Kimuhemuhe cha umiliki wa Gari ya kwanza

Kimuhemuhe cha umiliki wa Gari ya kwanza

Ukiizoea unaona kawaida..japo mhaho unasaidiaa kuendeleza matunzo

Hadi kesho kuazimisha gari siwezi...nikimpa basi kwa shingo upande sn..siamini atajali kama mimi
Miezi sita ya kwanza nakuwa busy sana ni ngumu mtu kuigusa maana inakuwa imeshikana na roho.
 
Nimecheka sana huu uzi.
Ila ukweli kumiliki gari ya kwanza raha sana. Nakumbuka ile nimenunua kigari changu nampitia mwana tukale bata, ile tunatoka ananiambia sijawahi kuendesha hii gari yako, niachie kidogo niisikie. Aloo nakwambia nilitamani kupasuka ila ndo hivyo nikamwachia lakini simwamini nataman tufike haraka.

Kingine kuna wale akifungua gari anabamiza mlango kwa nguvu; nilikuwa najaa upepo natamani kuwagombeza ila unaona utaharibu mahusiano.
Ha ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah hii kitu nilisahau. Unakuta mtu anabamiza mlango kwa nguvu kama niko pekee yangu ntaachia tusi hilo kutoa hasira kifuani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
The negative side of being born with a silver spoon
Taking things for granted
Thamani ya kitu hujaigharamia

And kuna tofauti though kujua kuendesha ukiwa mdogo vs actually owning a car...eitherways self purchase ya gari ina raha sana si km la kupewa
Kabisa yaani.
 
Ile siku nakumbuka sikupata usingiz kabisa

Nikiwa chumban kwangu nilikua nasikiliza vitu viwili tu

1.vishindo vya watu kutembea (hapa nilikua nahisi wezi wananyatia waondoke na usafiri wangu)

2. Mtikisiko wa geti. ( Hapa nilikua makini sana, nikua najua wezi ni wajanja Sana wanaweza kufungua geti pole pole na wakaiba gari langu.
Usiombe ununue gari halafu uishi sehemu hakuna uzio, hautalala. Kuna jamaa alikuwa anapaki gari kwa wazazi wake mtaa upo vema, hautoki geti kali mataa kila kona na walinzi kila nyumba.

Yeye anapoishi anakwenda na daladala ila ni mwendo mfupi sana wa kama kilometers nne kasoro.
 
[emoji23][emoji23]Dah iyo namba 6 yan adi paka hutaki aliguse...

Mim nakumbuka mzee wangu aliliosha maji kama nusu tank la lita 2000 sabuni yote ya bafuni aliimaliza alafu chaajabu gari yenyewe ilikuwa PASSO, dah aisee tumetoka mbali
 
Nunua afu utajua ni korosho au ni karanga lol
Tena anaweza kuwa mtata kama kuna mzee huyo alinunua nissan hard body kipindi zinatoka. Yakwake ilikuwa kali balaa. Sasa alikuwa anapita mtaani kuna madogo wanacheza mpira m'moja akabutua ukapiga kioo ila hakikuvunjika.

Mzee alishuka amechanganyikiwa madogo wakatawanyika. Akaenda akarudi tena akaulizia dogo aliepiga mpira ni nani, madogo wakamchoma mwenzao mzee akawaambia wapande wampeleke kwa huyo dogo.

Mzee walifika na akaonana na mzazi wa yule dogo dah dogo alichezea stiki kwa mshua wake.

Mzee kiroho kikasuuzika .
 
Siku nikipata uwezo navuta subaru legacy..
Kwanza nitabadilisha ID, Badala ya miquel, itakaa S.legacy
Then avatar itatulia picha ya chuma.
Halaf Kila nitakachokiona kigeni kwangu, ntakuja humu kufungua uzi.... Kila siku thread zangu ztakuwa za Subaru Legacy...
Mengine tutaambizana siku chuma kikiwa bandarini.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah tutakoma aisee.
 
The real deal....

Umenifanya nikumbuke ndoto ya kuja kusukuma Chevy Camaro...sisi watu wa mimbio kuna gari unatamani uwe nayo na siku unaendesha barabara iwe wazi kama anapita Mama Samia [emoji16][emoji16]
Ujiandae mpunga tu. Hiyo gari si mchezo. Kuanzia bei na hadi wese. Ila spear unapata dubai. Na kufunga itabidi utafute fundi mzuri.
 
Daaah, kuna vitu ukivipata mtoto wa kiume ukiwa na miaka 20's dunia lazima isimame mazee....
1. Mkataba wa kwanza wa kazi na mshahara wa kwanza,
2. Gari ya kwanza uliyonunua mwenyewe, (Kitu kama Ford Ranger hivi [emoji38] )
3. Nyumba uliyoijenga kwa jasho lako mwenyewe,

The benefits that come with these vanities, usipokuwa makini vinaweza kukufanya tukupoteze kabisa.......!! [emoji1787]
Ila katika vyoote aliyesema gari ni UCHAWI WA MZUNGU wala hakudangaya.......
True kabisa.
 
[emoji23][emoji23]Dah iyo namba 6 yan adi paka hutaki aliguse...

Mim nakumbuka mzee wangu aliliosha maji kama nusu tank la lita 2000 sabuni yote ya bafuni aliimaliza alafu chaajabu gari yenyewe ilikuwa PASSO, dah aisee tumetoka mbali
Loh. Mzee wako nae kazidi passo ndoo moja kubwa inatosha.
 
Unajua watu hawajui kuwa mzungu alishakaa akatathimini mapungufu ya manual ndipo akaona kipengele cha manual clutch kitolewe na hilo jukumu lifanywe na computer automatically.

Manual kuendesha kama mzembe utakaanga sana zile clutch plates, kwenye foleni ya Dar utajuta, maana ni bumper to bumper, safari za mbali ndio hivyo lazima uwe attention muda wote sababu gari inaingiza gear kwa kutumia akili yako na sio computer.

Sasa madereva wa safari ndefu akishachoka sehemu za hatari kuzingua ni dakika tano tu.

Wacha waseme ila Automatic ni transmission nzuri zaidi na rafiki kwa madereva. Siku hizi hadi wanawake tunagombania nao foleni ya leseni tofauti na zamani ukienda kuchukua leseni leo leo unarudi nayo hakuna foleni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nimeendesha manual transmission more than four years sijawahi kuumwa kiuno wala kukaanga clutch plate. Ni gari safi sana hasa safari ndefu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji2] Asee umenikumbusha mbali sana, kaka yangu aliponunua gari yake ya kwanza (Noah) aisee ilikua ni burudan. Ile Noah ilikua inapendwa kuliko mke[emoji1787][emoji1787]. Ile Noah masaa yote vioo havifunguliwi, haijawah kua na mafuta chini ya robo tank. Kuhusu kuiosha ndo usiseme, adi NUT za kufunga tyre zilishika kutu.

Japokua nilikua nimeshafikisha umri wa ku drive lakn ile Noah sikuwah kupewa, njia pekee niliendesha ile Noah tena ni mara moja, niliiba.

Nilivizia kaenda safr na nkachora ramani funguo inapofichwa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji39][emoji1787]. Aisee nilikula misele mbaya[emoji1787] ilikua ndo mara yangu ya kwanza kukimbiza gari juu ya 160 KM/H
Hehe hehe shukuru mungu tu hukula mzinga ungenyongwa[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom