ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Hata mihogo mliita white gold.....Kusini hii wanaiita green gold inalipa sana.
In 2 to 3 years unavuna mpka miaka 50 na kuendelea.
Mbolea wengi huenda kuifuata kanda ya kati uko mavi ya ngombe mengi tu.
Hapa hoja ni kuwa hao wakulima wana hakika ya soko, soko la Ulaya! Hii ni kutokana na ukweli kuwa matunda yao yote au karibu yote, yaani sehemu kubwa ya mavuno yao hununuliwa na walanguzi kutoka Kenya. Hawa wana soko tayari tayari Ulaya na hususan kwa aina hiyo ya HASS! Kwa mantiki hii, nadhani kuna ulazima wa sisi Watanzania wenye kuweza kupata hizo connection za hayo masoko na tuna mtaji/pesa za kununua hayo mazao tufanye hivyo. Tusipotumia hii fursa na hivyo kuacha OMBWE, basi hao wageni wataitumia na kunufaisha maisha yao na nchi zao.Nilimsikiliza jamaa mwny Co. Ya Malembo farm kwny kipindi cha kina masudi kipanya pale clouds+ cha saa 2 usiku.
Akasema sa hivi kinacho trend huko mitandaoni/mashambani ni kilimo cha parachichi(HASS) anasema wakulima wanalima sana na wote ukiwauliza mtauzia wapi wanakwambia Ulaya,ukiwauliza Ulaya nchi ipi maana sio nchi zote tunafanya nao biashara hawana majibu,ukiwauliza mnajua ni standards gani hizo nchi za ulaya zinataka ili kununua hayo matunda wao hawana majibu ila wanakwambia tu cha msingi iwe ni aina ya HASS.
Yajayo yanafurahisha,Parachichi inaenda kua kama kilimo cha Tikitimaji.
SAWA ila usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja (Do no put all your eggs in one basket)!The higher the Supply the lower the Price.... (If Demand remains Constant)
Wabongo tujikite kwenye kufanya jambo kwa muda mrefu na kutafuta masoko ya uhakika na ku-build relationship na wanunuzi..., hili la kurukia kila kilimo linasababisha unpredictable prices...
Yaani kama wewe ni mkulima wa kahawa endelea na kahawa zako uki-build relationship na wanunuzi na kuwa na uhakika wa product yako ni sustainable in the long run...
Stick to what you Know fanya research kwenye jambo au mambo machache ambayo una passion nayo yafanye kwa uhakika consistently na long term (hata hayo masoko unayatafuta na kuya-maintain) sio chasing them everytime na kila ukifika unakuta umechelewa...SAWA ila usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja (Do no put all your eggs in one basket)!
Ni kusini nyanda za juu ama kusini ipi?Kusini hii wanaiita green gold inalipa sana.
In 2 to 3 years unavuna mpka miaka 50 na kuendelea.
Mbolea wengi huenda kuifuata kanda ya kati uko mavi ya ngombe mengi tu.
Njombe parachichi zinapandwa wakati wa mvua nyingi. Mwaka huu mwezi March nilipanda miche 1500 ilikufa mitatu tu.Inasemekana ikipandwa masika miche mingi inakauka kwa sababu kwanza mmea unakuwa haupati maji kwa mtiririko mzur, pia unakuwa haujazoea mazingira . Lakin ukipanda kiangazi ni kwamba ile interval ya kumwagilia inaufanya mmea uutengenezee tabia fulani ya kuzoea mazingira. Hata mvua ikija inakuta ushazoea hvo haufi. Labda watafiti waendelee kufanya utafiti maana naona wengi wanapanda kiangazi tofauti na miti ya kawaida
Naogopa kuwa sheria itakayokuja ni ya kulipisha wote wanaomwagilia mashamba yao.Miaka yote wanahamasisha umwagilaji ila bado sana
Inatakiwa sheria haswa sio kila leo bunge linaongea na wakirudi hakuna kinachofanyika
Ila mdogo mdogo tutafika
Naogopa kuwa sheria itakayokuja ni ya kulipisha wote wanaomwagilia mashamba yao.
Masoko yapo miaka yote ila kwa ajili ya wizara kubana sana kuhusu vibali hili ndio tatizo kubwa kwetu
Fursa ni nyingi na mazao na matunda ya kila aina yapo ila tutaishia kupeleka Kenya tu aidha kwa kificho au ki halali lakini kwa Ulaya soko wanalo wao maana sisi tumeshindwa kabisa kwa uzembe wa na roho mbaya sijui kwa Wizara husika au gov kwa ujumla
Ukiangalia supermarkets Ulaya utaona [emoji1649] zimeandikwa kuwa zimetoka SA, Kenya au Ug
Utaratibu wa kutoa vibali uangaliwe upo kwani tunapoteza fursa nyingi sana huku tukisifia sisi ndio kaka wakubwa wa EA
Nimesikia India watanunua hayo maparachihi pamoja na south africaNilimsikiliza jamaa mwny Co. Ya Malembo farm kwny kipindi cha kina masudi kipanya pale clouds+ cha saa 2 usiku.
Akasema sa hivi kinacho trend huko mitandaoni/mashambani ni kilimo cha parachichi(HASS) anasema wakulima wanalima sana na wote ukiwauliza mtauzia wapi wanakwambia Ulaya,ukiwauliza Ulaya nchi ipi maana sio nchi zote tunafanya nao biashara hawana majibu,ukiwauliza mnajua ni standards gani hizo nchi za ulaya zinataka ili kununua hayo matunda wao hawana majibu ila wanakwambia tu cha msingi iwe ni aina ya HASS.
Yajayo yanafurahisha,Parachichi inaenda kua kama kilimo cha Tikitimaji.
Hali ilivyo kuna uwezekano kukaunda ka kampuni uchwara ka kununua hayo maparachichi bongo kisha soko analikamata mwanasiasa mmoja anajipigia hela tu!Mimi naamini kotu kizuri kinaweza kuwa na changamoto fulani, lakini changamoto hizo hazipaswi kuwarudisha nyuma watu wenye mawazo ya kusonga mbele.
Ninawaomba mliotutangulia kwenye harakati hizi muwe wawazi na wakweli mtusaidie kusema changamoto halisi.
Pia mtuambie nini ushauri wenu je watu walime parachichi au waache. Na katika kila jibu njooni na namna ya msaada.
Sidhani kama maisha yangekuwa hayana changamoto tungeishia kuwa watu mbumbumbu. Changamoto ndio akili.
Na sina iman kwamba hakuna uhitaji wa parachichi , eti kwamba mashamba yaliyopo yanatosha, kama ni hvo tujuezeni.
Asanteni karibuni tuendelee kujifunza .,...