Kimuhemuhe cha umiliki wa Gari ya kwanza

Nasisi tunapenda mkuu, ila mimi na huu uoga huwa nawaza hivi hii Dar hizi vurugu ntaweza kweli kuendesha, naonaga watu wote wako rough barabarani [emoji23]
Unazoea tu. Ukishapigwa pasi na daladala mara kadhaa unakuwa mzoefu
 
Ukiizoea unaona kawaida..japo mhaho unasaidiaa kuendeleza matunzo

Hadi kesho kuazimisha gari siwezi...nikimpa basi kwa shingo upande sn..siamini atajali kama mimi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kabisa yaani hapo jamaa hata ungemwambia nipeleke wapi anakupeleka sharti ni aendeshe yeye sio wewe uendeshe na hata akikuachia uendeshe atatafuta sababu msimame sehemu halafu mkiwa mnarudi kwenye gari anaomba ufunguo wake ili aendeshe.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dah aisee
 
Km kitu siwezi ni kuosha gari mwenyewe uwiii sijawahi..

I used to kupeleka twice..ubize naishia wash once a week
 
Hapo jamaa anajiuliza huyu jamaa sijui nimuombe aniuzie.
 
Nimecheka sana huu uzi.
Ila ukweli kumiliki gari ya kwanza raha sana. Nakumbuka ile nimenunua kigari changu nampitia mwana tukale bata, ile tunatoka ananiambia sijawahi kuendesha hii gari yako, niachie kidogo niisikie. Aloo nakwambia nilitamani kupasuka ila ndo hivyo nikamwachia lakini simwamini nataman tufike haraka.

Kingine kuna wale akifungua gari anabamiza mlango kwa nguvu; nilikuwa najaa upepo natamani kuwagombeza ila unaona utaharibu mahusiano.
 
Gari yenye flava ya kununua mwenyewe jmn

Unaona bidii yako..za kununuliwa au kupewa raha ila si km ya kununua mwenyewe
 
The negative side of being born with a silver spoon
Taking things for granted
Thamani ya kitu hujaigharamia

And kuna tofauti though kujua kuendesha ukiwa mdogo vs actually owning a car...eitherways self purchase ya gari ina raha sana si km la kupewa
 
Ile siku nakumbuka sikupata usingiz kabisa

Nikiwa chumban kwangu nilikua nasikiliza vitu viwili tu

1.vishindo vya watu kutembea (hapa nilikua nahisi wezi wananyatia waondoke na usafiri wangu)

2. Mtikisiko wa geti. ( Hapa nilikua makini sana, nikua najua wezi ni wajanja Sana wanaweza kufungua geti pole pole na wakaiba gari langu.
 
Siku nikipata uwezo navuta subaru legacy..
Kwanza nitabadilisha ID, Badala ya miquel, itakaa S.legacy
Then avatar itatulia picha ya chuma.
Halaf Kila nitakachokiona kigeni kwangu, ntakuja humu kufungua uzi.... Kila siku thread zangu ztakuwa za Subaru Legacy...
Mengine tutaambizana siku chuma kikiwa bandarini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…