Entrepreneur
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 1,087
- 622
Mkuu baraka607, wazo na
ushauri wako ni mzuri sana kwa wanajamii wanaotaka kujishughulisha na
Zao tajwa. hesabu ulizoweka juu ni za kuvutia hasa kwa anayehitaji
changamoto kutoka kwa mtu aliyejaribu biashara hio.
USHAURI WANGU KWAKO
Nadhani ungewavuta wengi sana na kununua mbegu kwa wingi iwapo
ungewaekea takriban za gharama. kwa mfano, kama inaitajika mbolea ni ipi
na kiasi gani, upandaji wake ni vipi, utaalamu wa kutoa vitunguu vingi
na kadhalika nyingine nyingi tu. mimi sio fundi wa haya mambo ila
nadhani umenipata. na kwenye gharama ukitaka mteja wa mbegu arudi
ungepiga kama ulivyosema hapojuu wewe umeuza at minimum price of 85K.
85k *100 gunia = 8500,000/=
Ans - 600,000 za mbegu kutoka kwako=7900,000 Then Gharama za uzalishaji
kwa takriban. kwa hilo mtu anaweza kujikuta faida ni ndogo kuliko
ulivyotaja na hapo akaamua kununua mbegu za eka mbili ama zaidi ili
kufikia malengo. kwa mtindo huu wewe utauza mbegu na mteja lazima
atasambaza sifa za mbegu yako.
Wazo zuri sana mkuu, na ili kutanua soko lake ni vyema kufanya utafiti wa udongo na hali ya hewa ili kujua mbegu hizo zinastawi zaidi sehemu gani.