Tuliwakashifu sana akina Mdee, Bulaya na Matiko, ila kwa Mambo ya ndani ya hawa akina Newton na Minja huenda akina Mdee wakawa na nafuu.
Wewe lazima utakuwa mtu wa Mataga jinsi unavyotia uchonganishi!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuliwakashifu sana akina Mdee, Bulaya na Matiko, ila kwa Mambo ya ndani ya hawa akina Newton na Minja huenda akina Mdee wakawa na nafuu.
Ninaendelea Kusisitiza ya hawa Wawili Hilda na Devotha yawezekana tukianikiwa yao hapa tutaandamana kwenda Kuwaomba Radhi akina Mdee.Wewe lazima utakuwa mtu wa Mataga jinsi unavyotia uchonganishi!!
Hawapaswi hata kupewa nafasi nyingine, wamekisaliti chama wakati ambao chama kikiwahitaji, wananchi walitegemea kuwaona wanasimama nao kwa hali na mali, na mbaya zaidi wamesaliti wakati ambao watu wana maumivu ya matokeo ya uchaguzi,watu wamepoteza maisha kwa sababu yao na watu wamefanya kila aina ya sacrifice ili kuhakikisha chadema inasimama, No second Chance, misingi na misimamo ya chama iheshimiwe, wao sio wa kwanza kufukuzwa na hawatakuwa wa mwisho, chadema bado itaendelea kuwa strong
Ninaendelea Kusisitiza ya hawa Wawili Hilda na Devotha yawezekana tukianikiwa yao hapa tutaandamana kwenda Kuwaomba Radhi akina Mdee.
I'll not go that far.Now you’re talking Mkuu. That was my point that some in this group should be given another chance if they are ready to accept their mistakes. Even Mdee she was very loyal to the party and its leaders for so long. She can be under probation let’s say for 24 months.
Mama Amon tenaaaa.Haya mambo yatapita tu kama yalivyopita mengine.View attachment 1664064
Mnyukano wa kugombania madaraka ndani ya Chadema sasa umethibitika. Tayari Hilda Newton na Devotha Minja wameanza kukinyemelea kiti cha Halima Mdee Bawacha. Wanafanya kila mbinu kuhakikisha kwamba Mdee na wenzake hawarudi. Wanatumia nguvu kubwa kupamba na kundi la kina Mdee kuliko nguvu ambayo imewahi kutumika kupambana na chama tawala cha CCM.
Juzi 29 Desemba 2020, Hilda Newton aliandika meseji ya twitter ifuatayo: "Aliyewaandikia Barua za rufaa Mzee Halima na wenzake Mungu anamuona yani maelezo yao wote yanafanana cha tofauto ni sahihi tu."
Anachosahau Hilda Newton ni kwamba, hata barua za tuhuma kwenda kwa kina Mdee zote zinafanana isipokuwa sahihi pekee!
Na hapo awali, Devotha Minja aliongoza maandamano ya kuilazimisha Kamati Kuu kuwafukuza kina Mdee. Maandamano hayo yalichukuliwa na kamera kama ifuatavyo:
Kwa hiyo sasa, BAWACHA imemeguka katika sehemu mbili: Bavicha ya Mdee na Bavicha ya kina Hilda. Hii maana yake ni kwamba, sasa Baraza Kuu linayo kazi ya ziada.
Linapaswa kuhakikisha kwamba BAWACHA inasimama kwa kutenda haki bila kuzingatia shinikizo lolote. Hoja zilizo katika rufaa ya kina Mdee ni nzito.
"Kuwabatiza majina mabaya kina Mdee, kama vile COVID19 na mengine hakusaidii kumaliza tatizo. Badala yake kunazidi kuongeza mpasuko ndani ya Chadema. Kwa hakika mie naona kuwa kina Hilda na Devotha ni hatari kuliko kinachoitwa covid19. Nashauri tangu sasa tuwaite kina Hilda na Devotha covid19+," alisema mwana Chadema mmoja kwenye kundi moja la whatsapp.
Nao wajumbe kadhaa katika kundi jingine la whatsapp wameonekana wakiandika maneno yanayofanana na hayo.
Mmoja anasema:
"Ninachojua kuna kina mama wa Bawacha walitaka kwenda Bungeni ila baada ya majina yao kutokuwemo kwenye list ya Halima, sasa hivi ndio vinara wa kushambulia waliokwenda kuapa kwa hoja eti wamesaliti chama."
Mwingine anaandika hivi:
"Ndio maan nasema haya mambo yaacheni tukutane nao kwenye vikao. Tutaelewana vizuri huko kwenye vikao. Hapa mtararuana bure. Haisaidii."
Mchangiaji wa tatu anasema:
"Katika suala ka kupeleka wabunge wa viti maalum Bawacha hhaikuwa na mpango wa kususia nawaambieni. Haya mengine tumshukuru Mungu nafasi zimekuwa chache. Wamegawanyika na hapo ndipo tulipoponea kama chama. Vinginevyo hawa akina Mama walikuwa wamoja before."
Hii maana yake ni kwamba, kelele za kina Hilda na Devotha ni kama kelele za sungura aliyesusa ndizi mbivu kwa kisingizio kwamba ni mbichi. Alikuwa ameshindwa kukwea na kuzifikia.
Baraza Kuu la Taifa la Chadema litapaswa kuyazingatia haya yote kusudu liweze kuwatendea haki covid19 bila kuwapendelea covid19+.
Hakuna shida bora nyumba yenye paaNdiyo mjue COVID19 kwamba usaliti haulipi. Rafiki yako Mama Mdee ndiyo kishapigwa chini sasa mjiandae rasmi wasaliti nyinyi mnaenda wapi kuendeleza usaliti wenu.
ACT Wasaliti kwa Zitto au maccm kwa wahuni, wezi, mafisadi na wauaji maccm. Vinginevyo msamaha wenu unakaribishwa ili mrudishwe kundini.
Inanikumbusha Uchaguzi wa Serkali za Mitaa CHADEMA walienguliwa mamya kwa makosa yale yale kujirudirudia. Waingereza wangesema Chadema want to eat their cake and to have it at the same time, yaani sheria hiyohiyo waitumie kuwafukuza Mashujaa-19 lakini sheria hiyohiyo walilalamika Tume walipoitumia kuwaengua. Halafu naona sahihi ya Katibu Mkuu Mnyika ni mkorokorogo tu, imechorwachorwa tu, si sahihi makini inayoweza kubalika kibenki. I bet hawezi kuirudia, ndiyo maana anaikataaBarua ya kutoka Chadema kwenda Covid19 kufanana ni sawa kwasababu wote wametenda kosa moja ambalo linafanana halafu hapo source ni moja CHADEMA ila kutoka Cobid19 kwenda chadema haiwezekani zifanane coz zinatoka sources 19 haiwezekani wote wawe na mawazo sawa katika kujibu tuhuma zao.
Hapo kwenye underline.... Makosa yale yale, chini ya vifungu vile vile, maana yake majibu yanapaswa kuwa ni yale yale, kutokana na mshauri yule yule. Kuna tatizo wapi? Hilda Newton anachofanya ni kuiambia dunia kwamba ana access na siri za chama, na kwamba hajali kuzivujisha mitandaoni. Huoni tatizo hapo?Barua ya kutoka Chadema kwenda Covid19 kufanana ni sawa kwasababu wote wametenda kosa moja ambalo linafanana halafu hapo source ni moja CHADEMA ila [barua] kutoka Cobid19 kwenda chadema haiwezekani zifanane coz zinatoka sources 19 haiwezekani wote wawe na mawazo sawa katika kujibu tuhuma zao.
Hapo kweney mstari.... Ushahidi wowote tafadhali.Anachokifanya Hilda ndicho kilekile alikuwa akikifanya Mdee mara zote. Ikitokea mgogoro kati ya CDM na wanachama wake basi Mdee ataubeba as if ni personal. Nampongeza Hilda kwa kupita "mulemule".
