Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Jamaa wanachezea milleage sana. Leo nimemdaka mmoja. Gari ina 156,000km yeye kasema ina 46,000km. Google don't lie nimeisaka ile gari jamaa kaikataa siyo yenyewe.... Bad enough nishailipia... Hapa nawaza nimtie mahakamani
Aisee hapo mtasumbuana sana kama kasha ikamata hela yako. lakini umepata pa kuanzia na pa kujifunza.
 
Bora washushe 0km tujue moja. Halafu Hawa jamaa ( madalali) wamazunguka nazo Sana bongo asubuhi wanaxipiga perfume Kama maiti
gari za kibongo zimezeeshwa sana kwa kilometa za uzurulaji kapita kwenye kila aina ya njia mbovu makorongo na mabonde.. bado mtu akushuhie mileage. Muda wa kubadili timing chain/belt nani anao?
 
Wanajamvi habari zenu...

Nina jambo linanipa ukakasi kidogo, kuhusu haya magari yanayo uzwa na wabongo wenzetu kwenye page mbali mbali kama insta na kwingineko, ukakasi huo upo hasa kwenye uhalali wa Mileage ya gari husika au kilometa za gari linalouzwa. Japo kuna ukakasi mwingi zaidi ya mileage...

Ipo hivi gari nyingi za SUV mfano Subaru Forester, Harrier, Vanguard, Landcruiser, Dualis, na zinginezo. Gari hizi ukiziangalia kwenye mtandano Befoward. SBT, na page zingine za Japan kwa gari za bei affordable unakuta nyingi gari hizo zina kilometa nyingi kuanzia 110,000 nakuendelea. Zenye mileage ndogo lazima utakuta bei yake imesimama sana na kupelekea kushindwa kuinunua kutoka Japan

Ukija kutafuta au kuangalia hizi za Bongo [emoji23] watu wanaagiza huko Japan, wanatumia then wanaziuza kwa sababu zao mbali mbali kupitia madalali wa page za insta,zoom na kupatana, sasa hizi gari cha kushangaza zina kuwa na low mileage kupita uhalisia, mfano unakuta ina 75,000 kms, na bei anayo kuuzia ni ya kawaida tu, na gari namba ya plate sio ya muda mrefu sana, yaani namba D...,

Hapa nina wasiwasi saana kuwa hizi gari zinashushwa kilometa kwahyo tunapigwa sana,nimeweka mifano kwa picha, tusaidiane mawazo
View attachment 1800662
View attachment 1800663
View attachment 1800664
Hao watakua madalali wa Round about ya Mlimani city/kanisa la kwa Kakobe jamaa wasanii Sana wale
 
We acha tu. Baadhi ya wabongo si watu wazuri.

Kwemye mwaka 2000 niliagiza gari kwa jamaa anayefanya biashara ya magari anayatoa Dubai, gari lilikuwa safi na ilikuja ikiwa na km kwenye 45,000. Gari ilipofikisha km 100,000 ile namba 1 ilikuwa imechubuliwa vibaya yaani watakuwa waliirudisha kwenye 0 ili waweze kupata hiyo 45,000 kutokana na ilo akili yangu ikaniambia hii gari ilikuwa kwenye km 145,000 wakafanya wamayojua wakairudisha 1 kuwa 0.

Dubai kwa wahuni... 😂😂😂
 
Back
Top Bottom