Kinachoendelea Msumbiji, magaidi na Jeshi - Part 3

Kinachoendelea Msumbiji, magaidi na Jeshi - Part 3

Uliye
Rwanda ni taifa dogo sana kwa size, watu wake wanavyozidi kuongezeka ina maanisha kuwa taifa litahitaji resources za kutosha ilikuweza kujisapoti na ongezeko la watoto wake.

Kitu anachoweza fanya Kagame ni kutumia akili sana kutumia resources za mataifa mengine kufaidisha raia wake huku raia wake wakitafutiwa makoloni mapya ya kwenda kuishi au kutake over na kuwa na assurance ya Maisha mazuri nje ya Rwanda.

Tusimlaumu Kagame, he is just a father looking after the interest of his children. Tunachotakiwa kufanya kwasasa ni kujitathimini namna tutalinda mipaka yetu, rasilimali zetu, ustawi wetu wa jamii, watu wetu ili tusiangukie kundi la wapumbavu kama msumbiji au Kongo ambao wanakubali kutumika vibaya kuneemesha mataifa mengine na wasikae chini kutazama namna hatima ya taifa lao inakuwa mikononi mwao na sio wageni au wahuni wachache.

Ni aibu kubwa sana kwa taifa kuamuliwa swala la usalama na majirani au humuiya, wizara ya mambo ya ndani inafanya nini? Usalama wa taifa wanafanya nini, wanainchi na raia mnafanya nini?

Kwann hakuna openi discussion and dialogue kuhusu usalama wa taifa na watu wao pamoja na rasilimali?

Hapa ndipo Nyerere alipocheza karata zake vizuri, kuliunganisha taifa letu na kulipa ujasiri wa kuhoji na kuwa wakali sana eneo la mipaka, mfano hapa Tanzania unaona namna tunakuwa wakali ingawa kuna vitisho na mikwara ya hapa na pale ila ni wazi kama raia tuna umoja na hatujachukua hatua sababu tunapiga hesabu zetu kuhoji ni nani atakuja baada ya hawa waliopo?
gemea Msumbiji wafanyaje mkuu! Magaidi Si watu wale!
 
Hivi mnaelewa hata mnaandika nini? Kwa sass TZ haina matatizo kwenye mipaka yao wanajeshi wapo tuu makambini sio busy, mission kama hizi wanalipwa pesa nyingi sana wanajeshi wanaokwenda na kuwapa experience ya vita na mambo mengine, acheni wajeshi wapige pesa au mnataka wawe busy kuwavua uniform za jeshi mitami na kuwatandika wanavijiji kwa utemi tuu na ulevi
Sio kila kitu ni hela, usalama wa taifa haulinganishwi na hizo dola elfu mbilimbili ambazo hazitoshi hata kufadhili kwa ukamilifu mission nzima. Unajua gharama za kuendesha mission na hasara zinazopatikana, landmines na IEDs zikiwekwa ardhini unajua ni gharama kiasi gani inatumika kulinda boots on ground kama kuwapa MRAPs? Au ndio yaleyale ya TPDF kwenda na Toyota double cabin kwenye warzone.

Opportunity cost inayotokana na ugaidi ni kubwa kuliko marupurupu yanayopatikana kwenye security missions za kiherehere na sifa za kijinga. Missions za kwenda ni kama za dhidi ya waasi na kulinda amani, ila hizi za kupambana na ugaidi ni hasara tupu.

Alafu inapendeza nchi kwenda mission ya mbali, sio Kenya ikakurupuka kwenda Somalia na Tanzania iende Msumbiji. Inafaa iwe ni Kenya iende Haiti, Tanzania ilivyoenda Comoro na angalau Rwanda ilivyo Msumbiji.

Alafu haya mambo hayaendeshwi kichwakichwa. Jeshi la Msumbiji lenyewe limegawanyika, wanasiasa hawataki vita iishe. Wewe Mtanzania unajiendesha kule kuchanganywa. Misaada hutolewa kwa serikali na jeshi lenye umoja, kama tulivyosaidia Namibia walikuwa na agenda moja na adui anajulikana. Sasa unaenda Msumbiji huelewi chanzo unaenda kutafuta sifa, unaiga Rwanda wakati hujui wao wamepanga nini na France kwa maslahi ya Total Energies.
 
- Shambulizi la kigaidi mji wa Macomia mwezi jana.

- Oparesheni ya SADC na jeshi la Rwanda.

- Interest ya Kagame katika vita za wengine.

Wa kwanza kufika hapa Msumbiji ni jeshi la Rwanda. Kwa makubaliano ya siri yalowekwa na raisi wa Msumbiji, Felipe Nyusi, na raisi wa Rwanda, Paul Kagame, polisi 300 na wanajeshi 700 wanaingia nchini kuanzia tarehe 9 July, 2021.

View attachment 3008214

Kikosi hiki maalum kinaongozwa na jenerali Innocent Kabandana (pichani) kabla ya hapo baadae kuja kupandishwa cheo kuwa Lt. General kwa oparesheni kubwa yenye matunda hapa nchini Msumbiji.

View attachment 3008215

Siku sita baadae, tarehe 15 July, ndo' kikosi cha SADC kinaingia hapa. Kikosi hiki kina jumla ya wanajeshi 2,200 wengi wao wakitokea Afrika Kusini ambapo ndo' pia anatokea kamanda wa kikosi hiki cha SADC, jenerali Xolani Mankayi. (pichani)

View attachment 3008216

Kwa pamoja, makamanda hawa wawili, Innocent Kabandana (wa Rwanda) na Xolan Mankayi (wa SADC) wanashirikiana na kamanda mwenyeji, Cristovao Chume (pichani), kupanga misheni ya kupambana na magaidi wa Ansar al-sunna.

View attachment 3008217

Jeshi la Rwanda linakabidhiwa mji wa Palma na Mocimboa de Praia na lile la SADC linapewa miji kama vile Nangende, Mueda na Muidumbe.

View attachment 3008218

Kuanzia hapo, magaidi ya Ansar al-sunna yakaepuka kufanya mashambulizi makubwa kwenye miji mikubwa, badala yake wakawa wanashambulia kidogo na kukimbia (small hit-and-run raids), haswa vijiji vidogo visivyo na ulinzi ama kambi ndogo za jeshi zisizokuwa chini ya uangalizi.

Oktoba 2022, magaidi wanavamia maeneo mapya kabisa ambayo hayakuwahi kushambulia hapo kabla. Maeneo ya kusini mwa Cabo Delgado kama vile Namumo, Balama na Montepuez na sio tena kaskazini kama vile Palma na Mocimboa de Praia.

View attachment 3008219

Baadae magaidi wanakuja na mkakati maalum. Wakiendelea kushambulia kule kusini, wanafanya tukio kubwa kaskazini kwa kuvuka mpaka wa Tanzania na kushambulia vijiji vya Kitaya na Michenjele kule Mtwara.

Wanaharibu, kuteka na kuua.

Lengo lao kugawa 'attention' ya vikosi hivi vipya ndani ya Msumbiji, vigawanyike kuzingatia kaskazini na pia kusini mwa Cabo ili wapate mwanya wa udhaifu kushambulia zaidi.

View attachment 3008221

Bahati mbaya mpango huu hauzai matunda na mpaka kufikia ukomo wa mwaka 2022, oparesheni ya kuwadhibiti inafanikiwa kuwapunguza kwa idadi kubwa sana.

Ripoti ya UN Security Council inasema kati ya magaidi 2,500 mpaka 3,000 walipoteza maisha kwenye oparesheni hii.

Matokeo yake tunakuja kuuuona mwaka 2023 kama mwaka tulivu zaidi tofauti na miaka ya nyuma tangu pale 2017. Kwa sasa ni wastani wa matukio 11 kwa mwezi ukilinganisha na hapo 2022 kulipokuwa na wastani wa matukio 36 kwa mwezi.

View attachment 3008224

Ndani ya mwaka huu (2023), Ansar al-sunna wanabadili mbinu na kuanza kutumia 'winning hearts and minds' strategy. Mbinu ya kushinda na kuvutia mapenzi ya watu kwa kutembelea jamii maeneo ya Macomia na Mocimboa ili kufanya nao biashara na kuwaambia wao si watu wabaya.

Hivyo mambo yanatulia kidogo.

View attachment 3008226

Lakini kwenye kimya hiki, kinakuja kishindo kikubwa sasa kuanzia mwanzo wa mwaka 2024.

Mwaka unaanza kwa tabu.

Siku ya tarehe 21 January, magaidi wanashika kijiji cha Mucojo na kuweka sheria kali kwenye mavazi, haswa kwa wanawake, na wanapiga marufuku uuzwaji na unywaji wa pombe, lakini chini ya wiki mbili wanadhibitiwa na kuondoshwa.

