Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

uko sawa kabisa sio wavivu wa kazi tu hata uvivu wa kufikiri: ingekuwa thread inazungumzia chadema,kagame,ccm ungeona watu 400 wanachangia lakini kama hii yenye faida hata kusoma hawasomi kufikiri

Sisi ni wataalam wa kuchonga ngenga
 
Wakuu mmenisusa.
Mkuu hebu pitia thread ya Babalao 2, inaitwa 'Nahitaji utaalamu wa kilimo cha vitunguu swaumu' ukisoma utajua mahitaji ya mbegu kwa ekari.

Nenda sokoni kaulize bei ya kilo ya vitunguu swaumu ili ujue itagharimu sh ngapi kwa eka. Kisha pitia humu kwenye jukwaa kunathread nyingi tu za kilimo cha vitunguu maji watu wamemwaga michanganuo makini ya gharama za kulima vitunguu maji.

Tumia hiyo michanganuo kufanya makadirio ya vitunguu maji kwa ajili ya vitunguu swaumu maana hakuna tofauti ya gharama za huduma. Kama unataka ulime eneo lenye wajuaji ili ujifunzie kwao nenda ukalimie eneo linaitwa Lumuma.

Je jibu hili limekupa mwanga kidogo? Nakutakia kila la heri.
 
Mkuu kubota nashukuru kwa majibu yenye tija naahid kuufanyia kaz ushaur wako.ila bado sijajua hiyo lumuma ipo wap mkuu.natangulza shukrani tena kwa msaada ujao.
 
Kubota, wewe hujishugurishi na hivi vitu maana yaonyesha una utaaramu wa kutosha na iwapo unajishugurisha tupe intro tukutemberee huko kwenye mashamba kwa kujifundisha zaidi.

Nadhani ungeomba ufahamishwe eneo la karibu na makazi yako linalolimwa zao ulitakalo ili ufike kwa urahisi.
 
Mkuu kubota nashukuru kwa majibu yenye tija naahid kuufanyia kaz ushaur wako.ila bado sijajua hiyo lumuma ipo wap mkuu.natangulza shukrani tena kwa msaada ujao.
Mkuu sorry nilipitiwa, Lumuma iko wilaya ya Kilosa. Ni eneo maarufu sana kwa kilimo cha vitunguu. Bonde la Lumuma liko mpakani mwa wilaya ya Kilosa na Mpwapwa.

Ni wilaya ya Kilosa yenye umaarufu wa kustawisha vitunguu japokuwa wilaya zingine mazingira yanaruhusu kulimwa zao hili.
 
mkuu sorry nilipitiwa, lumuma iko wilaya ya kilosa. Ni eneo maarufu sana kwa kilimo cha vitunguu. Bonde la lumuma liko mpakani mwa wilaya ya kilosa na mpwapwa. Ni wilaya ya kilosa yenye umaarufu wa kustawisha vitunguu japokuwa wilaya zingine mazingira yanaruhusu kulimwa zao hili.

nashukuru mkuu kubota,nitayafanyia kazi yote yahusikanayo.
 
baadhi ya jf members tunafanya projects zetu pamoja lakini kila mtu anamiliki kivyake. Unakuta kwa mfano huko kwenu Iringa tunawekeza pamoja kila mtu kwa kadri ya uwezo alio nao. Lakini kuna mambo tunashirikiana ili kupunguza gharama fulani fulani. Na sio kwenu tu, hata huku Pwani pia tunashirikiana ktk miradi mingine. Nakuletea mail.

Pwani mnaendeleza miradi gani mkuu?

