Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Hongera mkuu,

Umejaribia wapi, na ulifanya cha umwagiliaji au cha kutegemea mvua, na soko lako lilikua lipi kwa hayo majaribio yako?

Kitunguu huwezi lima kwa kutegemea mvua coz kitakuwa na magonjwa mengi na kukusababishia gharama kuwa kubwa sana. Kitunguu watu wanapenda kunyeshea zaidi ili kupunguza gharama za dawa.
 

Kweli kiongozi na ukipata hasara ni hasara kweli ila ukivuna basiii. Kuna wadudu fulani wanakata vitunguu kwa chini na dawa aina ya marshala au profetroni haiwezi kuwaua wananiumiza sana kichwa sijui huko mnatumia dawa gani mkubwa
 
Kiongozi ukiwa na kama 1.5mil jaribu hata heka moja hutoacha tena na utakuwa na mikakati kama yangu soon

well. am inspired mkuu

unaweza kunipa mchanganuo wa hyo 1.5 mil?

misimu ya kulima inakuwaje? vinakaa shambani kwa muda gani?
 

Safi sna mkuu,

Haya ndio mawazo tunataka hapa JF,

Kuna technolojia mpya na rahisi mno nimeinyaka sehemu juu ya huu ulimaji bado naimalizia resecrh yake nafikiri baada ya miezi sita itakua imekamilika nitaimwaga hapa jamvini.

Kifupi inawezekana kabisa kuchagua ukubwa wa kitunguu chako, kukuza ndani ya miezi miwili tu na kuchangua shape ya kitunguu.

Hii nikiikamilisha nitaileta hapa maana nafikiria kuteka soko lote la Comorro, Kenya na Zanzibar kwa vitunguu bora kabisa na vya bei nafuu na hakuna atakaye shindana na mie.
 
Kweli kiongozi na ukipata hasara ni hasara kweli ila ukivuna basiii. Kuna wadudu fulani wanakata vitunguu kwa chini na dawa aina ya marshala au profetroni haiwezi kuwaua wananiumiza sana kichwa sijui huko mnatumia dawa gani mkubwa

Sisi huku tunatumia dawa 1 hivi inaitwa selecron ni nzuri sana hiyo kwenye vitunguu kwa upande wa wadudu mkuu
 
Asigwe unakijua unachoongea lakin?

Nadhani asigwa anakijua alichokiandika, ndio maana anakifanyia research ili akishajiridhisha, aje kumwaga hapa kitu cha uhakika.

Nilishawahi ambiwa kitunguu kinatakiwa kisiwe kikubwa sana wala kidogo sana. Na kisiwe mapacha, inatakiwa round bulb.
 
Kiongozi ukiwa na kama 1.5mil jaribu hata heka moja hutoacha tena na utakuwa na mikakati kama yangu soon

Ni kweli, sema tukishakua kosa malengo na kujiridhisha na mawazo hewa, unaona kama 1.5M sio kitu na haiwezi kufanya kitu.
Kumbe kuna mtu ukimpa hata 500,000/= baada ya miezi sita utamkuta yuko hatua nyingine kabisa.

Nadhani hapo tunaongelea gharama za kuhudumia shamba, mbegu, mbolea, bila kujumuisha mashine ya kumwagilia maji na mafuta yake.
 
Mi nataka niwe mnunuzi,soko kuu lipo wapi la vitunguu,kuna mtu aliniambia soko ni Kenya ila sina uhakika
 

mkuu laki moja bei ya shambani au sokoni?
 
mkuu laki moja bei ya shambani au sokoni?

Yan hiyo ni ya shambani kabisa mkuu sokon kama dar kariakoo kwa sasa nimesikia ni 150,000 na kuna kipind shamban huwa vinafika had lak 2 gunia 1 najua hutaweza kuamin ila ukwel ndo huo.

Sisi kwetu huwa tunavuna kuanzia mwez wa 9 halafu tunahifadh had mwez wa 2 ndipo vinakuwa vimepanda sana so unapata faida kubwa, kuna jamaa mwaka juz hakulima kabisa akasubir wakat wa mavuno akaja shamban akanunua gunia 100 kwa bei ya elfu 40 akahifadh then akarud zake dar mwez wa pili akakuta bei lak 2 gunia moja akauza zikatoka gunia 90 maana vilipungua kutokana na kukaa kwa muda hivyo kusinyaa akapiga zake m18, akatengeneza faida kama ya m10 hiv ukitoa na garama zingine.
 
heshima kwenu wanajamvi
wakuu mimi naomba kujua mambo yafuatayo kuhusu hichi kilimo!

1. maeneo ambayo ni mazuri kwa ajili ya ulimaji wa hili zao.

2.aina ya mbegu ianayotoa matokeo mazuri.

3. Gharama za ulimaji kwa hekta moja nikimaanisha kuanzia kuandaa shamba, kupanda adi uvunaji!!
Pamoja na gharama nyingine kama dawa nk

5. Pia ningependa kujua vinatumia mda gani mpaka kuvunwa!!
Naombeni sana msaada wenu wakuu
 
Wakuu nani anauzoefu au alishawai lima kiunguu SWAUMU? Nimefatilia sana naona wengi wamejikita kwenye kitunguu maji, kuna mtu aliniambia eti kinalipa sana kushinda kitunguu maji, je wadau ni kweli?

Na kama ni kweli kwanini naona watu wengi wanakikwepa au ulimaji wake ni mgumu sana, wadau mimi nilikuwa nataka kujaribu kulima kitunguu swaumu sasa sijajua vizuri, msaada ma Great thinker mwenye kufahamu kuhusu ulimaji wa kitunguu swaumu na soko lake likoje!
 
hiyo ni gharama ya kila kitu ikiwa ni pamoja na pump na mafuta utaweza hudumia heka moja na vitunguu hukaa shambani miezi mitatu tuu unatoa almasi yako swafiii na mteja uakuwa hapo shambani.
 

Nimejaribu kufuatilia kuhusu kitunguu swaumu huwa akitoki kama kitunguu maji so watu wachache wanalima dus y wanasema kinafaida ila kwa sokoni hakitoki haraka kama kitunguu maji
 

Tunakuombea mungu ufanikiwe kwenye search yako mkuu coz utatukomboa
 
Asigwe unakijua unachoongea lakin?
Believe me mkuu najua nachokiongea,

Umewasikia wale madogo waliomaliza vyuo juzi kati wakatia timu Igunga wakajikita katika kilimo cha kitunguu wanayoyafanya mapaka saa izi??

Believe me ukiinvest katika mambo kama haya kwa nguvu na elimu you are unbeatable
 
hiyo ni gharama ya kila kitu ikiwa ni pamoja na pump na mafuta utaweza hudumia heka moja na vitunguu hukaa shambani miezi mitatu tuu unatoa almasi yako swafiii na mteja uakuwa hapo shambani.

Kama nnachokiona hapa kwenye screen ni cha kweli, kukodi shamba ni kiasi gani? kufanya usafi na yanapatikana kirahisi?
 
mimi kwa huku kukodi shamba kwa heka moja ni 110k then na kukodi mashine ni 100k na muhudumu wa shamba ambaye ndo muangalizi ni 700k then iliobaki ni dawa na mafuta.
kulima na kuweka matuta kwa heka moja 250k.

hiyo ndo pesa utakayo tumia kama vitunguu vyako havijapata ugonjwa wowote kwa heka moja, ugonjwa ukitokea coz dawa ni ghali itaweza panda kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…