View attachment 3008229

Wiki moja mbele, tarehe 31, wanashambulia msafara wa wanajeshi na kusababisha vifo vya wanajeshi wawili.

February 9, wanashambulia eneo la Mazeze na kuchoma makanisa yaliyokuwa yanahifadhi watu.

View attachment 3008230

Lakini kilele cha mwaka huu ni siku ile ya Ijumaa, tarehe 10 mwezi wa tano katika mji wa Macomia.

View attachment 3008232

Siku hiyo, kwenye majira ya alfajiri, magari yalobebelea wanaume zaidi ya mia mbili wenye silaha za moto, yanavamia Macomia kupitia magharibi (Xinavane), kusini (Bangala) na mashariki (Nanga) ili kuwakuta wanajeshi wa Msumbiji katikati.

View attachment 3008233

Swala la kufumba na kufumbua, mvua ya risasi inaanza kushuka kila kona.

Kujiokoa roho zao, watu wanakimbilia huko porini na mashambani.

View attachment 3008234

Simu inaita upesi kwa jeshi la Rwanda pamoja na la SADC kuwa Macomia hali ni tete na unahitajika msaada wa haraka sana.

Magari yalobeba wanajeshi wa RDF na SADC yanatoka mji wa Pemba, mji mkuu wa jimbo la Cabo Delgado, na kuanza safari ya kwenda kuokoa jahazi huko Macomia.

View attachment 3008236

Baada ya mapambano makali, mabwana wanazidiwa na kuondoka lakini baada ya dakika arobaini na kitu, wanarudi tena na mapambano yanazuka upya.

View attachment 3008237

Ni mpaka tarehe 12 May, baada ya siku mbili, ndipo jeshi la Msumbiji na washirika wake wanafanikiwa kuurejesha mji wa Macomia mikononi.

View attachment 3008238

Serikali ya Msumbiji, kwa ajenda wanayoijua wao wenyewe, wanaficha maswahibu yalotokea katika huu mji lakini shida huwezi kufumba macho na mdomo wa kila mtu.

Waliokuwapo wanasema waliona miili ya watu kuanzia kumi mpaka ishirini na tatu. Wanajeshi kadhaa waliuawa, maduka kadhaa yaliporwa na pia 'ambulance' moja ilibebwa.

View attachment 3008240

Hivyo kwa hali hii, tofauti kidogo na hapo nyuma, hatuwezi tukasema hali ni shwari hapa jimboni Cabo Delgado.

Sasa kwenye nyakati hizi za mashaka, 'members' wa SADC, hususani Afrika ya Kusini, Botswana na Lesotho, zinaondoa majeshi yao hapa nchini Msumbiji.

Kama haitoshi, oparesheni yenyewe ya SADC inatarajiwa kufikia mwisho rasmi tarehe 15 July mwaka huu.

View attachment 3008241

Just imagine.

Lakini ajabu upande wa pili, kwa wenzetu wa Rwanda, ambaye si hata mwanachama wa SADC, mambo ni kinyume kabisa na hawa wengine.

View attachment 3008242

Kwanza jeshi hili, kwa namna ya pekee, limejichimbia kwenye mioyo ya wanamsumbiji, wanajeshi wake wanaaminika zaidi ya wenyeji wao linapokuja kwenye swala la uadilifu na ufanisi.

Mara kadhaa, wanajeshi wa Msumbiji wanaleta shida kwa wananchi. Wanafanya uonevu. Wanaiba. Wananchi wanaita wanajeshi wa Rwanda kuja kuwatetea na kweli wanaupata msaada.
(pichani wananchi wa Msumbiji wakiwa wamebebelea picha za Kagame na Nyusi)

View attachment 3008243

Lakini pili, wakati wengine wanabeba mabegi kuondoka hapa nchini Msumbiji kama tulivyoona hapo juu, Rwanda ndo' kwanza anasogeza kiti chake apate kuketi vizuri.

Jenerali Karuretwa (pichani), kiongozi wa ushirikiano wa kijeshi kimataifa nchini Rwanda, anasema;

"Kuondoka kwa majeshi ya SADC nchini Msumbiji kunatufanya tuchukue hatua fulani ... tutawapa mafunzo wanajeshi wa Msumbiji ili kuyachukua maeneo yaliyoyoachwa na jeshi la SADC na pia tutaongeza idadi ya wanajeshi kucover maeneo zaidi."