Naomba unijuze bro
 
Binafsi nalima kitunguu maeneo ya Kware Ruaha Mbuyuni hapa ni potential kw maana ya irrigation na ardhi ni nzur kw kitunguu. Hili zao linahitaj ujikamilishe kifedha unapoanza kulima ni muhimu ukaitenga pesa yake pemben kbsa kw heka inayohudumiwa vzur kila kitu inagarim million 3 ukiweka na lak 5 ya miscellaneous inakua vzur incase kuna mlipuko wa magonjwa km n'gonyo ambao wana athar kubwa na hugarim dawa kila baada ya siku kadhaa. Kware heka moja inakodishwa kw laki na nusu na pamp ya kumwagilia ni elf 50 jumla lak 2 mbegu huuzwa kw lita yale makopo yanayo nywewa mbege vilabuni ambapo kw kila lita ni elf 25 na heka moja inahitaj lita 10 ukiongeza mbili sio mbaya Kulima kw trekta ni sh elf 50 kw heka na ngombe ni 30 ila kw trekta ni nzur zaid cz inachimbua udongo vzur na hupunguza majan meng kuota halaf kuna kupengelenga hii ni kutengeneza majaruba kw ajili ya vitalu vya mbegu na yale ya kupandia shamban kw yale jaruba za mbegu hufanyaga sh 300 kw jaruba kw lita 10 unaweza pata jaruba 35 na zikizid bas kidgo sna halaf kw zile za shamban uwa wana charge kw heka ambapo kw heka wana pelenga laki na 20 hapo inabidi wasawazishe ardhi mana trekta linatifua sna ambapo kw heka wanafanya chini kbsa elf 10 ila wanaanzia elf 20.. Then kuna kupanda mbegu (Kuombeka) hapa ni sh 400 mpka 500 kw jaruba heka moja huwa na jaruba maxmum 400 halaf unapiga dawa ya kuzuia magugu weed stop na ile ya kuua majan yaliyo ota galgan au oxfan hizi ni elf 22 kw lita kw weed stop na unahitaj lita 4 kw heka kuna zile za kuua na kuzuia wadudu km DuDuba 13 kw ml 500 na unahitaj lita 1 kw heka na profercon elf 17 kw lita na unahitaj lita 2 kw heka na ile ya kuzuia ukungu kwenye majan ya kitunguu Amezeb elf 8 kw gram 500 na unahitaj kilo 1 kw heka then kuna mbolea apply after 2 wks urea elf 60 sehem nyngne mpka 66 kw mfuko na heka huitaj mifuko 4 then baadae CAN hii ni kw kukuzia mfuko elf 50-55 weka tena 4 ila dawa zinaweza kua constant kutokana na uwepo wa magonjwa pia gharama constant ni ya kumwagilia ambapo eka moja huitaj diesel lita 10-15 kutegemea na umbali wa shamba toka mtoni pia gharama za kijana atayemwagilia ambapo hudai elf 10-15 kw heka na pia wapiga dawa hudai elf 15 kw heka close supervision ni muhim sna inacse bajet inabana unaweza mwaga urea once then after 3-4 weeks ukapiga booster inaitwa super grow hii ni nzur sna kw kukikuza kitunguu jus elf 22 unapata lita nzima na inatosha kw heka nzima ukishapanda maji ni mara moja kw wiki kumwagilia na wakat wa kuvuna wanacharg 100-200 kw jaruba halaf kuna kukata majan ya kitunguu sh 2000 kw gunia. Eka moja iliyohufymiwa vzur hutoa gunia 70-80 na kila gunia ni elf 80 uwa inapanda mpka lak na 10 kikiwa adim na pia huweza kusguka mara chache mpka elf 70-75 ila average ni 80 kw shamban Vitunguu vya Ruaha Mbuyuni vinalimwa kiustad tofaut na singida au dodoma ivyo bei yake iko juu na huweza kulipa mara 3 mpka 4 zaid kw faida ila uhudumie vzur shamba.. Karibuni

Mkuu hii umeiweka vizuri..Ntakutafuta
 
Safi sana mkuu wewe ni zaidi ya afisa kilimo naomba uni PM namba yako mkuu natanguliza shukrani
 
wakuu vitunguu saumu kwa mkoa wa iringa vina kubali sehem gani?kule mbuyuni sijaona kama wana lima hili zao zaidi ya kitunguu maji.
 
Nashkuru Mkuu kubota heshma yako sana. Aisee uliposema mnatifulia kitunguu nimeogopa sna manake iyo gharama yake naona km unaweza kulima heka nyngne tano za mahindi. Dawa hizi ni msaada mkubwa sna mfano weed stop unapiga mara tu baada ya kupanda hii huzuia nyas yoyote ambayo haijaota isiote tena hii ni maalum tu kw sehem ambayo haijaota nyas ukipiga cc km 60 mpka 80 ivi umemaliza kaz jan halioti mpka unavuna kitunguu lakin kuna majan yanaweza yakawa yalishaanza kuota kipind unapiga weed stop so hapa ndo unapiga Galgan au Oxfan haya magugu yape wiki moja tu yote yamekauka mfano wa kuungua so kw heka moja utatumia elf 60 kudhibiti magugu kw msim mzima mpka unavuna.. kwan ww unalima wap mkuu?

Nimekucheck mkuu hongera sana kwa kuwa na information za kutosha,naamini nitapata ushauri wa kutosha kutoka kwako!!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom