Kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine ndo kitazaa World War III (WW3)

Sawa
 
Tuliwahi kusema humu ndani, hii vita imekuwa well calculated na Magharibi before and after.

Wanamjua Putin ana Nuclear ila mpaka wakafikia hatua ya kumsapot Ukraine na kutupilia mbali vitisho vya Putin, maana yake kuna namna wameshajua wanamuweza.

NATO ilishasema wameweka bajet for 5 years. Wajinga wakabeza, wakasema kwa nguvu ya Russia, vita haiwezi kumaliza mwezi.

Hakutakuwa na WW III, ila kwa hesabu hizi za NATO, wataidondosha serikali ya mabavu ya Putin na watu wake wa kijamaa.
 
Walikuahidi wapi?Unaweza kuweka source ya habari Yako?Wenzako tumeshawaomba Toka mwaka Jana watupe source lakini wameshindwa na imebaki ni porojo tu za hapa na pale!Hizi propaganda mfu hazibadili chochote uwanja wa mapambano!
Huyo super power wenu kasha feli kitambo mkuu. Hamna kitu mikwara mingi kazi kidogoooooooo!!!!!
 
NATO walisema Russia hawezi survive kwenye hii SMO miezi mitatu, vipi tuendelee kuwaamini?.
 
Kama wanamuweza si wammalize Sasa kuepusha roho za waukraine zinazopotea Kwa mamia kila siku?
Russia alisema malengo ya SMO lazima yatimie!So hata ikichukua 10 or 20 years ni sawa!
 
China kutomuunga mkono huyu Russia ni moja ya pigo kwa Russia na wale wazee wenye itikadi za miaka ya 60,70 80 na 90.
 
Atumie nuclear hlf uwe mwisho wa vita ? Wazungu sio km ww , kuruhusu mtu atumie nuclear na kumkalia kimya kesho anapiga kwako so urusi akijichanganya tu imekula kwake
UK ilishasema ipo tayari kuweka Nuclear nchini Poland. Na ninaamini mpaka sasa wazungu watakuwa wameshaweka Nukes kadhaa jirani na Russia.

Wazungu huwa hawapuuzii mambo.
 
Nimepitia comments zote naona hakuna comments za maana hasa kwa pro NATO/US.

mtoa mada ungeleta kiini cha vita hii na objectives za Putin au Russia kwa ujumla ili tuone je

1. Urusi imefikia malengo yake?

2. Je ikiisha kwa sasa nani amepoteza?

Jambo la pili naona watu wanazungumzia Urusi kuishiwa silaha sijui kuwa dhaifu. Lakini hakuna anayeweka takwimu zozote kuonesha ni namna gani silaha zao zimepungua?

Jambo la tatu hakuna anayesema combat readiness ya jeshi la Urusi vs wapinzani wake. Hapohapo hakuna anayesema hao wenye nguvu wanazo silaha kiasi (hivyo udhaifu inasemwa ni propaganda).

Kuna wanaosemwa marekani na washirika wanaogopa kutoa silaha nzito kwa Ukraine.... tafsiri ya huo uoga ndio nguvu yenyewe kwa Urusi. Hakuna anayezungumzia.

Vita ni inteligensia kwanza kisha combat readiness na mwisho silaha. Hakuna aliyeonyesha ubora wa intel ya Russia vs NATO/US.

Mwisho mleta mada tahari ulianza na upande mmoja hutapata hoja zenye mizania.

Swali: unaweza kutuambia kwa nini spring counter offensive imesimamishwa hadi sasa na kimsingi haipo tena.

Je unajua kilichoipata NATO main Commanding centre iliyopo Ukraine?

Ni hayo tu
 
Mahaba yako kwa Urusi yanakufanya uufumbie macho ukweli. Jamaa wamechemka, hivyo tunavyo chat hapa majeshi ya Urusi yamenaza kukimbia mji wa Bakhmut.

A super power that can't establish air superiority after one year of war is no super power.
Kama ilivyo desturi yao, hiyo ya kuikimbia Bakhmut wamekana.

Niliwahi kusema humu, kuna wakati majeshi ya Russia yataachia hizo ardhi kwa mkupuo.

Hakuna askari wa Russia anayetamani kufa ktk hii vita. Unapigania nini? Je, vita inaonesha ni matakwa ya Taifa au ya Putin? Morale iko chini kwa askari wa Russia.

Ukraine morale iko juu sababu wanatamani kukomboa ardhi, huku wakikumbuka hasara nzito ya vifo na mali walizopoteza.

Morale yao itaongezeka zaidi endapo wakawa wanakomboa kila eneo lililowahi kutekwa. Hapo wataona everything is possible.
 
mkuu umemaliza mjadala ufungwe mengineo ni blaah blaah blaaah .......
THE GREATS RUSSIA [emoji123][emoji123][emoji123]View attachment 2619147
 
1. Umetoa maelezo mengi kweli, nimejitahidi kusoma kwa makini lakini sijaona mahala popote ulipojibu hoja au maswali niliyouliza hata moja. Kama ni penati zote umebutua nje ya goli.

2. Maelezo uliyotoa yako ki hisia zaidi (Hisia zako) kuliko uhalisia. Sijaona fact(s) yoyote zaidi ya story tamu. Propaganda imekuongoza zaidi kuliko kuongozwa na facts. Mtu akikuomba ushahidi wa uliyoeleza nadhani utatokea mlango wa nyuma na tusijue ulikoelekea.

3. Tunasubiri uje na analysis nzuri itakayojibu maswali ya dodoso kwa facts na evidence kibao. Karibu tena
 
Uzi umejaa hisia tu.mleta Uzi una mapenzi ya upande wa west ila umejificha kichaka Cha karanga....
Kwa hiyo haya ndo majibu yako ya kujibu hoja au maswali yaliyoulizwa.

Tuna safari ndefu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…