Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kuna mtu mmoja alilima kama heka 5 huko kilosa.wanunuzi walikuja shambani akaondoka ns 28M,aliuza sh 80,000 kwa gunia,mwezi wa sita na mie nafikiria kutia timu kilosa nianze na kama heka 3
 
nilikuwa na wazo la kulima vitunguu ila sijapata tu shamba,nadhani unaweza kunisaidia kwa hilo me nipo arusha
 
Believe me mkuu najua nachokiongea,

Umewasikia wale madogo waliomaliza vyuo juzi kati wakatia timu Igunga wakajikita katika kilimo cha kitunguu wanayoyafanya mapaka saa izi??

Believe me ukiinvest katika mambo kama haya kwa nguvu na elimu you are unbeatable

I second you., Mkuu that's right.
Mimi nasubiria hiyo research yako tu mkuu, ili after two years kama Mungu akijaalia niweze kulima
 
Wanasema RED BOMBEY vitunguu vyake ni Vzr Ingawa vinaharibika kwa muda mfupi kwa mtu anataka kusafirisha Mbali ni aina gani ya Mbegu atumie? kwa yyt anaefahamu Ushauri plz!
 
usiingie shambani kulima KWASABABU TU mwenzako amelima akafanikiwa, nenda kwasababu unajua unachoenda kukifanya na umeamua kukifanya.
 
Ndugu zangu najitahid kufuatilia maeneo haya mnayotaja ila sijajua ni kilimo cha vitunguu maji au swaum?
 
Mie ningependa kununua mzigo (mkoan) na kuleta mjini kuuza sasa je! Soko la vitunguu maji liko vipi? Na ni kipind gan bei inakuwa juu? Ili ninunue niweke stoo nisubirie kipind cha kuuza?
 
Mkuu npo sehemu moja inaitwa malolo mpakan na iringa, ni kilimo cha umwagiliaji means kuvuna ni uhakika 100% halafu pia uzuri wa kitunguu huwa hakikosi soko mara baada ya kuvuna sema tu kama soko sio zuri utakiuza kwa bei ya chini na si kukosa soko na wateja huwa wanakuja wenyewe shamban kuvitafuta na si wewe kuwatafuta.
Kingine mkuu kuhusiana na uzuri wa kilimo cha vitunguu ni kwamba utapata hasara kama hutavuna lakin ukivuna huwez kupata hasara hata bei iwe mbaya vip au soko liwe baya vip mtaj wako lazima urudi huwez kupata hasara had ukapoteza na mtaji kwa kitunguu hicho kitu ni never!!!

Ndugu yangu nataman sna kilimo cha vitungu au kununua kutoka kijijin na kuleta mjin ila sijui hata pa kuanzia na mtaji wangu ni 5m ebu nisaidie mawazo
 
Zao la vitunguu swaumu ni zao ambalo linaonekana limesahaulika japo linalipa sana,
Nilikua manyara mwaka jana nilipata jifunza haya yafuatayo:
/zao hili haliitaji maji meng kama ilivo vitunguu maji huitaji maji mengi mara moja kwa mwezi
/ zao hili huchukua mieZ 4 hadi 5 kuweza kua tayari kuingia sokoni
/ zao hili haliuzwi kimagunia wala kimadebe ni bei sana hivo linauzwa kwa neti ( net moja ni sawa na beseni moja na nusu) ambayo bei ya neti moja n shillingi elfu 56.
/ bei ya mbegu mara nyingi huwa wakulima wazao hili wananunua kwa mabeseni ambapo beseni moja la mbegu ni shillingi elfu 35
/ zao hili huna haja ya kubeba na kupeleka sokoni wanunuzi wanakufata wenyewe na mafuso yao japo ukienda navyo mombasa au sudani pia uganda ni ghari sana huuzwa huko.
/ mahali ambapo zao hili hustawi n katika udongo wa pemben mwa mabonde udongo ambao sio mgumu sana mtanisamehe aina ya udongo sijui ila mabonden lakn maji yawe yanazuiwa na kuruhusiwa mara moja kwa mwezi au hata mara mbili cio mbaya ila yawe kwa wingi yaende chini,
/ mikoa ya manyara , singida morogoro na baadh ya mikoa ya kusimi yanasupport sana

Asante mkuu kwa maelezo yaliyojitosheleza.
 
I second you., Mkuu that's right.
Mimi nasubiria hiyo research yako tu mkuu, ili after two years kama Mungu akijaalia niweze kulima
Haina shida mkuu nitaitoa soon, ila kwa kuwa itakua na impact kubwa sana kwa kilimo cha kila aina ni lazima niitafutie haki miliki, wajanja wasije tokea kwenye mgongo wangu wakati mie nakufa masikini
 
Haina shida mkuu nitaitoa soon, ila kwa kuwa itakua na impact kubwa sana kwa kilimo cha kila aina ni lazima niitafutie haki miliki, wajanja wasije tokea kwenye mgongo wangu wakati mie nakufa masikini

Hilo nalo neno! Mkuu nimeku2pia PM cjui km umeiona!
 
Mkuu npo sehemu moja inaitwa malolo mpakan na iringa, ni kilimo cha umwagiliaji means kuvuna ni uhakika 100% halafu pia uzuri wa kitunguu huwa hakikosi soko mara baada ya kuvuna sema tu kama soko sio zuri utakiuza kwa bei ya chini na si kukosa soko na wateja huwa wanakuja wenyewe shamban kuvitafuta na si wewe kuwatafuta.
Kingine mkuu kuhusiana na uzuri wa kilimo cha vitunguu ni kwamba utapata hasara kama hutavuna lakin ukivuna huwez kupata hasara hata bei iwe mbaya vip au soko liwe baya vip mtaj wako lazima urudi huwez kupata hasara had ukapoteza na mtaji kwa kitunguu hicho kitu ni never!!!

Mkuu mi nililima mwaka jana pale ruaha mbuyuni nilikula hasara!
 
Safi sna mkuu,

Haya ndio mawazo tunataka hapa JF,

Kuna technolojia mpya na rahisi mno nimeinyaka sehemu juu ya huu ulimaji bado naimalizia resecrh yake nafikiri baada ya miezi sita itakua imekamilika nitaimwaga hapa jamvini.

Kifupi inawezekana kabisa kuchagua ukubwa wa kitunguu chako, kukuza ndani ya miezi miwili tu na kuchangua shape ya kitunguu.

Hii nikiikamilisha nitaileta hapa maana nafikiria kuteka soko lote la Comorro, Kenya na Zanzibar kwa vitunguu bora kabisa na vya bei nafuu na hakuna atakaye shindana na mie.

Mkubwa kufanya mapinduzi ya vipi vitunguu vyako unataka viwe inawezekana, ila kwenye suala la soko ni ngumu sana. Me ni mkulima wa vitunguu huu mwaka wa tano sasa na mali yangu huwa ziuzii shamba naleta mjini mwenyewe.

Madalali wameharibu soko na wameteka kila mahala, huwez kutoka na vitunguu vyako hadi zanzibar au commoro hautauza na utashangaa ni kwann.

Kuna mkongwe mmoja aliwah jibeba na mzigo wake hadi comorro kufika kule wakawa wanamuangalia kama nini sijui, na alipiga hasara mzigo wote. Individually huwez kuwatoka madalali na hii ni mpaka wizara husika iingilie kati, bila ivo tutaendelea kufanya biashara na madalali tu.

Naongea kwa experience wakuu.
 
Safi sna mkuu,

Haya ndio mawazo tunataka hapa JF,

Kuna technolojia mpya na rahisi mno nimeinyaka sehemu juu ya huu ulimaji bado naimalizia resecrh yake nafikiri baada ya miezi sita itakua imekamilika nitaimwaga hapa jamvini.

