Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Wanafanya kuanzia 250,000 - 300,000@ heka kwa msimu. Kilimo chake kinaanzia mwezi wa 4 mpaka wa 11. Huwa wanamwagilia kwa mfereji. Shida ni moja hasa wakati wa soko kwani vitunguu vingi huwa vinakuja toka eneo la Mang'ola, hivyo bei hushuka sana.
ok kiongoz nashukuru. hapo inabidi ukilima , lazima usome nyakati ambazo mang'ola wanalima. ili kuweza ku- overtake nao katika soko.ili kabisa kuwa tofauti nao! lakini inaonekana inalipa pia katika hilo eneo kama maji ni mfereji manake ni uhakika w a kupata maji.
nitapita huko siku moja
 
ok kiongoz nashukuru. hapo inabidi ukilima , lazima usome nyakati ambazo mang'ola wanalima. ili kuweza ku- overtake nao katika soko.ili kabisa kuwa tofauti nao! lakini inaonekana inalipa pia katika hilo eneo kama maji ni mfereji manake ni uhakika w a kupata maji.
nitapita huko siku moja

Kitunguu kinatoka fresh sana. Ila shida ni bei sokoni.
 
Mkuu hv haiwezekani kuifadhi vitunguu kwa miezi3/4 mbele

Inawezekana hata mwaka. Ila kumbuka kadiri vinavyokaa muda mrefu toka kuvunwa huwa vinanywea. Yaani unaweza kuvuna maguni labda 100, lakini ukiyahifadhi yatupungua labda mpaka 70 kulingana na muda wa uhifadhi.
 
Duh kumbe shughuli ipo. Hujaweka usafiri wako wakwenda shambani mpaka mavuno
Na ukifqnikiwa unapata she ngapi
Shughuli sio ya kitoto mi nilisha wahi kulima ndugu yangu nakushauri pambana kweli kweli sio kazi ya kitotoooo
 
3.UPANDAJI HAPO PIA UMAKIN UNATAKIW.KTK UPANDAJI WENG HAPO TUMEPISHANA KIMAWAZO KUTOKAN N MAENEO HUSIKA.km ifuatavyo..
MUHESHIMIWA GEBA, inaonekana wewe ni mzoefu.naomba unipe mawazo kuhusu kilimo cha vitunguu swaumu. kwa hapa arusha, kuhusu gharama zake na mavuno katika heakari.
 
naomba kuuliza kwa sasa bei ya shambani gunia la kitunguu ni sh ngap kwa upande wa ruaha
 
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
Naungana na kiongozi katika hili. Kilimo cha kitunguu ni gharama sna. Inaweza ikafika milioni 2 kama unavyosema.
 
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
Umefafanua vizuri sana... Ila ungetuambia ukiuza sokoni faida unaweza kupata bei gani?
 
Mkuu tindo tatizo lako dogo tu. Ilikuwa mara ya kwanza kulima ulipaswa uanze kidogo ili ujifunze kwa gharama kidogo. Biashara yoyote unapoianza mara ya kkwanza mieleka ni kawaida, kama unapojifunza kuendesha baiskeli. Mtu asitarajie anapoanza jambo kwa mara ya kwanza apige bingo haiko hivyo. Pia ukae ukijua kuwa kunapokuwa na mafuriko ya zao sokoni wanunuzi wote na si madalali peke yao hunyanyasa sana wakulima. Hali hiyo ipo katika kilimo cha nyanya pia. Mkoa wa Morogoro ukilima nyanya za kiangazi mwezi wa nane hadi wa kumi na moja huwa kuna mafuriko ya nyanya. anaevuna miezi hiyo na kkama ni mara yake ya kwanza ataapa kwamba nyanya si biashara. Kuna msemo huku NYANYA NINYANYUE NYANYA NINYANYASE. Soko zuri la vitunguu ni mwwezi March hadi June. Ukiweza kuwa na kitunguu majira hayo huna maumivu. wateja wanakutafuta na unaweza kuuza kwa utaratibu unaotaka wewe. wakati huo wewe mwenye mali ndio mjanja. suala la madalali linakuwa halina umuhimu na wala si lazima upeleke sokoni na hata ukipeleka sokoni mzigo wako utagombaniwa.

Tumia utaallam uweze kuhifadhi kitunguu uweze kulifikia soko la Mwezi March, au lima vitunguu uvune February au uvune kuanzia mwezi May hadi July. Ukilima kitunguu cha msimu ambacho kila mtu analima maumivu yake ndiyo hayo. Kwenye suala la soko kunapokuwa na mafuriko hakuna serikali itakayokusaidia hapo utakuwa umeumia tu. wewe mkulima ndiyo unatakiwa uchemshe bongo kuona utalifikia vipi soko la mwezi March hadi July. Hii miezi hakuna dalali atakae kunyanyasa. Na pia sio lazima upeleke mzigo sokoni kunawanunuzi wazuri tu hufuata mazao mashambani. watu wengi wanafanikiwa sana kwa kuuzia mashambani. kama huna uzoefu afadhari ukauzia shamba ukapata bei utakayoridhika nayo kuliko kwenda mjini ukakutana na madalali wajanja ukarudi kijijini na story tu huna pesa mfukoni.

Kwa hiyo Mkuu kila biashara inachangamoto zake. Tumia muda mwingi kujifunza kwa wazoefu badala ya kulalamika hivyo. Ulikosea kuanza kwa kulima pakubwa ukapata hasara ukarudia makosa yaleyale kwa kulima pakubwa zaidi huku hujarekebisha kilichokutia hasara ulipo anza. Ushauri wangu msimu wa kwanza jifunze mbinu za kilimo cha vitunguu uzijue changamoto zake. Msimu unaofuata boresha uzalishaji kwa kutatua changamoto, pata ushauri kwa wazoefu. Panua eneo kadri unavyopata uzoefu. Hata kama unauwezo mkubwakifedha usianze kuwekeza eneo kubwa kama huna uzoefu. Usivutiwe na takwimu tamu unazosikia nyingi hufikiwa na wazoefu na nyingi ni exagerated. Ukizalisha eneo dogo inakupa picha halisi itakayokufanya uamue iwapo kilimo hicho kinalipa au la. Na hapo ndiyo utaamua kupanua eneo la shamba kwa kutokana na picha halisi uliyoiona na changamoto zake.
Samahani kiongozi hilo soko la mwezi march mpaka April linakuwa zuri kwa Dar es Salaam au mikoa mingine? Asante.
 
Mimi na mwenzangu tushalima vitunguu mara moja tukafanikiwa kurudisha capital na faida juu, japo sio tulitegemea. Na tunajipanga tena. Hii kitu hii sio lelemama. Unapaswa kwenda benet nayo, kuanzia kusia, transplanting, majaruba hakikisha yanawekwa vizuri, umwagiliaji, palizi, madawa etc process zote ushuhudie, shirikisha locals majirani wenye uzoefu wakupe sifa ya udongo wako na hekari zako. Mambo ya kupiga simu, kutuma hela na kuagiza mtu akuangalizie ww upo busy na issue zingine, ninakuhakikishia utapigwa mimba. Ama la weka dogo au mtu una uhakika na yy ana machungu na huo mradi akusaidie kama upo busy sana.

Jambo jingine ninahisi hizi mvua zinazotokeaga from nowhere kipindi cha kuvuna vitunguu ni ndumba na uchawi sometimes, locals wanakuwaga na wivu design. Heard this stories na nimesoma humu. I have confirmed
Ulilimia mkoa gani kiongozi? Na gharama kwa ujumla ilikuwa kiasi gani? Asante
 
Tatizo mtu hajui abc za kilimo ila anataka nae alime ,jaman kulima sio kukwatua ardhi ni profession tumeikalia darasan tukaisoma ,hivi kama wewe ni mwanasheria,muhasibu,dereva,doctor any profession ni rahisi mtu yeyote kumuelekeza akafanya kazi yako !!!??? Jibu ndio utafahamu why kilimo ukiingia kichwa kichwa unaumia ,tumieni wataalam wa kilimo mlionao / wanaowazunguka kama mnataka kufanikiwa ndugu zanguni
Well said bro
 
nimechukua kitu hapo, ila tatizo kubwa kwa watz wakisikia kitu furani kina faida watakitenda hapo hapo ila wakishaona au kupata hasara wanakata tamaa hawajui kilimo ni timing kati ya mkulima na mkulima na mkulima na hali ya hewa usipo cheza na hvyo vitu viwili utadai kilimo ni kigumu ila kilimo kina hela kwa 7bu kimetusomesha hahahaaaaa ukikata tamaaa mi nalimaaa ili sokoni tuwe wachache.
Hapo kweli, si suala la kuumiza kichwa mteja atapatikana wapi bali ni kufanya timing kwa mzalishaji mwenzako pamoja na hali ya hewa. Maana bidhaa ikiwa adimu soko huwa juu.
 
Ndio kitunguu hakipatani na mvua haswa kikiwa kimekomaa,kikiwa kichanga hakuna shida hvyo zingatia kukilima kikomae kiangazi,pia ardhi yako iwe na matoleo ya maji maana kama.maji si ya kusimama pia hakitoharibika ,na kuna variety mfano tajirika ya east west vinavumilia maji mengi hata vikiwa vimekomaa,lazima utazame shamba kwanza .kulima eka haizidi milioni mbili kwa kila kitu yaani from kukodi shamba mpaka mavuno
Hapo unaongelea mkoa gani kiongozi? Maana nimesikia ukiwa na laki saba tu unaweza kulima heka moja na kukamilisha kila kitu.
 
Mimi napenda kuwasisitiza mambo makuu matatu katika kilimo hichi kwasababu nimeshuhudia watu wana ingizwa Chaka na kupoteza mamilioni

1. Usianze kulima kabla hujapata ABC kamili za kilimo na changamoto zake. Tembelea watu ambao wana uzoefu Kwenye kitunguu. Jua Majira ya kukilima kitunguu, jua soko lilivyo na linavyo badilika, jua mbegu bora na mahitaji ya kitunguu n.k

2. Kama Ni muajiriwa chonde chonde achana na kilimo cha whasap na simu, yaani usikae ofisini ukawa unatuma tu hela shamba, weka ratiba ya Kwenda shamba at least twice a month ukaone maendeleo

3. Hakikisha hakikisha ndugu unapata mtu mwaminifu wa kusimamia shamba masaa yote. Yani ndio awe project manager wako ambaye kazi Yake Ni kusimamia shamba lako. Awe amesha lima kitunguu au anakijua kilimo

NB: Usiwaze faida kwasasa, achana na habari za kuuliza ekari moja inatoa gunia ngapi na gunia shilingi ngapi. Target yako kwasasa iwe kujifunza hivyo anza na ekari moja au chini ya hapo.
Dah, jamaa upo vizuri wewe kwenye ushauri! Safi sana maana umetoa maarifa yako pasipo uchoyo kabisa yaani!
 
Back
Top Bottom