Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Bei zao ni FOB mzee sio CIF ukiingia kichwa kichwa unapigwa kitu kizito balaa...in fact nimelinganisha na Be forward ambao wao ni CIF ni almost the same
Mkuu, kwani ile total price pale chini sio CIF?
 

Mkuu umewahi itumia hii website.

www.realmotor.jp

naona nayo ina magari cheap sana na km chache.nataka niagize kupitia wao
 
Aaaghh!!! umeshaunguza siri ya biashara za watu mjini. Ungeitumia kula mgao kwa madalali. Waki post wewe unai Google na unamfuata inbox akurushie ya soda kabla hujanyea kambi
 
Jamaa wanachezea milleage sana. Leo nimemdaka mmoja. Gari ina 156,000km yeye kasema ina 46,000km. Google don't lie nimeisaka ile gari jamaa kaikataa siyo yenyewe.... Bad enough nishailipia... Hapa nawaza nimtie mahakamani
Natamani uniuzie hiyo kesi
 
Mkuu umewahi itumia hii website.

www.realmotor.jp

naona nayo ina magari cheap sana na km chache.nataka niagize kupitia wao

Moja ya website kali sana wanauza Magari mazuri sanaaaaaaa!
Tena Bei cheee ukilinganisha na wauzaji wwngine.
Tena ukiliona gari kwenye hii website nunua haraka ndani ya muda mfupi unakuta limechukuliwa.

All the best
 
Natamani uniuzie hiyo kesi

Mkuu
Kwa utandawazi huu
Unaanzaje kumpa mtu fedha gari akuagizie?
Yaani kika kitu fanya mwenyewe chagua gari uliyoipenda lipia mwenyewe Japan na ikifika lipia ushuru mwenyewe kila kitu kwa Control number
Hela unayopa Agent haizidi 250,000/=

Hawa madalali wetu wanakuchagulia kitu chenye ubora mdogo kikifika wanarudisha nyuma kilometer unadhani umepata kumbe umepata kitu kisichoendana na fedha yako.

Watanzania wanaumizwa sana kwa hili
 
Duuh noma saana ukiangalia gari jinc ilivyo dah beforward kumbe nao wanakoseaga
 
Upo sahihi, juzi niliona IST km 28k tuu, na mshkaji wangu pia alipata gari km 7k tuu japan na bei chee. Wabongo wengi wamezoea Beforward kumbe kuna machimbo ya maana sanaaa
Tuelekezeni hayo machimbo mkuu
 
Hatari saana Toyota crown hiyo mileage imeshuswa from 119,089 km mpaka 54,000km
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…