Kitunguu huwezi lima kwa kutegemea mvua coz kitakuwa na magonjwa mengi na kukusababishia gharama kuwa kubwa sana. Kitunguu watu wanapenda kunyeshea zaidi ili kupunguza gharama za dawa.
My appreciation..... Ila msimu huu soko linakatisha tamaa
Bei ikoje kwani mkuu? Maana hata mikoani mfano Morogoro Kwa rejareja gunia linakusanya 135,000 (bei ya jana). Natarajia bei ya jumla (Kwa mkulima) iwe angalau 100,000 hivi.
Bei ikoje kwani mkuu? Maana hata mikoani mfano Morogoro Kwa rejareja gunia linakusanya 135,000 (bei ya jana). Natarajia bei ya jumla (Kwa mkulima) iwe angalau 100,000 hivi.
Jamani tuache masihara. Wenzenu huku Igurusi na Igawa mbeya tunalia bei ni mbaya sana. Na inakatisha tamaa. Sasa hivi navyoandika hii kitu. Bei ya gunia la vitunguu lenye ujazo wa debe saba ni Tsh. 35000/= (Elfu thelathini na tano) Kama kuna namna nyingine tusaidiane bei inakatisha tamaa. Mimi hadi sasa nasita kuvuna hivi vitunguu.
Nimesema kwa anaetaka kujiunga na group la kilimo whatsapp ani PM namba yake ya simu please!
Sasa Si uvileteee Mjini au Upelekee ArushAa....Bei nzuri sana Huko
Changamoto za kulifikia soko nazo ni kubwa. Madalali nao wengi wao ni wahuni sana. Yaani soko lingekuwa wazi moja kwa moja ningezama.
MILCAH28 soko lilishatekwa na madalali sehemu zote,mkulima akiwa mgumu anafanyiwa fitina apate hasara,ni changamoto sana........
Kuna level nyingi katika uuzaji wa vitunguu, kuna dalali wa shamba,mnunuzi wa kwanza then dalali sokoni mnunuzi wa pili husafirisha mpaka sehemu husika mfano dar then dalali tena ndo vinamfikia muuzaji wa rejareja......hii ndiyo Tanzania
Londoto Moshi
Ntakupa figures kesho,habari nyingi zisemwazo kuhusu ulimaji wa vitunguu hazina uhalisia na zaidi watu huzungumza mazuri tu bila kuweka wazi changamoto zilizopo mwisho wa siku ni majonzi na vilio......kilimo ni kizuri na kinaweza kukutoa kimaisha but yampasa kila aingiaye ajue ya kuwa kuna upande wa pili wa kukosa pia.............