Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Bongo hatari sana...
Unakuta kagari kameshazurura kuliko mbwa koko..

Kanapigwa rangi, kanaogeshwa, kanashushwa mileage...

Anasubiriwa mteja mwenye wenge..[emoji2957][emoji2957][emoji2960][emoji2960]

Nilishawahi kusema na leo narudia, ni afadhali uagize gari Japan lenye km 1500k kuliko kununua bongo lenye km 600k
 
Hizo gari za yard siku hz wauzaji wanatembelea zile Chassis# hata mwaka. Baadhi walikua wanakosiaha wanaotaka kusafir nazo Moshi sikukuu
 
Kweli kabisa mkuu tunajipiga wenyewe tunaangalia mileage kwanza kabla ya yote, kuna mshikaji wangu wakati anatafuta gari alikuwa anataka mileage chini ya 50,000km akahangaika akapata Forester XT ina 45,000km kila tukionana anajisifia sasa hivi iko 49,000km. Nikamwambia hii michezo haamini kabisa anakwambia ajent aliyeniagizia ni shemeji yangu hawezi kunipiga.

Hizi kampuni za waswahili ni shida sana, kuna yard ukienda gari zao zimeenda mileage ila ni nzima mfano JanJapan hawana hii michezo ya kitoto.
 
Jan Japan ukikuta chombo ni chombo kweli japo km zimesonga ila isitoshe gari za toyota timeframe yake ni 400,000 kms baada ya hapo ndio unashauriwa kufanya overhaul
 
Wewe nae unajichanganya Sasa pale JanPapan mbona wapo waswahili wenzetu? Labda ungesema mtu aagize mwenyewe. Niliwahi kwenda kuuliza Mitsubishi Outlander nikaambiwa 27m TZS wakati mtandaoni mpaka kufika Bongo 16.5m TZS
 
Wewe nae unajichanganya Sasa pale JanPapan mbona wapo waswahili wenzetu? Labda ungesema mtu aagize mwenyewe. Niliwahi kwenda kuuliza Mitsubishi Outlander nikaambiwa 27m TZS wakati mtandaoni mpaka kufika Bongo 16.5m TZS
Mkuu pale Outlander wanaanzia 18 hadi 17.5m Desemba hii nilienda kuulizia japo binafsi sikuzipenda gari zao na pia huwa ni chache ikabidi niagize. Kingine management ya JanJapan sio waswahili ni wapakstan kama sikosei wabongo wapo kwenye marketing na kutemebeza watu pale yard pamoja na ufundi..
 
Mkuu uswahili umeuambatanisha na ngozi. Hao wapakistan unaowatetea waswahili pia. Au zile kobazi zinakuchanganya?
 
Mkuu uswahili umeuambatanisha na ngozi. Hao wapakistan unaowatetea waswahili pia. Au zile kobazi zinakuchanganya?
Mkuu mjadala ulikuwa kwenye mileage ya gari, hapo ndipo nilipojikita pale Jan kuna magari yanasoma hadi 200,000km ila wabongo wengi magari yanayouzwa ni chini ya 100,000km.
 
Kweli kabisa mkuu bei zinakuwa zimesimama ni mara 2 au 3 ya hizi tunazonunua hapa kwetu. Nimeona moja ina 159,000km bongo imewekwa 59,000km gari hiyo hiyo.

Ni kuwa makini tu na kufuatilia taarifa za gari kwa ukaribu hasa likiwa na mileage ndogo.
Gari ya mileage ndogo ni ya kuikagua physically kwanza, angalia siti ya dereva usawa wa paja la kulia kwake, angalia door knobs, buttons za ac, mirror na vingine, angalia kirungu cha gia, angalia pedeli zake ukiona zimechoka au zimechubuka sana jua umechezewa.
 
Shukurani kutuongezea madini Mkuu, nyingine unakuta hadi steering imechubuka ila unaambiwa ina 63k
 
Shukurani kutuongezea madini Mkuu, nyingine unakuta hadi steering imechubuka ila unaambiwa ina 63k
Sure nilisahau kutaja na steering, imechubuka imekwaruzwa na pete kila upande, kuna jamaa yangu aliwahi kupigwa tena aliagiza gari Befoward ni Ist ( BH427758) ukizigoogle hizi namba itakuja hiyo ist wame list kuwa ilikua na 6000 kms, angalia kwa umakini sana picha zake, speedometer inasoma buku 6, jamaa akashawishika akanunua.

Gari imefika bongo shoo ya kwanza ina miss za hatari ikiwashwa inatetemeka kama generator na imechoka kupita kiasi inatoa moshi mweupe .

NB. Gari ilinunuliwa mwaka jana (Kipindi gari zinakaguliwa Japani) .Sasa bas gari baada ya kuinunua zile document za Inspection report walivyo zi upload kwenye CAP, ndo zikatusanua kuwa gari ilikua na kilometer 106,000 km (paper mileage) ila kwenye actual mileage wakafuta 10 ikabaki 6000 ndo ina display ( wanasemaga ni ku cloack mileage).. ikabidi ni mueleweshe mshkaji gari kapigwa na wajapan ..angalia hiyo inspection report ya japan nime attach hapo chini..

Gari iko kwenye meli inakuja bongo tukaanza kuchapana email na beforward full kuchimbana mikwara ya kufunguliana kesi na kuikataa gari jamaa wana chomoa tu wana sema nao walinunua hivo hivo mnadani. Ikabidi jamaa aikubali tu kishingo upande baada ya kufika gari ndo alichoka zaidi na zile miss, plus pedal zimechoka, usukani umechoka, siti ya dereva kigodoro kimelala, gear lever imechubukaa ile silver .Ilikua ni balaa tu

Kwahiyo kupigwa hata nje unaweza pigwa piaa, lesson tujifunze ku pay attention to details sana , tuwe inquisitive na curious.

FOLLOW HII LINK kama itafunguka uone hiyo chuma

 

Attachments

Daaah Beforward nao hufanya huu uhuni kumbe Mkuu, ni hatari ndio maana binafsi sinunui gari kwa kuangalia mileage.

Kuna gari niliinunua hapa bongo kwenye Kampuni fulani ilikuwa inasoma 10,000Km ila kuna muda inaonekana namba ilifutwa ilikuwa na kilometer zaidi ya laki 2.
 
Watz tunapenda sana kuangalia Odo ndo maana twapigwa hapo.
Wakati muhimu ni kuangalia YOM
 
Jan wanakula gari kama lilivyo, kama linahitaji matengenezo wanakwambia kabisa
 
Ndo Michezo ya madalali
 
Sababu ni kodi kandamizi za kuingiza gari.Unakuta kodi ya gari la zero km ni zaidi ya gari lenyewe.

Ndio maana tunaendesha magari chakavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…