Msamaha ni jambo zuri sana, lakini hapa tuangalie maslahi mapana ya Taifa pamoja na Chama, akina Halima waliweka maslahi yao mbele na sio maslahi ya chama
Ina maana hawawezi kuvumilia maisha ya uanachama wa kawaida na mapambano nje ya bunge?
Na kwa nini hawakusubiri ridhaa ya chama? Hii sio ndoa BAK useme tusameheane tulee watoto
Wananchi wenye imani na chadema walipata faraja baada ya chama kuchukua hatua za kuwafukuza akina halima la sivyo hata mimi singekua na imani tena na chadema
Halafu, kilichonihuzunisha ni kwamba Bulaya alikana mpaka mwisho, mipango yote ya usaliti wameifanya kwa siri na wameshirikiana na watesi wa wapinzani
Ndugai keeps attacking Mbowe and Chadema kwa sababu anapata nguvu kutoka kwa hao covid 19, mateso ambayo chadema imepitia kwenye utawala huu yametokana na ccm, sikutegemea kabisa kama mwanachama mwenye akili anaweza kuungana na watesi for her personal gain, akina halima wametesqa na utawala huu lakini wamepata nguvu ya kuungana nao kwa sababu wanataka pesa za ubunge
Hawafai kuwa viongozi wa chadema na hawaaminiki, who knows, labda watasamehewa halafu next year watapanda dau tena, chadema isilambe matapishi, isonge mbele na wale ambao wako tayari kukipigania chama kabla ya maslahi yao binafsi