Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kwan gharama/mtaji wa kuwekeza kwenye hekta moja unawekurange sh. Ngapi jamani wachambuzi mnahitajika pls

Hao vijana sina imani nao sana kwani hata mimi ninalima vitunguu, lakini hiyo bei ya kuuzia ni kama wameweka juu ili kuwavutia watu. Naona kama wanaleta siasa kwenye jambo hili.

Gharama ya kulima heka moja ya kitunguu ni kama ifuatavyo. Kulima kwa tractor ni 50,000, Mbegu wangalau ya heka moja haitapungua kilo 4. Kilo moja ya mbegu ni kama 40,000. Dawa zitakazohitajika ni kama za shilingi 50,0000 kwa heka. Mifuko wangalau 8 ya mbolea kwa heka. Kila mfuko ni 60,0000.

Gharama nyinginezo kama chakula, malazi, na gharama ya umwagiliaji kwani utakuwa unatumia mashine au maji mto/mfereji yenye utaratibu wa kijiji nk hayatapungua 400,000 kwani kilimo hiki ni karibia miezi mitano mpaka kuvuna. Kwa haraka haraka gharama ya kulima heka moja inakaribia milioni 1, gharama hizi zinaweza kutofautiana kidogo sehemu na sehemu.

Kiwango cha mavuno kwa heka ni kama gunia 60-70 iwapo mavuno yatakubali. Kumbuka hayo magunia wanunuzi wanaangalia ubora wa kitunguu achia mbali rumbesa la wanunuzi. Bei itategemea na demand na supply.

Iwapo utauza kitunguu kikiwa kingi sokoni ni dhahiri bei itakuwa ndogo, bali bei itakuwa nzuri iwapo kuna uchache wa kitunguu. Hizo bei za 120.000 mpaka 170,000 ni nadra sana kutokea kutokana na mazingira ya soko.

Hivyo kwenye heka moja unaweza kupata faida 500,000 mpaka milioni kutegemea na soko. Kama hiyo faida wanayosema ni kweli kila mtu angelima kitunguu. Mbona wakulima wengi wa kitunguu wamechoka tu.
 
Kumradhi mkuu tindo vp hio bei ya mfuko mmoja ni 600000 umechanganya au ndo ilitakiwa iwe 60000
 
Kuna mtu alinidokeza juu ya kilimo cha vitunguu. Maelezo yake yanafanana na maelezo ya hapa. Nimejifunza kuna fursa nyingi ambazo tunaziona ndogo kumbe kimsingi ni kubwa sana.
 
Tanzania agriculture extansion officers employed and un-employed
 
hivi vitunguu kwanini vinamtoa machozi mkataji, tafadhali nijibu kwa lugha ya taifa.
Kitunguu hakipendi kukatwa na kisu, ndio maana nacho huwa kinajitahidi kumliza mkataji, kinapenda kukatwa kwa meno, jaribu uone
 
Kitunguu hakipendi kukatwa na kisu, ndio maana nacho huwa kinajitahidi kumliza mkataji, kinapenda kukatwa kwa meno, jaribu uone
ahh!
nimetafuta kitunguu humu ndani, sijapata, kesho nitafanya hilo zoezi.
 
Hongera sana. Hiyo sasa ndio nature ya biashara. Baada ya hapo utafanikiwa. Ushauri wangu uangalie hayo uliyojifunza na ubashiri changamoto nyinginezo ambazo zinaweza kutokea na jinsi ya kuzikabili. Kila lakheri
Safi sana Mr Ha Muji!!! Gogyureo military analyst.
 
Jamani wadau katika masuala ya fursa tusipeane habari za kizushi,..mwenye mawasiliano na TAYOA hatupatie hapa ili tuweze
 
Hizo bei mbei na idadi ya movuno mbona inakinzana?niliulizia watu wanao kaasehemu zinazo limwa kitungu kama mwanga kileo wanasema heka moja inatoa gunia 80 mpaka 120 kama shamba litaudumiwa vizuri na bei ni laki 1 kama soko ni baya..kwa maelezo pitieni YOUTUBE search kilimo cha umwagiliaji cha vitunguu maji mtapata clips nyingi za wakulima mbali mbali wakizungumzia swala hili.
 
Tatizo ni moja, wanaandikaga utafikiri kazi ni rahisi kama kucheza pool kijiweni, ifikie mahali watu waseme ukweli, ujasiriamali ni mgumu unahitaji akili itumike sana na uvumilivu kwa sana, kama hujiwezi kufikiri na sio mvumilivu kaajiriwe tu, la sivyo utaanzisha ujasiriamali na kuacha na kuanzisha nyingine,then utakuwa frustrated na kuperish
 
Tuleteeni mambo yaliyoko jikoni hapa tunasubili kwa hamu kubwa sana.inaweza kufungua mawazo ya walio wengi Na kuwapa mind stability katika kuchukua maamuzi
 
Back
Top Bottom