Kwan gharama/mtaji wa kuwekeza kwenye hekta moja unawekurange sh. Ngapi jamani wachambuzi mnahitajika pls
Hao vijana sina imani nao sana kwani hata mimi ninalima vitunguu, lakini hiyo bei ya kuuzia ni kama wameweka juu ili kuwavutia watu. Naona kama wanaleta siasa kwenye jambo hili.
Gharama ya kulima heka moja ya kitunguu ni kama ifuatavyo. Kulima kwa tractor ni 50,000, Mbegu wangalau ya heka moja haitapungua kilo 4. Kilo moja ya mbegu ni kama 40,000. Dawa zitakazohitajika ni kama za shilingi 50,0000 kwa heka. Mifuko wangalau 8 ya mbolea kwa heka. Kila mfuko ni 60,0000.
Gharama nyinginezo kama chakula, malazi, na gharama ya umwagiliaji kwani utakuwa unatumia mashine au maji mto/mfereji yenye utaratibu wa kijiji nk hayatapungua 400,000 kwani kilimo hiki ni karibia miezi mitano mpaka kuvuna. Kwa haraka haraka gharama ya kulima heka moja inakaribia milioni 1, gharama hizi zinaweza kutofautiana kidogo sehemu na sehemu.
Kiwango cha mavuno kwa heka ni kama gunia 60-70 iwapo mavuno yatakubali. Kumbuka hayo magunia wanunuzi wanaangalia ubora wa kitunguu achia mbali rumbesa la wanunuzi. Bei itategemea na demand na supply.
Iwapo utauza kitunguu kikiwa kingi sokoni ni dhahiri bei itakuwa ndogo, bali bei itakuwa nzuri iwapo kuna uchache wa kitunguu. Hizo bei za 120.000 mpaka 170,000 ni nadra sana kutokea kutokana na mazingira ya soko.
Hivyo kwenye heka moja unaweza kupata faida 500,000 mpaka milioni kutegemea na soko. Kama hiyo faida wanayosema ni kweli kila mtu angelima kitunguu. Mbona wakulima wengi wa kitunguu wamechoka tu.