Kifupi inawezekana kabisa kuchagua ukubwa wa kitunguu chako, kukuza ndani ya miezi miwili tu na kuchangua shape ya kitunguu.

Hii nikiikamilisha nitaileta hapa maana nafikiria kuteka soko lote la Comorro, Kenya na Zanzibar kwa vitunguu bora kabisa na vya bei nafuu na hakuna atakaye shindana na mie.

Mkubwa kufanya mapinduzi ya vipi vitunguu vyako unataka viwe inawezekana, ila kwenye suala la soko ni ngumu sana.

Me ni mkulima wa vitunguu huu mwaka wa tano sasa na mali yangu huwa ziuzii shamba naleta mjini mwenyewe. Madalali wameharibu soko na wameteka kila mahala, huwez kutoka na vitunguu vyako hadi zanzibar au commoro hautauza na utashangaa ni kwann.

Kuna mkongwe mmoja aliwah jibeba na mzigo wake hadi comorro kufika kule wakawa wanamuangalia kama nini sijui, na alipiga hasara mzigo wote. Individually huwez kuwatoka madalali na hii ni mpaka wizara husika iingilie kati, bila ivo tutaendelea kufanya biashara na madalali tu.

Naongea kwa experience wakuu.
 
Ndugu yangu nataman sna kilimo cha vitungu au kununua kutoka kijijin na kuleta mjin ila sijui hata pa kuanzia na mtaji wangu ni 5m ebu nisaidie mawazo
Kwa m5 yako labda uingie shamba kulima ila kama unataka kusimama kama mlanguzi pesa yako ni ndogo sana, kwa makadilio ya chini kabisa labda uwe na m8 na kuendelea unaweza kumudu fuso ya gunia 85. Manake kuna gharama nyingi sana hapo katikati.

Lets say umeenda shamba umekuta bei ni 65*85=M5.5 bado hujanunua magunia tupu, hujawalipa wajazaji na wachambuaji, hujalipa nauli ya fuso na mambo mengine kibao.
 
Wakuu kwa mkoa wa pwani --Mkutranga rufiji vitunguu vinasitawi kweli?
 
Mkuu ni kweli kabisa unachosema ni kuwa watu hawajajua tu mim nimegusa tu kidogo mwaka jana nimeondoka na mil 3 sasa nataka mwaka huu ndiyo nizame ki kwel kwel, maana kupata gunia 100 kwa kitunguu ni kugusa halafu kuna kipind kama sasa gunia moja laki ×100 una 10milion hapo bado hujatoka tu kimaisha kwa mtaj wa 10 mil wakat wewe garama uliyotumia haizid mil 2 lakin kwa muda mfup unatengeneza faida ya mil 8 Mungu akupe nin tena. Mkuu komaa tu mim ninao mfano kuna watu walianza na mtaj wa laki kadhaa kwenye kilimo cha vitunguu lakin sasa ni matajiri wa kutupwa had unakuja kufikiria kuajiriwa hakuna dili kabisa kwa mtu anaezingatia kilimo

Tuungane bas mkuu tupige kaz .
 
Kwa m5 yako labda uingie shamba kulima ila kama unataka kusimama kama mlanguzi pesa yako ni ndogo sana, kwa makadilio ya chini kabisa labda uwe na m8 na kuendelea unaweza kumudu fuso ya gunia 85. Manake kuna gharama nyingi sana hapo katikati. Lets say umeenda shamba umekuta bei ni 65*85=M5.5 bado hujanunua magunia tupu, hujawalipa wajazaji na wachambuaji, hujalipa nauli ya fuso na mambo mengine kibao.

Ngoja niendelee kuiongezea ka m5 kangu angalao bas ifike 10. Na fuso yenye gunia 100 kutoka iringa-dar inaweza kuwa bei gan?
 
Back
Top Bottom