View attachment 3008244

Mbali na fungu la pesa linalotoka Umoja wa Ulaya (EU) kwenda kwa Rwanda, jenerali Karuretwa anasema kuguswa kwa Rwanda katika oparesheni za kutunza amani ni matokeo ya mauaji ya kimbari, mwaka 1994.

Kama watunza amani wa Umoja wa Mataifa wasingeliwatelekeza, basi wangelinusurika na kikombe kile cha mauaji, hivyo wanaujua umuhimu wa kuitunza amani.

Ikumbukwe mbali na Msumbiji, Rwanda wana jeshi lao kule jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) tangu walipopeleka kikosi chao cha kwanza Januari, 2014 baada ya makubaliano ya Kagame na Raisi Faustine Touadera.

View attachment 3008245

Mpaka kufikia sasa wanajeshi wa Rwanda katika nchi hiyo ni zaidi ya alfu moja, wakiwa hapo kwa makubaliano rasmi ya kuisaidia nchi hii maskini barani Afrika kupambana na waasi wanaoitaka serikali kwa udi na uvumba.

View attachment 3008246

Achilia mbali hapo, tarehe 15 April 2023, Raisi Kagame anafunga safari mpaka nchi ya Benin kukutana na Raisi Patrice Talon ambaye katika kikao anamuahidi kumpatia msaada wa jeshi kupambana na magaidi wanaotokea mipaka ya kaskazini.

View attachment 3008247

Sasa yote haya Rwanda anayafanya kwa gharama ya kitu gani?

Ananufaika vipi na wanajeshi wake waliotapakaa Afrika kupambana na kifo uso kwa uso?

Bila ya shaka kuna mchezo Rwanda anaucheza na mchezo huo unamwingizia zaidi kuliko vile anavyopoteza. Na hii inamfanya autake mchezo zaidi na zaidi.

Kwenye mchezo huu, mbali na kocha mwenyewe bwana Kagame, kapteni si mwingine bali kampuni ya CRYSTAL VENTURES Ltd (CVL). Kampuni yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 500 za kimarekani.

View attachment 3008249

Kampuni hii iliyoanzishwa 1995, ni mkono wa kuume wa chama tawala hapa Rwanda (RPF) na inashikilia karibia kila nyendo ya kiuchumi katika nchi hii kwa kupitia makampuni yake madogo madogo yanayosimama kama matawi.

View attachment 3008251

Mkono wa kampuni hii unagusa kuanzia sekta ya kilimo, madini, ujenzi na hata ulinzi.

Kuanzia 2014, wawakilishi wa kampuni hii wanaambatana na serikali yao kwenda nchini Afrika ya kati, nchi ambayo Rwanda imepeleka wanajeshi wake kupambana na waasi, na tokea hapo wamekuwa wakifungamana na Afrika ya kati kwa makubaliano kadhaa.

Mojawapo ni lile la mwezi wa 9, 2021 ambapo tawi la CVL, Vogueroc, linaidhinishwa na serikali ya Afrika ya kati kufanya uvumbuzi wa migodi ya dhahabu na almasi nchini humo.

THERE'S NO FREE LUNCH.

Hata kule nchini Msumbiji mkondo ni huohuo.

Habari ni zilezile.

Mpaka muda huu unaposoma hapa, tayari makampuni matatu ya CVL; Macefield Ventures, NPD Ltd na Strofinare, yapo kwenye ardhi ya nchi hiyo kwa shughuli mbalimbali chini ya makubaliano ambayo wanayafahamu Felipe Nyusi na Kagame.

View attachment 3008256

Taratibu, shughuli za ujenzi na ulinzi binafsi katika nchi hii, vinaanza kuhodhiwa na makampuni ya Rwanda.

View attachment 3008257

Wataishia wapi na ingali wanazidi kujitanua hivi sasa wakiachwa peke yao na SADC?

Na nini hatma ya Ansar al-sunna mbele ya mabwana hawa wa Rwanda na sisi Tanzania tuliopakana nao?

Bila shaka tutalibakiza jeshi letu hapo Msumbiji, hata kama ni kwa gharama kubwa, lakini yatakayojiri huko mbeleni bado hatujajua.

Ngoja na tuone.
Umechambua visuri.
Ni dhahiri Rwanda ina jeshi bora zaidi ya nchi yoyote kwa ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara.

Jeshi lenye ufanisi na kuaminika na mataifa mengi.
 
Sio kila kitu ni hela, usalama wa taifa haulinganishwi na hizo dola elfu mbilimbili ambazo hazitoshi hata kufadhili kwa ukamilifu mission nzima. Unajua gharama za kuendesha mission na hasara zinazopatikana, landmines na IEDs zikiwekwa ardhini unajua ni gharama kiasi gani inatumika kulinda boots on ground kama kuwapa MRAPs? Au ndio yaleyale ya TPDF kwenda na Toyota double cabin kwenye warzone.

Opportunity cost inayotokana na ugaidi ni kubwa kuliko marupurupu yanayopatikana kwenye security missions za kiherehere na sifa za kijinga. Missions za kwenda ni kama za dhidi ya waasi na kulinda amani, ila hizi za kupambana na ugaidi ni hasara tupu.

Alafu inapendeza nchi kwenda mission ya mbali, sio Kenya ikakurupuka kwenda Somalia na Tanzania iende Msumbiji. Inafaa iwe ni Kenya iende Haiti, Tanzania ilivyoenda Comoro na angalau Rwanda ilivyo Msumbiji.

Alafu haya mambo hayaendeshwi kichwakichwa. Jeshi la Msumbiji lenyewe limegawanyika, wanasiasa hawataki vita iishe. Wewe Mtanzania unajiendesha kule kuchanganywa. Misaada hutolewa kwa serikali na jeshi lenye umoja, kama tulivyosaidia Namibia walikuwa na agenda moja na adui anajulikana. Sasa unaenda Msumbiji huelewi chanzo unaenda kutafuta sifa, unaiga Rwanda wakati hujui wao wamepanga nini na France kwa maslahi ya Total Energies.
Angalau wewe kidogo umejitahidi kuelezea ukweli kwa kiasi fulani, kwa bahati mbaya sana kwamba Watu wengi humu mitandaoni wamekuwa wakitoa Maoni yao kwa kuzingatia hisia zao tu bila ya kujikita kwenye ukweli kuhusu Mgogoro wenyewe.
Wanaropoka ropoka tu maneno yasiyokuwa na ukweli wala hakuna uhakika. Mgogoro huo unaihusu nchi ya Msumbiji ambayo Ina majeshi yake ya ulinzi, lakini katika hali ya kustaajabisha Jeshi linalojadiliwa sana na wachangiaji wengi zaidi ni lile kutoka nchini Rwanda (yaani Jeshi la Rwanda na Rais wa huko Paul Kagame), badala ya kulijadili Jeshi la nchi ya Msumbiji na Utawala wake uliopo huko Msumbiji. Very sad in deed.
 
Sio kila kitu ni hela, usalama wa taifa haulinganishwi na hizo dola elfu mbilimbili ambazo hazitoshi hata kufadhili kwa ukamilifu mission nzima. Unajua gharama za kuendesha mission na hasara zinazopatikana, landmines na IEDs zikiwekwa ardhini unajua ni gharama kiasi gani inatumika kulinda boots on ground kama kuwapa MRAPs? Au ndio yaleyale ya TPDF kwenda na Toyota double cabin kwenye warzone.

Opportunity cost inayotokana na ugaidi ni kubwa kuliko marupurupu yanayopatikana kwenye security missions za kiherehere na sifa za kijinga. Missions za kwenda ni kama za dhidi ya waasi na kulinda amani, ila hizi za kupambana na ugaidi ni hasara tupu.

Alafu inapendeza nchi kwenda mission ya mbali, sio Kenya ikakurupuka kwenda Somalia na Tanzania iende Msumbiji. Inafaa iwe ni Kenya iende Haiti, Tanzania ilivyoenda Comoro na angalau Rwanda ilivyo Msumbiji.

Alafu haya mambo hayaendeshwi kichwakichwa. Jeshi la Msumbiji lenyewe limegawanyika, wanasiasa hawataki vita iishe. Wewe Mtanzania unajiendesha kule kuchanganywa. Misaada hutolewa kwa serikali na jeshi lenye umoja, kama tulivyosaidia Namibia walikuwa na agenda moja na adui anajulikana. Sasa unaenda Msumbiji huelewi chanzo unaenda kutafuta sifa, unaiga Rwanda wakati hujui wao wamepanga nini na France kwa maslahi ya Total Energies.
Sikiliza wewe, unaonekana bado unaishi miaka 100 iliyopita na enzi za kina Nyerere walioamini ukombozi wa bara la Africa, 2024 usalama wa nchi ni juu yako hakuna wa kusaidia na ukitoka usaidiwe utalipa na ndio kinachoendelea sasa, hizo mission zote unazoona ni biashara tupu na nchi husika inalipa gharama zote kuanzia vifaa mpaka mishahara ya wanajeshi, na nchi nyingi wanazitaka sana hizo mission na JWTZ ikiwemo, Rwanda hajaenda Msumbiji Kwa sababu anaipenda Msumbiji au Kenya anaipenda Haiti au Somalia, mission zote hizo motivation ni pesa, kutumia Wagner ni very expensive so kwanini usilipe kidogo Kwa jina la kulinda amani ili kuwadhibiti wabaya wako, na ndio mwanzo utaona mengi sana na hizi mission zitaongezeka sana
 
Angalau wewe kidogo umejitahidi kuelezea ukweli kwa kiasi fulani, kwa bahati mbaya sana kwamba Watu wengi humu mitandaoni wamekuwa wakitoa Maoni yao kwa kuzingatia hisia zao tu bila ya kujikita kwenye ukweli kuhusu Mgogoro wenyewe.
Wanaropoka ropoka tu maneno yasiyokuwa na ukweli wala hakuna uhakika. Mgogoro huo unaihusu nchi ya Msumbiji ambayo Ina majeshi yake ya ulinzi, lakini katika hali ya kustaajabisha Jeshi linalojadiliwa sana na wachangiaji wengi zaidi ni like kutoka nchini Rwanda (yaani Jeshi la Rwanda na Rais wa huko Paul Kagame), badala ya kulijadili Jeshi la nchi ya Msumbiji na Utawala wake uliopo huko Msumbiji. Very sad in deed.
Kaka, kwanini usingefanya busara kidogo ukatupatia uzi ili tujifunze mengi ulonayo? Si mbaya ukatushirikisha your research.
 
Msumbiji ikitaka kukomesha ugaidi. Ni kukamata viongozi wote wa kiislamu wale wakubwa wote na kuwaweka ndani pasipo kujulikana siku yao ya kutoka.
Wajifunze Tanzania, walianza ugaidi wa kuchoma makanisa na kuwamwagia watu tindikali, ila walivyokamatwa magaidi yote ya UAMSHO, kuchomwa kwa makanisa pakakoma.
Tanzania ikawa amani
 
Migogoro kama huo wa huko Msumbiji siyo ya kuingilia kichwa kichwa, umakini na uangalifu mkubwa sana unapaswa kuzingatiwa wakati wote unapo-deal na Migogoro ya aina hiyo.
Aliyekuwa Rais wa Nigeria Bw. Buhari wakati wa kampeni za kugombea Urais alijitapa kwamba kutokana na uzoefu mkubwa alionao kwenye masuala ya medani' za Jeshi, angeweza kulitokomeza kabisa ndani ya muda mfupi usiozidi miezi sita Kundi la Wapiganaji la Boko Haram. Lakini alipoingia Ikulu akaja kugundua ukweli kwamba Boko Haram siyo kundi la Wapiganaji wa Jihad kwa 100% kama alivyokuwa akifikiri. Mbaya zaidi pia akagundua kwamba kundi hilo pia lina 'mkono wake' ndani ya Serikali ya Nigeria, hivyo, uwezekano wa kulitokomeza na kufutika kabisa haupo.
 
Hta usipoteze muda wako kumuelezea huyo mlokole njaa
Yeye anawaza ufunuo wa tiro na sidoni wakati wakati hata kula yake ni mashaka
 
Hapa point ni moja tu mpaka kuiamini Sadc, Tanzania ana upper hand katika ushawish kuliko Rwanda when it comes to Drc issues.

