Tokea hotuba za uapisho, tumeambiwa waandamanaji na wahamasishaji hawakuwa Watanzania.
Na baadae maafande wa polisi na wasemaji wa serikali na makada wa chama wamekuwa wakiiga na wakurudia maneno hayo. Sasa kimeumania mahakamani.
Charge sheet ya Niffer na wapanga uhaini wenzie 147 haijataja utaifa wa washitakiwa.
Kijamii, hawara hawezi kukamatwa ugoni. Hawara hawezi kuwa na kesi ya ku chiti, kwa saab hana kiapo cha uaminifu na wewe, hujatoa mahari, hujatoa kishika uchumba, hujatoa chochote.
Kisheria na Kikatiba, Mkenya, Mnyasa, Mmarekani, Mchina, na Mganda, hawawezi kufanya uhaini Tanzania. Hawana kifungo cha uaminifu, hawana allegiance kwa Tanzania. Watafutie kesi nyingine.
Sasa mawakili wa wahaini hawa wameweka pingamizi wakiitaka serikali itaje uraia wao. Wamesema tuanzie hapo kwanza. Hawa kina Niffer wametokea wapiiiiiii ? Serikali imeiomba mahakama irudi Jumatatu kujibu.
Ndio tutajua tuomboleze vifo vya Watanzania wale na kuwazika kwa heshma, au twende na kauli ya Rais kwamba wale si Watanzania na tufute kesi ya uhaini.