotambaa kwa kuzunguka shina la mti. Lakini baadhi ya mataifa hasa ya Asia ambayo watu wa huko ni wajanja na wanachukulia siriazi jambo lolote linaloingiza pesa, walishafanya utafiti kiasi kwamba zao hili linalimwa popote bila kutegemea uwepo wa miti ili zao hilo litambae juu yake, badala yake zinasimikwa nguzo kama zile za umeme kwa mistari na zao hupandwa kisha likatambaa juu yake.

Zao hili huweza kukua na kufikia kimo cha mita 10. Kadri linavyokua hutoa matawi mengi sana na kufanya kakichaka kuzunguka kitu (shina la mti) lilipojishikiza. Na kadri linavyokwenda juu ndiyo linazaa zaidi. Ingawa linaweza kustawi juani lakini linapenda kivuli na hewa yenye unyevu nyevu mwingi (humid air) ndiyo maana linapatikana zaidi maeneo yenye mvua nyingi. Zao hili hustawi maeneo yenye joto kama ilivyo ukanda wa pwani. Linahitaji mvua za uhakika.

Huweza kulimwa kwa kuotesha mbegu lakini huoteshwa kwa urahisi zaidi kwa kutumia vipande vya shina. Likishapandwa huchukua miaka 3 hadi 4 kuanza kuvuna. Uzalishaji wake huchanganya ikifikia umri wa miaka 8 na huendelea kuzaa hadi miaka 30. Huchukua miezi 9 baada ya kutoa maua hadi kuvuna. Zao hili huzalishwa kwa kutambaa kwenye nguzo zenye kimo cha mita 4 (au mbao pia nguzo za zege au miti hai kama minazi) zilizosimikwa umbali wa mita 2.4 kwa 2.4. Kwa hiyo hupandwa baada ya kuweka nguzo. Kuna aina tofauti tofauti za pilipili hizi. Zao hili pia hushambuliwa na wadudu na magonjwa yapo.

Ugumu wa zao hili uko kwenye muda mreu wa kusubiri hadi uanze kuiona faida, mahitaji makubwa ya nguvu kazi ya kuvuna na kuchakata, gharama kubwa kama utatumia nguzo kwa ajili ya kusapoti zao. Huwekewa mbolea kwa ustawi wenye uhakika.

Mavuno kwa mmea mmoja wenye umri wa miaka 7-8 unaweza kuzalisha kilo 2 ya pilipili kavu kila msimu wa mavuno. Kwa hiyo mavuno kwa shamba itategemea idadi ya mashina. Utaalamu ukitumika ekari moja yaweza kuzalisha pilipili zilizokaushwa kilo 1500.

Sina uhakika na bei ya kilo moja sokoni, tusaidiane kwa hilo ili tuweze kuona mwanga vizuri zaidi. Ukipita maeneo ya Mkuyuni - Matombo utaona zao hilo limejikalia bila kupewa matunzo yanayostaili kama wanavyofanywa kuku wa kienyeji lakini nchi za wajanja zao hili linaitwa Black Gold (dhahabu nyeusi) nadhani unaelewa ninachomaanisha.

Huu ni muhutasari mfupi sana mazao ya pesa hayawagi na maelezo mafupi hivi, kuna mengi yakuzingatia nimeona nifupishe nisichoshe wasomaji.
 
Basi pilipili manga huhitaji uwe na shamba lako mwenyewe na si kukodisha.
 
habarini za jioni,
naomba mwongozo, je ardhi ya maeneo ya bagamoyo inasupport kilimo cha vitunguu swaumu?
 
habarini za jioni,
naomba mwongozo, je ardhi ya maeneo ya bagamoyo inasupport kilimo cha vitunguu swaumu?

Wanadai bora isiwe ngumu na pia iwe angalau imeshiba mbolea za asili kwani itakuwa laini kwa balbu za vitunguu kujitanua kwa urahisi.
 
Kubota, wewe hujishugurishi na hivi vitu maana yaonyesha una utaaramu wa kutosha na iwapo unajishugurisha tupe intro tukutemberee huko kwenye mashamba kwa kujifundisha zaidi.
 
Kubota, wewe hujishugurishi na hivi vitu maana yaonyesha una utaaramu wa kutosha na iwapo unajishugurisha tupe intro tukutemberee huko kwenye mashamba kwa kujifundisha zaidi.

Mkuu Myanyembehalisi, naomba niiweke vizuri post yako maana ukiisoma kwa haraka haraka ni kwamba HUELEWEKI

Unachomaanisha hapa ni kwamba huamini kama mimi ninautaalamu huo kweli, na iwapo kama kweli mimi ninautaalamu kiasi hiki umenitaka kwa lugha ya upole nikuonyeshe mashamba yangu!

Hicho ndicho ulichohangaika kuandika hapo. Ni mara yangu ya kwanza kukutana na challenji aina hii!! Nimechagua kunyamaza.
 
Poleni lakini pia hongereni kwa majukumu wakuu,ninaomba kufahamu maeneo ambayo yanastawisha ama yana ardhi na hali ya hewa rafiki kwa kilimo cha vitunguu MAJI/SAUMU mkoani MOROGORO.

Lakini pia nipate mchanganuo wa jinsi na GHARAMA za uzalishaji,MATUNZO na mengineyo kwa ujumla.na nitafurahi sana kama nitampata mkulima wa zao hilo moja kwa moja ili awe SHAMBA DARASA kwangu.natanguliza shukrani zangu za dhati.

"Nawasilisha wakuu"
 
Back
Top Bottom