Kimara, Dar: Polisi wawakamata kwa uzururaji Daktari chriscyrilo na Daktari Shindo Kilawa

Kimara, Dar: Polisi wawakamata kwa uzururaji Daktari chriscyrilo na Daktari Shindo Kilawa

Kuna mtubjana alikua anashkuru wamarekani kwa kuondoa wasio julikana haya sasa ndio hao sasa wameshafanya yao.

Watanzania amkeni mtoke usingizini acheni kujifarji.
 
Habari mpya ni kuwa wameachiliwa na kuwa eti walikamatwa kwa uzululaji, madaktari?!!
Ni kuwa walikuwa wanatoka zao kazini Mloganzila ndio wakavamiwa na askari wenye SILAHA na kupelekwa kituo cha Temboni. Kwa nini silaha? Hivi kesho daktari anaweza kufanya kazi ya ziada kwa amani bila kuogopa kukamatwa uzurulaji akichelewa?
Screenshot_20200324-072452.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga na upumbavu wa Makonda umerudia Marekani njooni chukueni hii takataka huku
 
Explain,it means wasiojulika ni vyombo vya usalama?
Wewe wasema, Na inakuwaje uite vyombo vya usalama ni wasiojulikana?

Uandishi wa kijinga Sana huu, mtoa tarifa anatarifu watu wametekwa na wasiojulikana halafu yeye hiyohuyo anahitimsha kwamba walikuwa kituo cha police na wameachiwa!

Pamba..Fu kabisa
 
Wasio julikana wameshawahi kumteka mwana ccm japo mmoja au wapinzani tu?


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hii habari haina maana bila kutupatia kidogo historia ya hawa madaktari.

Kuna madaktari wangapi nchi hii?Kwa nini wao?Au siku hizi watu wenye silaha wamekuwa vichaa?Wanateka tu?Kwa nini wao?

Na kama walikuwa wanacheza na mke wa kigogo au mchepuko wake utarajie vitu kama hivyo kutokea!Au pengine ni wanaharakati wa siasa?

Kama ni wanasiasa,hiyo ni haki yao kama walivyo akina Kigwangala,na kwa hiyo sitaunga mkono kwa wao kufanyiwa kitendo hicho.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Doctor Anasema Ulale Sana Upumzishe Mwili Wako Afya Iwe Njema. Serikali/Mwajiri Anasema Kulala Sana Yaani Usingizi Ni Uzembe.

Kutembea Muda Wowote Wakati Wowote Siyo Kosa Endapo Una Sababu Za Muhimu Ila Sasa Hivi Ndiyo Hivyo
 
Hivi huu utaratibu wa kukamatana bila kuambiwa kosa, kupitia serikali ya mtaa, bila ya taarifa ya kuitwa polisi au mahakamani ni utaratibu wa askari wa Tanzania pekee? Sheria inasemaje kwani wakikuhitaji kwenda polisi either kwa mahojiano au vyovyote vile?
Mtu anajulikana kituo Cha kazi anachofanyia kazi wanaanzaje kumkamata Kama jambazi kwanini wasitumie utaratibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo ya hovyo sana,hii ndiyo tunasema unamnyima raia haki yake ya kuishi.
Waachieni Ma Dr waje wasaidie kupambana na Corona.
 
Hii nchi inamaajabu mengi Sana, msomi na mjinga huwezi kuwatofautisha, inawezekanaje mtu tunayemuona angalau alimaliza darasa la saba anaandika tarifa ya watu kutekwa na wasiojulikana

Halafu hiyohuyo ndani ya tarifa zake hizo anahitimisha kuwa watu waliokuwa wametekwa na wasiojulikana Wapo kituoni na wameachiwa, hatuoni kwamba huo ni uduni wa mtoa tarifa?
 
Fumbo mfumbie mjinga...
Hii nchi inamaajabu mengi Sana, msomi na mjinga huwezi kuwatofautisha, inawezekanaje mtu tunayemuona angalau alimaliza darasa la saba anaandika tarifa ya watu kutekwa na wasiojulikana

Halafu hiyohuyo ndani ya tarifa zake hizo anahitimisha kuwa watu waliokuwa wametekwa na wasiojulikana Wapo kituoni na wameachiwa, hatuoni kwamba huo ni uduni wa mtoa tarifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani walikuwa na vitambulisho au walijitambulisha ? Ni mhimu kutembea na vitambulisho haswa usiku.
Nakumbuka mwaka Jana nilikuwa natoka songea nimefika iringa saa 6 nikaanza kutafuta lodge wajomba wakanikamata kuwaonesha kitambulisho wakaniachia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom