Kilo moja ya nyama kuuzwa 13,000 ni laana au ni nini?

Hii mizani Ya Daslam sasa, nyama bei juu, Na hapo hapo anakupiga kwenye mzani, Kg 1, anakupa 3/4....
 
Kitimoto haiwezi kuwa mbadala wa nyama ya ng'ombe! Sijawahi ona sherehe za heshima zikiandaliwa na nyama ya nguruwe
Nasikia enzi za mtume ndiyo ilikuwa mlo wa kifalme mpaka mtume akapiga marufuku kitimoto kuliwa hadharani ila mpaka siku maalum tena inaliwa na wafalme tu
 
Ulianza vizuri ila hapo mwisho umeonyesha hasira na vijana wanaomaliza chuo kwa shida zako.

Kama unaona kuna fursa changamkia then uje kuajiri hao vijana kukata majani.
Tatizo letu kama taifa hatutaki ukweli! Nimesema hali halisi kwa upande mwingine ni fursa! Shida hiko wa mkuu!
 
Kula kuku au dagaa. Chukulia kupanda Bei ya nyama Kama fursa kula vyenye afya
 

Labda Ilani ya CCM inatutaka kufuata mabaniani , kutokula nyama ya Ng`ombe labda ni mungu wa CCM pia.
 
Japo nauza elfu 9, ila bei ime panda machinjioni wazee.

Speaking as an expert, utumbo tuli kuwa tuna nunua elfu 3- kuuza elfu 4.
Sasa hivi nunua elfu 3.5 -4 - nawa ambia wauze elfu 5.

Nyama ili kuwa elfu 5 kununua, kuuza elfu 7, Sasa hivi kuuza ni elfu 9, kununua 7- 7.5

Mtu ana taka stake kwa elfu 9 hiyo hiyo, akati stake elfu 12 aisee.
 
Kula kuku au dagaa. Chukulia kupanda Bei ya nyama Kama fursa kula vyenye afya
Hivyo vyote haviwezi kuwa mbadala wa ng'ombe! Wengine watakuambia kula kula kunde! Waingereza wanaita kunde "poor man's meat". Ikiwa na maana masikini kama huwezi mudu nyama kula kunde! Huu ni upuuzi kwa nchi ksma Tanzania ya pili kwa kuwa na ng'ombe wengi! Wakati huo tuna mapoli yako tu na nguvu kazi ya vijana wanawaza ngono tu!
 
Hao vijana wanaozurura, umewaps hela za kununua hao ndama na kuishi miaka 3 hadi ndama wanenepe wakauze?
Watu wengine sijui mnawaza kutumia nini.
 
Wakati wa sikukuu ilikuwa lazima ipande, soon tu itashuka mkuu
 
kabla hujaenda mbali uliza bei ya madawa ya mifugo alafu rudi tuendelee...
 
Kiangazi itashuka mpaka 5K
 
Humu jf tumejaa matajiri hata bei iwe 20000 kwetu sawa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…