Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Bei zao ni FOB mzee sio CIF ukiingia kichwa kichwa unapigwa kitu kizito balaa...in fact nimelinganisha na Be forward ambao wao ni CIF ni almost the same
Mkuu, kwani ile total price pale chini sio CIF?
Screenshot_20220305-174214.jpg
 
Inawezekana kaka
Ila uhakika UKIAGIZA mwenyewe Japan.
Mimi niliagiza ALLION ya 2003 ina 23,971 km (ONE OWNER)View attachment 2133117
.
Labda kama Japan wana hiyo michezo.

Ila nilivyo ichukua bandarini kila mtu alikuwa anashangaaa (Walidhani nimeitoa TOYOTA TANZANIA [emoji16]) ndani ilivyo haikuwa na doa hata kidigo.
Tena ilikuwa ya mdada maana nilikuta mambo ya kike kike ya Make-up kwenye Glove box.

Ukitaka kuagiza agiza mwenyewe yaani usiwe na papara kuna website wanauza gari tamu sana.
Sisi tumewazoea Befoward ila ukitulia kuna Website za japan unapata kitu kizuri sana.

Mkuu umewahi itumia hii website.

www.realmotor.jp

naona nayo ina magari cheap sana na km chache.nataka niagize kupitia wao
 
Nimekuja na uzi mwingine, ukiona mtu kapost chassis namba ya gari na ile gari kaiagizia Befoward.. ichukue ile chassis number kama ilivyo igoogle, ilegari itakuja kama ilivokua listed na Befoward wakati inauzwa ikague zile picha nenda mpaka kwenye picha inayoonesha odometer reading utacheka ufe.. nakupa mfano gari hii apa chini naipost.. na nnaenda kuitafuta befoward ilivokua listed. Jaman tuache ukitonga na uvivu wa kutafta maarifa mapya, haya magari tuyaagize wenyewe tu hakuna mateso yoyote unayoweza kuya pata kwa kusubiri meli ifike mwezi mmoja mpaka miwili.View attachment 1890299
Gari inauzwa na dalali wa kibongo anaandika uongo uongo. Ukiichukua hiyo chassis namba ukaweka google ngoma zinakuja kama hivi chini[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116] cheki mileage halisi ya gari, jamaa kaamua kuficha hiyo laki kasema gari ina 51000km[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]View attachment 1890301
View attachment 1890302
View attachment 1890303
View attachment 1890304
Aaaghh!!! umeshaunguza siri ya biashara za watu mjini. Ungeitumia kula mgao kwa madalali. Waki post wewe unai Google na unamfuata inbox akurushie ya soda kabla hujanyea kambi
 
Jamaa wanachezea milleage sana. Leo nimemdaka mmoja. Gari ina 156,000km yeye kasema ina 46,000km. Google don't lie nimeisaka ile gari jamaa kaikataa siyo yenyewe.... Bad enough nishailipia... Hapa nawaza nimtie mahakamani
Natamani uniuzie hiyo kesi
 
Mkuu umewahi itumia hii website.

www.realmotor.jp

naona nayo ina magari cheap sana na km chache.nataka niagize kupitia wao

Moja ya website kali sana wanauza Magari mazuri sanaaaaaaa!
Tena Bei cheee ukilinganisha na wauzaji wwngine.
Tena ukiliona gari kwenye hii website nunua haraka ndani ya muda mfupi unakuta limechukuliwa.

All the best
 
Natamani uniuzie hiyo kesi

Mkuu
Kwa utandawazi huu
Unaanzaje kumpa mtu fedha gari akuagizie?
Yaani kika kitu fanya mwenyewe chagua gari uliyoipenda lipia mwenyewe Japan na ikifika lipia ushuru mwenyewe kila kitu kwa Control number
Hela unayopa Agent haizidi 250,000/=

Hawa madalali wetu wanakuchagulia kitu chenye ubora mdogo kikifika wanarudisha nyuma kilometer unadhani umepata kumbe umepata kitu kisichoendana na fedha yako.

Watanzania wanaumizwa sana kwa hili
 
Sure nilisahau kutaja na steering, imechubuka imekwaruzwa na pete kila upande, kuna jamaa yangu aliwahi kupigwa tena aliagiza gari Befoward ni Ist ( BH427758) ukizigoogle hizi namba itakuja hiyo ist wame list kuwa ilikua na 6000 kms, angalia kwa umakini sana picha zake, speedometer inasoma buku 6, jamaa akashawishika akanunua.

Gari imefika bongo shoo ya kwanza ina miss za hatari ikiwashwa inatetemeka kama generator na imechoka kupita kiasi inatoa moshi mweupe .

NB. Gari ilinunuliwa mwaka jana (Kipindi gari zinakaguliwa Japani) .Sasa bas gari baada ya kuinunua zile document za Inspection report walivyo zi upload kwenye CAP, ndo zikatusanua kuwa gari ilikua na kilometer 106,000 km (paper mileage) ila kwenye actual mileage wakafuta 10 ikabaki 6000 ndo ina display ( wanasemaga ni ku cloack mileage).. ikabidi ni mueleweshe mshkaji gari kapigwa na wajapan ..angalia hiyo inspection report ya japan nime attach hapo chini..

Gari iko kwenye meli inakuja bongo tukaanza kuchapana email na beforward full kuchimbana mikwara ya kufunguliana kesi na kuikataa gari jamaa wana chomoa tu wana sema nao walinunua hivo hivo mnadani. Ikabidi jamaa aikubali tu kishingo upande baada ya kufika gari ndo alichoka zaidi na zile miss, plus pedal zimechoka, usukani umechoka, siti ya dereva kigodoro kimelala, gear lever imechubukaa ile silver .Ilikua ni balaa tu

Kwahiyo kupigwa hata nje unaweza pigwa piaa, lesson tujifunze ku pay attention to details sana , tuwe inquisitive na curious.

FOLLOW HII LINK kama itafunguka uone hiyo chuma

Duuh noma saana ukiangalia gari jinc ilivyo dah beforward kumbe nao wanakoseaga
 
Upo sahihi, juzi niliona IST km 28k tuu, na mshkaji wangu pia alipata gari km 7k tuu japan na bei chee. Wabongo wengi wamezoea Beforward kumbe kuna machimbo ya maana sanaaa
Tuelekezeni hayo machimbo mkuu
 
Hatari saana Toyota crown hiyo mileage imeshuswa from 119,089 km mpaka 54,000km
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
20220528_202317.jpg
Screenshot_20220528-202108_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom