Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kitunguu huwezi lima kwa kutegemea mvua coz kitakuwa na magonjwa mengi na kukusababishia gharama kuwa kubwa sana. Kitunguu watu wanapenda kunyeshea zaidi ili kupunguza gharama za dawa.

Lakini pia kinalipa mno mno ukilinganisha na hizo bei za dawa.

Kwamfano kitunguu kinacholimwa wakati wa kiangazi bei yake huja kuwa kati ya elfu 60 -80 Kwa gunia wakati kile cha wakati wa mvua huanzia laki na sehemu zingine kama Mbeya kinafika hadi lakini na sitini Kwa gunia.

Kwahiyo bado unapata faida sana tu mkuu.
 
My appreciation..... Ila msimu huu soko linakatisha tamaa

Bei ikoje kwani mkuu? Maana hata mikoani mfano Morogoro Kwa rejareja gunia linakusanya 135,000 (bei ya jana). Natarajia bei ya jumla (Kwa mkulima) iwe angalau 100,000 hivi.
 
Bei ikoje kwani mkuu? Maana hata mikoani mfano Morogoro Kwa rejareja gunia linakusanya 135,000 (bei ya jana). Natarajia bei ya jumla (Kwa mkulima) iwe angalau 100,000 hivi.

Dah hiii ni Pesa Nje Nje Aiseee
 
Bei ikoje kwani mkuu? Maana hata mikoani mfano Morogoro Kwa rejareja gunia linakusanya 135,000 (bei ya jana). Natarajia bei ya jumla (Kwa mkulima) iwe angalau 100,000 hivi.

Jamani tuache masihara. Wenzenu huku Igurusi na Igawa mbeya tunalia bei ni mbaya sana.

Na inakatisha tamaa. Sasa hivi navyoandika hii kitu. Bei ya gunia la vitunguu lenye ujazo wa debe saba ni Tsh. 35000/= (Elfu thelathini na tano) Kama kuna namna nyingine tusaidiane bei inakatisha tamaa.

Mimi hadi sasa nasita kuvuna hivi vitunguu.
 
Jamani tuache masihara. Wenzenu huku Igurusi na Igawa mbeya tunalia bei ni mbaya sana. Na inakatisha tamaa. Sasa hivi navyoandika hii kitu. Bei ya gunia la vitunguu lenye ujazo wa debe saba ni Tsh. 35000/= (Elfu thelathini na tano) Kama kuna namna nyingine tusaidiane bei inakatisha tamaa. Mimi hadi sasa nasita kuvuna hivi vitunguu.

Sasa Si uvileteee Mjini au Upelekee ArushAa....Bei nzuri sana Huko
 
Sasa Si uvileteee Mjini au Upelekee ArushAa....Bei nzuri sana Huko

Changamoto za kulifikia soko nazo ni kubwa. Madalali nao wengi wao ni wahuni sana. Yaani soko lingekuwa wazi moja kwa moja ningezama.
 
Changamoto za kulifikia soko nazo ni kubwa. Madalali nao wengi wao ni wahuni sana. Yaani soko lingekuwa wazi moja kwa moja ningezama.

soko lipo wazi banaa..Tafuta Wateja Mbona wako.wengi tu...Jishughulishe Kijanaa
 
MILCAH28 soko lilishatekwa na madalali sehemu zote,mkulima akiwa mgumu anafanyiwa fitina apate hasara,ni changamoto sana........
 
MILCAH28 soko lilishatekwa na madalali sehemu zote,mkulima akiwa mgumu anafanyiwa fitina apate hasara,ni changamoto sana........

Hapana f2 Madalali awawezi kubadili bei ya soko....Sokoni hapa Dar gunia 135 sasa how come dalali akwambie gunia 50000 si kweli na huku kwetu dalali anakula 5000-7000 per gunia....
 
Huenda mkuu but ukweli uko hivyo,kipindi kama hiki bei hushuka sana mpaka elfu thelathini kwa gunia kwani mazao huwa mengi kutokana na kupungua kwa magonjwa tofauti na msimu wa November to January.

Niko wanakolima vitunguu na nimesimama kwa muda mpaka October kuangalia hali itakuwaje msimu huu.....
 
Kuna level nyingi katika uuzaji wa vitunguu, kuna dalali wa shamba,mnunuzi wa kwanza then dalali sokoni mnunuzi wa pili husafirisha mpaka sehemu husika mfano dar then dalali tena ndo vinamfikia muuzaji wa rejareja......hii ndiyo Tanzania
 
Kaka upo wrong sana aiseee....Labda nikuulize unalimaa wapi..?
 
Ntakupa figures kesho,habari nyingi zisemwazo kuhusu ulimaji wa vitunguu hazina uhalisia na zaidi watu huzungumza mazuri tu bila kuweka wazi changamoto zilizopo mwisho wa siku ni majonzi na vilio.

Kilimo ni kizuri na kinaweza kukutoa kimaisha but yampasa kila aingiaye ajue ya kuwa kuna upande wa pili wa kukosa pia.
 
Ntakupa figures kesho,habari nyingi zisemwazo kuhusu ulimaji wa vitunguu hazina uhalisia na zaidi watu huzungumza mazuri tu bila kuweka wazi changamoto zilizopo mwisho wa siku ni majonzi na vilio......kilimo ni kizuri na kinaweza kukutoa kimaisha but yampasa kila aingiaye ajue ya kuwa kuna upande wa pili wa kukosa pia.............

f2 achaa kupaniki kijanaa Kuna ishu nyingi sanaa...Kwa nn Usiifadhi hadi mwezi wa 10 uuze kwa.bei nzuri....Mbona soka la dar Liko Powaaaa sanaa......
 
Habari wakuu wote!!..Tumetengeneza group la whtsapp la Ujasiliamali ili kurahisisha vizuri mawasiliano ya karibu. Kama huto jali unaweza weka number yako ya simu hapa au uka ni PM ili tukuaDd mule.

Tungependaa sana Kupata mabwanaa shambaa na mabibi shambaaa , wafugaji , wafanyabiashara pia' ili tupeani maujuzi na mbinu mbali mbali za ujasiliamali.
KARIBUNI

#GAZETI
#ELNINO
#f2rk
#concrete15
#KITANGE
#Gagurito
#Livanga
#Baraka69
#KIRIKIOU
 
Back
Top Bottom