Kinachoendelea hapa Dar es salaam sio mgao wa maji, ni kwamba Dawasa imeshakufa

Asante sana mkuu, serikali yetu lazima waamke sasa ili walete mitambo tutumie ya bahari maana hamna namna.
Mkuu sidhani kama tunahitaji maji ya chumvi. Tuna maji mengi ya mito yanapotelea bahari. Mimi nadhani tunatakiwa kuyavuna hayo maji. Tujenge mabwawa na mwisho wa siku yangetusaidia. Ila tatizo tumezoea quick fix zisizo na tija ktk kila jambo
 
Kwa mara ya kwanza naomba niseme wazi tena bila kificho DAWASA na maboss zao wooote walio juu yao hawajui kazi zao, wanachofanya sio kabisa yaan haituingii akilini kabisa
...Kweli Umechukia, Mkuu!![emoji848][emoji848]...
 
Mkuu sidhani kama tunahitaji maji ya chumvi. Tuna maji mengi ya mito yanapotelea bahari. Mimi nadhani tunatakiwa kuyavuna hayo maji. Tujenge mabwawa na mwisho wa siku yangetusaidia. Ila tatizo tumezoea quick fix zisizo na tija ktk kila jambo
Tatizo ni mipango
Kulikuwa na mradi.mkubwa wa upanuzi wa mitambo ya ruvu chini ,wala haijapita miaka mitano, ruvu tayari ina mtambo wa ruvu juu ambao unasupply maji kwa nija ya mlandizi ,
Hela iliyotumika bora hata ungejengwa mtambo wa maji rufiji, mto amqbo kwa sasa unamwaga tu maji baharini
 
Visima vya aina hii vilipigwa marufuku kwa kuwekewa tozo za kutosha , na mlipishaji ni huyo hyo dawasa
Kwanza kupata kibali pili kupata cheti cha ubora wa maji kote ni pesa inatembea na usumbufu mwingi
 
Ni kweli.
 
Nchi inajiendea yenyewe wakati bi tozo anachanja mbuga majuu.
 
Hii inchi kwakweli kabisa hatuna wahandisi wa maji,wakakaa mezani na kutuletea solution lakudumu,yaani ikatokea leo hii Mwalimu Nyerere kufufuka basi atatushangaa sana yaani vyanzo alivyoviachaga kipindi chake Dar ikiwa na wakazi elfu 5 ndio tunavyovitumia atatushangaa sana kwakweli
 
Kazi zinafanywa kwa mazoea.
 
Hivi unajua kuwa mto ruvu haina maji?
 
Aisee.. Kumbe mimi huku niliko Pugu tunapendelewa, maana wiki yote hii yakikatika ni masaa tu yanarudi
 
Awamu hii kila sehemu pameoza.maji yanapelekwa kwa viongozi tu lakini kwa wananchi wa kawaida yana zaidi ya wiki hawajayaona maji.
 
Aliyemteua ndo amfukuze , hata Mimi siwez kuachia ugali wakat walioko juu yangu ndo wabovu zaidi , waanze wao na Mimi nitafata , vinginevyo labda wanifukuze Kwa mamlaka waliyo nayo
Mlishaambiwa huyu msilitarajie 😇
 
Tatizo huyu mukulu wa DAWASSA hana lolote ....janja janja tu ! Ila uzuri ana tawi lake analoning'inia huko jumba jeupe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…