Kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine ndo kitazaa World War III (WW3)

Uko low sana kwenye huu mzozo,kwa taarifa yako Russia anapigana na ulaya nzima+Amerika ni zaidi ya nchi 40,

Ukraine ni uwanja wa mapambano tu, nothing else
Ulaya watapigana bila ndege zao?
 
Update urself
 
Changamoto kubwa iliyopo kwenye hii battle ya Ukraine na Russia ni propaganda nyiiingi kuliko uhalisia

Ndio maana huwa nasema iko siku anaepigika atatoa tu mlio halisi

Haya maneno ya Urusi dhaifu sijui nini kwa mwenye akili timamu hawezi kuyatamka.Urusi angekuwa kaonekana dhaifu hadi sasa NATO wangekuwa wameshaenda kumchapa.

Mifano iko mingi tu ya nchi zilizoonekana dhaifu na zikaenda kupigwa na NATO.

Jiulize tu Urusi kawekewa vikwazo ambavyo hakuna nchi duniani inaweza kuwekewa na ikatoboa hadi sasa bila kuona milio mingi lakini bado wanaendesha vita na NATO hawajaenda kumpiga.Kabla haujanijibu jiulize tu je vile vikwazo akiwekewa France,England,Germany n.k je hadi sasa wangekuwa wanaendesha Vita na wanashikilia maeneo ya adui yao.
 
Wakitaka vita iishe inaisha mapema sana ila itabidi nao walinywe
 
Umesema propaganda ndo Inaendesha vita Ukraine na siyo uhalisia. Cha ajabu na wewe umechangia ki propaganda badala ya facts, hapo ndo umeniacha hoi.

Binafsi ningefurahi kama ungejikita kwenye kujibu maswali ya dodoso ya hoja uliyopo mezani.

1. Hebu tueleze uhalisia ukoje? Na uje na takwimu kudhibitisha uhalisia unaoujua ili na sisi tuelimike.

2. Hebu tupe uhalisia wa nchi ambazo NATO walienda kuzichapa baada ya kuona zimekuwa dhaifu. Na nani alizifanya hizo nchi kuwa dhaifu kabla ya NATO kwenda kuzichapa.
 
wacha kuota amka kumekucha
 
Kwanini unaweka mipaka ya jinsi ya kujadili vitu?
 
Kwanini unaweka mpika ya jinsi ya kujadili vitu.
1. Hoja hujadiliwa siyo nje ya hoja.
Kutoka nje ya hoja ni sawa na kupiga mpira nje ya uwanja badala ya golini.

2. Tunataka kupata maoni ya kichambuzi kwa hoja iliyoko mezani na siyo propaganda na matusi au kejeli

3. Nimeomba utupe ufafanuzi lakini badala yake unateleza kiaina kwa kutaka kupotezea.
 
Uko low sana kwenye huu mzozo,kwa taarifa yako Russia anapigana na ulaya nzima+Amerika ni zaidi ya nchi 40,

Ukraine ni uwanja wa mapambano tu, nothing else
1. Kuhesabu idadi ya nchi Russia anazopigana nazo haileti maana sana(It doesn't hold water) kwani kinachoangaliwa hapo ni Objective achievement i.e. umeshinda au umeshindwa vita?
2. Ni kweli Ukraine ni uwanja wa mapambano na uwanja huo aliyeuandaa ni Russia mwenyewe. Kama wajanja waliitumia Ukraine kama chambo, basi Mrusi alimeza chambo. Mrusi kwa bahati mbaya sana hakuzisoma alama za nyakati. Yan Mrusi hawezi kujitoa ufahamu na kudai kwamba hakujua kitakachotokea endapo atatekeleza kile alichokiita ni SMO. Otherwise tukubaliane kwamba Inteligensia yake ni very inferior and rudimentary.
3. Hakuna tena kitisho cha uwezekano wa kuwapo kwa WW111 kwa sababu vita (mapambano) inaelekea ukingoni kwani wapiganaji Warusi wengi hawana usongo/hamu tena na vita hiyo isiyo na malengo. Lakini zaidi wapiganaji wabobezi( Long experienced) fighters walishauawa. Waliopo ni hawa wenye elimu lakini hawana uzoefu kazini. e.g. Hata wababe (Wagners) nao hilo wameliona.
4. Maadui wa Mrusi inaonekana wameongezeka na wamesambaa wapo nje na ndani ya Urusi kwenyewe kitu ambacho kinamchanganya akili na wakati huo huo washirika wake wanasua-sua kutoa misaada e.g. Putin mwenyewe analalamika (hotuba ya tar.09/05/2023) eti watu wake wanataka kumpindua.
 
1. Hoja hujadiliwa siyo nje ya hoja.
Kutoka nje ya hoja ni sawa na kupiga mpira nje ya uwanja badala ya golini.

2. Tunataka kupata maoni ya kichambuzi kwa hoja iliyoko mezani na siyo propaganda na matusi au kejeli
pole......
 
wacha kuota amka kumekucha
Uliyeamka na usiye na usingizi wala tongotongo hebu tupe maoni na uchambuzi kwa hoja na maswali tuliyouliza bila propaganda za u pro-Russia au Ukraine. Sisi ndo tutafanya :facts check"
 
Mkuu wewe russia huijui ungekaa kimya tu ili usionekane mjinga. Marekani peke yake haiwezi kusimama na russia katika uwanja wa medani. Na sijui kama unaelewa kwamba russia haijapeleka mwanajeshi wake hata mmoja ukraine kwenda kupigana, wanaojambisha nato ni wanamgambo tu kama huku kampuni za ulinzi, kule kuna majeshi binafsi na ni untrained cops ndo wanwahangaisha hivo nato. Ujeruman tayari wameshatoa statement ya kupingana na missio na mmarekani kuingia front ukraine, na ujerumani kwa kauli yake niloisikia leo basi hayuko upande wa marekani sababu anamtetea mrusi, na wametamka wazi marekani na nato ndo wanaleta chokochoko russia na wao ndo walilipua bomba la mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…