Kilio cha Walima Vanilla Kagera kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kilio cha Walima Vanilla Kagera kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Kwako Rais Wetu Mpenda.

Nianze kwa kukupa pole na majukumu yako ya kila siku, pia nikushukru jinsi unavyoongoza nchi kwa amani na utulivu. Bila kuacha kukupongeza kwa unavyopambana na miradi ya kimikakati katika kuiinua nchi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi wakulima wa vanilla Kagera tumekumbwa na tatizo kubwa sana ambalo limeleta mgogoro sana na mgongano ya masilahi. Wakulima wakagera tuliitwa tarehe 20 Mei 2022 kujadiri mstakabari wa Vanila zetu.

Waliohudhuria ni sisi wakulima pamoja na kampuni zinazonunua vanila. Pamoja na katibu tawala wa mkoa. Kikao kiliisha salama licha ya kuwa na marumbano makali juu ya uhuni unaofanywa na mkurugenzi wa MAYAWA ambao ndio wanunuzi wakuu.

Iko hivi: Mkurugenzi wa Mayawa anatuhumiwa kula njama na kuwashawishi makampuni anayoshindana nayo kutozidi kiwango fulani ili wapate faida kubwa.

Mayawa kwa kutumia makampuni mengine madogo alifanikiwa kushusha bei kilo moja kutoka tshs 32,000/= to tshs 20,000/= wakati yeye akinunua kwa tshs 30,000. Mayawa ilizidiwa wingi wa vanila ikabidi ikope Bank kutoa ADB kulipa wakulima.

Lakini bado wakulima wanadai mil. Mia mbili. Mpaka sasa ajawalipa licha ya kuambiwa na mkuu wa mkoa kwa kauli ya serikali kuwa tarehe 31 May 2022 awe amewalipa. Sasa likichofanyika ni kwamba mayawa amesusa kununua na kushawishi kampuni nyanza zilizokuwa zinanunua kwa bei nafuu nazo zikasusa.

Sasa hivi ni kampuni moja tu NEI LTD kutoka Moshi Makao Makuu ndiyo inayonunua. Kampuni hiyo nayo imezidiwa na imesitisha kwa muda. Wakulima wa sasa hawajui cha kufanya vanila mashambani zimeanza kuharibika.

Tunaiomba serikali kupitia takukuru wachunguze hii kampuni ya mayawa alafu wamuombe NEILTD aendelee kununua vanila zetu tusije kukata tamaa. Kama ikishindikana tunaomba tufunguliwe mipaka tuize Uganda kwani wao wananunua kilo moja kwa tshs 50,000/= vanila mbichi.

Mkoa wa Kagera mwaka huu unazalisha tani mia 4 jambo ambalo watunza takwimu hawana, kwa kuwa nyingi zinatoroshewa nchi za jirani kukwepa mitego ya kampuni zetu za kijanja janja. Pia kampuni kwa sasa hazifuati wakulima kwenye vituo. Hii inatokea kwa sababu ya kukwepa ushuru.

Mwaka jana tu serikali ilikuwa inadai makampuni manne tshs miliioni 20. Kama ushuru hivyo kuitisha kuwapelekea ni njia mojawapo ya kukwepa ushuru.
Mwisho nakuomba umwagize waziri wako kilimo Bashe pamoja na Katibu wake waende kuhitisha kikao cha dharura wawasikilize wakulima wanasemaje kuhusu mambo mabaya wanayotendewa kwenye hii dhahabu ya kijani.

Wako mkulima wa Vanilla Bukoba
 
Poleni sana wakulima.
Msikate tamaa mkaacha kulima vanilla.

Igeni ujanja wa watu wa Kilimanjaro, walizuiwa kupeleka mahindi Kenya, lakini wakatumia njia za panya kwa nguvu zote mpaka serikali ikaamua kuhalalisha upelekaji wa mahindi huko.

Wakati mwingine inabidi HAKI yako uipore kwa aliyeishikilia!
 
Jambo baya kwa serikali yangu ni bora ziharibike mashambani kuliko kuvusha Uganda eti... mi nashauri mchange nauli muunde kamati ndogo ya kumuona bashe it's seriously issue
Na ajabu hakuna mkoa unaongoza kwa magendo kama Kagera...

Sio kahawa sio vanilla
 
Back
Top Bottom