Unaongea kwa jazba wee mama, hivi kuna wauaji kama hilo genge la kikundi chako?Ndiyo mjue COVID19 kwamba usaliti haulipi. Rafiki yako Mama Mdee ndiyo kishapigwa chini sasa mjiandae rasmi wasaliti nyinyi mnaenda wapi kuendeleza usaliti wenu.
ACT Wasaliti kwa Zitto au maccm kwa wahuni, wezi, mafisadi na wauaji maccm. Vinginevyo msamaha wenu unakaribishwa ili mrudishwe kundini.
Mkuu Mmawia alishamaliza kwa kusema hawa watu hawatarudishwa CDM hata wakija na muhuri wa mbinguni, sasa sijui @Erythrocytes anasemaje.Unasemaje? Wewe?
Pengine nimuulize Erythro. kuhusu mstari huu. Siamini nilichosoma toka kwako!
Ila walipoitwa kwenye kikao (cha kamati kuu) halali ili wajitetee hakuna hata mmoja aliyefika wala kutoa sababu za kutofika, hivi inaingia hakilini mtu akose kikao cha maamuzi then aje kwenye kikao cha rufaa?Nakubaliana na msimamo wako 100%. Hapo hapo napata taabu kuamini kuwa chama kitatenda haki kwa kuwaweka wote katika kundi moja; naamini kuna wengine humo wamejikuta wako katika kundi hilo bila kuelewa nini kilikuwa kinaendelea. Mfano ni huyu mama aliyetolewa mahabusu na kupelekwa kuapishwa, sidhani kama atatendewa haki kuwekwa kundi moja na hao waliokubuhu wakina Mdee na Bulaya!!! Itakuwa busara kama hawa watahukumiwa kutokana na kuangalia kila mmoja na kesi yake ingawa wametumia ujanja wa WOTE kuleta majibu sawa!!!
Wahojiwe na kutafakali kwa kina nani kati yao wako tayari kutubu kwa dhati na kukubali kufuata miongozo ya chama!! Wale viiongozi wao vinara na wanajulikana itakuwa sio busara kuwarudisha hata wakitubu kwani wamekwisha kula nyama ya NDUGAI hawawezi kuacha!!!
Safi sana, you nailed it; hii huruma kwa hao wapuuzi sijui inatoka wapi, waliitwa wajitetee wakaingia mitini kisa wakidai usalama wao, kwanini wasingetafuta ulinzi binafsi if they really care?Msamaha ni jambo zuri sana, lakini hapa tuangalie maslahi mapana ya Taifa pamoja na Chama, akina Halima waliweka maslahi yao mbele na sio maslahi ya chama
Ina maana hawawezi kuvumilia maisha ya uanachama wa kawaida na mapambano nje ya bunge?
Na kwa nini hawakusubiri ridhaa ya chama? Hii sio ndoa BAK useme tusameheane tulee watoto
Wananchi wenye imani na chadema walipata faraja baada ya chama kuchukua hatua za kuwafukuza akina halima la sivyo hata mimi singekua na imani tena na chadema
Halafu, kilichonihuzunisha ni kwamba Bulaya alikana mpaka mwisho, mipango yote ya usaliti wameifanya kwa siri na wameshirikiana na watesi wa wapinzani
Ndugai keeps attacking Mbowe and Chadema kwa sababu anapata nguvu kutoka kwa hao covid 19, mateso ambayo chadema imepitia kwenye utawala huu yametokana na ccm, sikutegemea kabisa kama mwanachama mwenye akili anaweza kuungana na watesi for her personal gain, akina halima wametesqa na utawala huu lakini wamepata nguvu ya kuungana nao kwa sababu wanataka pesa za ubunge
Hawafai kuwa viongozi wa chadema na hawaaminiki, who knows, labda watasamehewa halafu next year watapanda dau tena, chadema isilambe matapishi, isonge mbele na wale ambao wako tayari kukipigania chama kabla ya maslahi yao binafsi