Kimuhemuhe cha umiliki wa Gari ya kwanza

Kimuhemuhe cha umiliki wa Gari ya kwanza

Nasisi tunapenda mkuu, ila mimi na huu uoga huwa nawaza hivi hii Dar hizi vurugu ntaweza kweli kuendesha, naonaga watu wote wako rough barabarani [emoji23]
Unazoea tu. Ukishapigwa pasi na daladala mara kadhaa unakuwa mzoefu
 
Ukiizoea unaona kawaida..japo mhaho unasaidiaa kuendeleza matunzo

Hadi kesho kuazimisha gari siwezi...nikimpa basi kwa shingo upande sn..siamini atajali kama mimi
 
Hiyo namba 11..
Kuna jamaa yangu mara ya kwanza kumiliki gari alikuwa hatulii, kila muda anakuwa na safari tu.
Alikuwa anaamka hata saa 6 usiku anaingia road na atarudi hata saa 8
Kuna muda alikuwa anaweza akatoka Kinondoni akaenda hata Tegeta ukimuuliza vipi tena Kuna issue gani huko, anakuambia ameenda kula msosi[emoji1] wakati sehemu za chakula zimejaa Kinondoni.
Ni kawaida ni wenge Fulani ambalo kila mtu anayemiliki kitu kwa mara ya kwanza anaweza kuwa nalo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kabisa yaani hapo jamaa hata ungemwambia nipeleke wapi anakupeleka sharti ni aendeshe yeye sio wewe uendeshe na hata akikuachia uendeshe atatafuta sababu msimame sehemu halafu mkiwa mnarudi kwenye gari anaomba ufunguo wake ili aendeshe.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dah aisee
 
😀😀😀Umenipeleka mbali kichizi 2009 gar yangu ya kwanza ni raum ile old model,T 702 ATR hapo bado nlikuwa naishi home kwa wazazi, kila siku ilikuwa ugomvi na maza nakausha ukoka kwa kuoshea gari hapo kila siku lazima
Ipigwe kiwi
Lakini hata sasa sijaacha hiyo tabia, gar yangu iko mng'aro daily na naosha mwenyewe sijui car wash
Km kitu siwezi ni kuosha gari mwenyewe uwiii sijawahi..

I used to kupeleka twice..ubize naishia wash once a week
 
Mimi nilinunua ka vitz old model no B ,ndo kalikuwa kangu ka kwanza ...

kalitunzwa mpka aloniuuzia ananiuliza ndo hiii gar niliokuuzia au??[emoji23][emoji23][emoji23]

Aisee car wash sana tu...wese fulu mno

Hata akija mshikaji ntampeleka ppte

ni ujinga but its natural being
Hapo jamaa anajiuliza huyu jamaa sijui nimuombe aniuzie.
 
Nimecheka sana huu uzi.
Ila ukweli kumiliki gari ya kwanza raha sana. Nakumbuka ile nimenunua kigari changu nampitia mwana tukale bata, ile tunatoka ananiambia sijawahi kuendesha hii gari yako, niachie kidogo niisikie. Aloo nakwambia nilitamani kupasuka ila ndo hivyo nikamwachia lakini simwamini nataman tufike haraka.

Kingine kuna wale akifungua gari anabamiza mlango kwa nguvu; nilikuwa najaa upepo natamani kuwagombeza ila unaona utaharibu mahusiano.
 
Ndo maana wazungu wana utamaduni watoto wao wakitimiza miaka 16 anampeleka driving school. Akipata leseni mzazi anamnunulia mtoto gari ya kuanzia maisha.
Ile inawasaidia vijana kuwa confidence kumiliki na kutumia gari kwa utulivu. Yaani akija nunua gari anakuwa very confident kuitumia na comfortable.

Bongo mzee akununulie gari sijui labda awe ni kibopa au tajiri sana.
Gari yenye flava ya kununua mwenyewe jmn

Unaona bidii yako..za kununuliwa au kupewa raha ila si km ya kununua mwenyewe
 
To be honest I was wondering!, How that possible!?, ulipoandika hivi ndo nikaelewa kumbe, when you start driving at early age, huwezi kua hivyo bcoz owning a car inakua kitu cha kawaida sana, tho unakua happy ku own your dream car lakin not that much😆..... by the way I started driving at 15 years na nilikua naend popote napotaka, some of my friends walikua wanaenda secondary school na gari, so today..even if niki own Buggati I don't think nitakua hivyo, zaidi yakuwa proud of myself to own a such expensive car in the world. Sijui kwann Mimi huwa I get bored easily naweza furahia kitu kwa muda mchache sana after that naona kawaida ama nisione thamani yake tena 😟 so sad.
The negative side of being born with a silver spoon
Taking things for granted
Thamani ya kitu hujaigharamia

And kuna tofauti though kujua kuendesha ukiwa mdogo vs actually owning a car...eitherways self purchase ya gari ina raha sana si km la kupewa
 
Ile siku nakumbuka sikupata usingiz kabisa

Nikiwa chumban kwangu nilikua nasikiliza vitu viwili tu

1.vishindo vya watu kutembea (hapa nilikua nahisi wezi wananyatia waondoke na usafiri wangu)

2. Mtikisiko wa geti. ( Hapa nilikua makini sana, nikua najua wezi ni wajanja Sana wanaweza kufungua geti pole pole na wakaiba gari langu.
 
Siku nikipata uwezo navuta subaru legacy..
Kwanza nitabadilisha ID, Badala ya miquel, itakaa S.legacy
Then avatar itatulia picha ya chuma.
Halaf Kila nitakachokiona kigeni kwangu, ntakuja humu kufungua uzi.... Kila siku thread zangu ztakuwa za Subaru Legacy...
Mengine tutaambizana siku chuma kikiwa bandarini.
 
Back
Top Bottom