Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo wote!
Lema anahaki ya kuongea atakachoongea. Kulingana na maoni yake yanayoendeshwa na uelewa wake, maslahi yake na na muono wake. Hiyo ni haki yake.
Lakini Lema atafanya Kosa la kiufundi ikiwa atadhani anaushawishi ndani ya CHADEMA.
Huo ushawishi hana.
LEMA ajue Chadema ndio inayombeba Yeye na sio Yeye anaibeba CHADEMA.
Uwezo wake ni wakawaida ingawaje alikuwa anajuhudi na bidii kubwa. Hilo ni jambo la kumpongeza.
Mtu pekee ambaye anaushawishi mkubwa ndani ya CHADEMA ni Tundu Antipas Lissu. Na hii ni kutokana na character yake, uwezo wa akili, na elimu yake.
Yeyote atakayeondoka CHADEMA ajue hataleta madhara yoyote Makubwa.
Kwenye siasa kuna mambo mawili makubwa ambayo mtu akiwa nayo tunasema huyu ananguvu ndani ya chama Husika;
a) Nguvu ya Ushawishi.
Inaitwa Charismatic Leadership.
b) Nguvu ya Fedha.
Hapo kwenye Nguvu ya Ushawishi ndipo anapoangukia Tundu Antipas Lissu.
Lissu hana pesa lakini ana nguvu ya ushawishi. Anauwezo mzuri wa kujieleza na kushawishi watu, anaupeo mkubwa, anajiamini sana kiasi kwamba yeyote anayesimama mbele yake anamuweka level moja na watu wengine.
Nguvu ya Pili ni Pesa. Hii walikuwa nayo Kina Lowasa, na Hata Mbowe anaingia kundi hili.
Mbowe ukubwa wake ni kutokana
na mambo makuu mawili;
Mosi, kukita mizizi zaidi ya miaka 20 hali iliyompa nguvu ya uzoefu, kuweka mifumo yake, na kujijenga kisiasa na kiuchumi.
Pili, Pesa. Mbowe sio Maskini. Yeye mwenyewe anakuambia sio mbangaizaji. Hivyo nguvu yake kubwa ipo hayo maeneo mawili.
Ushawishi wake upo kwa vijana wake aliowaweka na kuwawezesha kimaisha..
Ndio maana siku anakabiliana na Tundu Lissu tangu siku ya kwanza nilisema Mbowe hatatoboa. Kwa sababu nilijua kuwa Pesa haijawahi kushinda Mapenzi(Upendo).
Sasa Lema anapojichanganya akidhani akiondoka basi chama kitatikisika basi itakuwa imekula kwake kwa kiwango cha kutosha tuu. Kwa sababu CHADEMA haimtegemei LEMA.
Alafu Hata akisema Aende CCM bado potentiality yake sio kubwa ukilinganisha na waliopo CCM.
CCM inahitaji watu kama kina Tundu Lissu,
Tukija kwa Heche, huyu ni kiongozi mzuri lakini kiuwezo bado sana. Ndio maana hata kwenye kesi ya Lissu mliona alivyoonyesha uwezo wa kawaida tofauti na ilivyotarajiwa.
Angalau John Mnyika.
Mbowe kihoja anajua kutoa hoja. Lakini kinachomponza Mbowe ni kwamba yeye ni mfanyabiashara. Na ukiwa mfanyabiashara kanuni namba moja kabisa ni Kuangalia faida. Kanuni namba mbili ni Never Fight the State.
Pamoja na hayo, bado Lema ni kiongozi mzuri na aliyeonyesha mchango wake kiasi kikubwa. Kwa uwezo aliobarikiwa. Hivyo sisemi hana mchango. Au hana faida. Nope!
Nazungumzia ule ushawishi ambao akiondoka Gap la wazi na pigo kwa CHADEMA litaonekana.
Kingine, Lema ameongea mambo mengi mazuri lakini kuonyesha nia ya kukata tamaa, na kujiunga na Watesi, wauaji, na watekaji aliokuwa anaamnisha watu ni jambo ambalo limekera wengi.
Hakuwa na sababu ya kuita press kuelezea kukata tamaa kwake. Kushindwa kwake.
Press yake ingeishia pale alipokuwa anasema CHADEMA haitapokea na haiendeshwi kwa maneno ya wanaharakati na watu wa mitandaoni. Hiyo ni hoja.
Pili, Kujitetea uhuru wake wa kuchangamana na kuchagua marafiki iwe wa CCM, iwe mapolisi, iwe ACT iwe waokota makopo. Iwe nani. Hiyo ni haki yake. Na ni hoja.
Tatu, Kuwakosoa wale wanaharakati wanaotaka wao ndio mawazo yao yaonekane bora na kuwakejeli wengine na kuwapangia wengine chakuwaza na upande wa kuwa. Hii ni hoja.
Nne, kwa kuwaonya nakuwakemea wenye mawazo potofu kwamba kutukana mitandaoni au ukiwa uhamisho umejificha sio ujasiri wala ushujaa kuwazidi waliobaki wanaokosoa kwa Busara na kuangalia Mustapha. Hii Lema kaongea Hoja.
Ni kweli, huwezi jificha alafu ukajifanya wewe ni jasiri na mbabe kisha kuwazodoa ambao hawajajificha kama wewe,ukiwaambia ni waoga.
Wewe kama ni Jasiri njoo live, tukana.
Wapo watu wapo humuhumu Tanzania wanafanya kile wanachofanya kina Mange, na wanaharakati wengine. Wapo!
Yupo Tundu Lisu ambaye Viunga na kona zote za usalama nchi hii jina lake lipo. Kwa ukorofi na usumbufu wake. Huyo ndiye unaweza kumuita jasiri.
Yupo Mdude Chadema. Huyo katekwa zaidi ya mara moja. Na aliendelea alipoishia. Huyo unaweza kumuita jasiri.
Lema alikuwa na hoja nzuri. Kwamba watu wasilinganishane au kuringishiana ujasiri. Kwamba mimi ninafanya zaidi ya wengine. Kila mmoja afanye kwa sehemu yake, kwa uwezo wake, kwa mazingira yake. Lengo likiwa kuifanya Tanzania iwe Nchi bora.
Nimemaliza!
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam