Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Ndo Michezo ya madalali
Nyingine imesajiliwa kwa namba BNS ila inasoma 68,000km na inetengenezwa 2002. Hivi kweli miaka 19 gari itembee km hizo sawa na wasitani wa 9.9km kwa siku Japan na Bongo.
Screenshot_20220101-220228_Instagram.jpg
 
Jan wanakula gari kama lilivyo, kama linahitaji matengenezo wanakwambia kabisa
Kabisa mkuu, kuna jamaa yangu alinunua X-Trail pale walimwambia ukweli wa mapungufu yake.
 
Bongo hatari sana...
Unakuta kagari kameshazurura kuliko mbwa koko..

Kanapigwa rangi, kanaogeshwa, kanashushwa mileage...

Anasubiriwa mteja mwenye wenge..[emoji2957][emoji2957][emoji2960][emoji2960]

Nilishawahi kusema na leo narudia, ni afadhali uagize gari Japan lenye km 1500k kuliko kununua bongo lenye km 600k
Mkuu Niliwahi kusikia kwamba bora ukanunua gari lenye 120+kms huko japan,,,, coz huwa yanafanyiwa service kubwa yakifikisha 100k km

Hapo kuna ukweli??
 
Mkuu Niliwahi kusikia kwamba bora ukanunua gari lenye 120+kms huko japan,,,, coz huwa yanafanyiwa service kubwa yakifikisha 100k km

Hapo kuna ukweli??
Hata mimi nimewahi kusikia maneno kama hayo ila sina uhakikam..binafsi niliagiza gari Japan likiwa na km 110000 na moaka sasa linakaribia km 170000....sijawahi kuligusa chochote kwenye engine zaidi ya Plugs na servise ya oil.....na ignition coil moja...
 
Nyingine imesajiliwa kwa namba BNS ila inasoma 68,000km na inetengenezwa 2002. Hivi kweli miaka 19 gari itembee km hizo sawa na wasitani wa 9.9km kwa siku Japan na Bongo.View attachment 2065498

Ndio hizi gari zimechezewa, hiyo kitu haiwezekani hata kwa akili za kulewa nitakataa..
 
gari za kibongo zimezeeshwa sana kwa kilometa za uzurulaji kapita kwenye kila aina ya njia mbovu makorongo na mabonde.. bado mtu akushuhie mileage. Muda wa kubadili timing chain/belt nani anao?
Madalali wa pale round about ya Mliman city Ni kwikwi
 
Wanajamvi habari zenu...

Nina jambo linanipa ukakasi kidogo, kuhusu haya magari yanayo uzwa na wabongo wenzetu kwenye page mbali mbali kama insta na kwingineko, ukakasi huo upo hasa kwenye uhalali wa Mileage ya gari husika au kilometa za gari linalouzwa. Japo kuna ukakasi mwingi zaidi ya mileage...

Ipo hivi gari nyingi za SUV mfano Subaru Forester, Harrier, Vanguard, Landcruiser, Dualis, na zinginezo. Gari hizi ukiziangalia kwenye mtandano Befoward. SBT, na page zingine za Japan kwa gari za bei affordable unakuta nyingi gari hizo zina kilometa nyingi kuanzia 110,000 nakuendelea. Zenye mileage ndogo lazima utakuta bei yake imesimama sana na kupelekea kushindwa kuinunua kutoka Japan

Ukija kutafuta au kuangalia hizi za Bongo [emoji23] watu wanaagiza huko Japan, wanatumia then wanaziuza kwa sababu zao mbali mbali kupitia madalali wa page za insta,zoom na kupatana, sasa hizi gari cha kushangaza zina kuwa na low mileage kupita uhalisia, mfano unakuta ina 75,000 kms, na bei anayo kuuzia ni ya kawaida tu, na gari namba ya plate sio ya muda mrefu sana, yaani namba D...,

Hapa nina wasiwasi saana kuwa hizi gari zinashushwa kilometa kwahyo tunapigwa sana,nimeweka mifano kwa picha, tusaidiane mawazo
View attachment 1800662
View attachment 1800663
View attachment 1800664
Mkuu Kuna hii jamaa kapunguza kilomita 100,000



Screenshot_2022-01-11-18-14-41-00_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg


Screenshot_2022-01-11-18-13-48-78_1c337646f29875672b5a61192b9010f9.jpg
 
Back
Top Bottom