And the vice versa has applied on Mozambique matter, Tz kapoteza kabisa ule ushawishi aliopaswa kuwa nao. RWANDA wametupoka hii fursa. Tujijkize hapo, what ia going on???
'Vijana' wanalewa baa za Kawe, na kugombaniana malaya na civilian, wakilewa vibaka wanawaibia simu wanakwenda kambini kuita wenzao wake wawachape raia mtaa mzima, afisa mkubwa anafokezana na wahuni, wanajaa upepo na kumchoma kisu jeshi linaomboleza, .....
NIDHAMU, UBUNIFU NA KUJUTUMA vinalingana kama zama zile?
Hizi mambo za migogoro na ugaidi ni miradi kama ilivyo kilimo, viwanda, n.k.
Ili utoke kimaisha - kama jamii, hakikisha wenzako hawana utulivu ili wasieze kupanga na kutekeleza maendeleo, na unanufaika vilivyo na huko kukosekana utulivu; ndio michezo US anayowafanyia wapinzani wake, na jirani yetu - PK - amekuwa wakala wake mzuri. Mkenya nae kaelewa somo, amejaa, sisi je?
Kwa sasa bara la Afrika linagombaniwa kwelikweli - ni kigori - kama zile zama za 1880. Baada ya west kupoteza kule magharibi mwa Afrika, nguvu imeelekezwa ukanda huu, je tumejipanga kiulinzi na kunufaika?
 
Hamna sehemu yoyote inaposema Nyusi kawaomba SADC waondoke. Kinachowaondoa SADC ni muda wao ulopangwa kuisha na huku ikiwa ni gharama sana kuendelea na oparesheni hii.

Tanzania kubaki hapo ni sababu ya kumbukumbu ya kilichowatokea mwaka 2022. Hamna taifa jingine la SADC lililowahi kuvamiwa na watu wake kuuawa mbali na Msumbiji na Tanzania.

Kama haitoshi, jeshi la RDF na SADC hapo nchini Msumbiji, hayakuwa yakipeana support. Mwanzoni kila mmoja alikuwa anafanya kazi mwenyewe bila kumpa ripoti mwenzake.

Ni baadae ndo' wakaanza kushirikiana, tena kidogo sana. Ni kana kwamba kila body ina misheni yake japo adui ni mmoja.
Itawezekana vipi adui kuwa mmoja na wakati kuna taarifa zilisikika kuwa magaidi wakipigwa au wakiona wanazidiwa baada ya mapambano na vikosi SADC na FADM wanakimbilia eneo walipo jeshi la rwanda kupata msaada
 
KWA KUWEKA SAWA TAARIFA
SteveMollel.

Shambulizi la Ugaidi kubwa Tz kwa Mara ya kwanza kijiji cha Kitaya lilifanyika kipindi Cha kampeni za uchaguzi wa awamu ya pili ya JPM na baada ya kama wiki 3 mbele ndipo lilifanyika hapo Michenjele siku ya uchaguzi Mkuu.

Na taharuki haikuwa kama ulivyoilezea kwa kuwa wengi wa wananchi milio ya bunduki walitafsiri ni Askari polisi wanajaribu kutengeneza usalama kwenye chumba cha kupiga kura.
Na hata baadhi ya wale wapambe kindaki ndaki wa siasa zilipoanza kusikikwa wakaanza kuzomea kwa kusema
"HATOKI MTU........MNATAKA KUIBA KURA........."
Na mfano wa maneno kama hayo ila hali ilivyozidi ndipo walipobaini wale sio Askari polisi.........

Na haya yote yanajiri ni kipindi ambacho sio Jeshi la JWTz wala RDF Rwanda lililokawa limewasili Msumbiji.
kipindi hichi kulikuwa na Jeshi la Wagner likisaidiana na wenyeji na ufanisi wao bado ulikuwa ni changamoto na ilitokana na Jeshi LA Msumbiji kuwa na tabia za Jeshi la DRC kama walivyokalalamika Vecenaries wa WAGNER na zipo duru zinasema kuwa hata ushauri wa kuwaleta RDF ulitolewa na wao kumwambia Nyusi baada ya wao kuwaona mission inawapwaya ijapokuwa napo naona kama palishauriwa kimkakati.
Na kukuongezea chief tangu JW limevuka kule Mozambique magaidi walivuka awamu moja mwishoni mwishoni mwa uhai wa Mzee Baba na kilichokawakuta hawajajaribu tena kuigusa Tz kiliwaka haswaa mwaka wa nne sasa tunaishi kwa Amani.

Jambo la Mozambique ni mtambuka Kuna scenario zenye kushabihiana na ukweli ukiunganisha dots na mtu smart hawezi unganisha na Jambo la dini hata kwa 5% na kwa aina ya nchi kama ile si ya kuwaachia wenyewe Msumbiji hawatoboi.
Nidokeze kidogo na hapa nipaweke Sawa kwa SteveMollel kipindi Tukio la uvamizi wa Mocimboa tukio linajili palikuwepo na mwanafunzi wangu ile siku alikuwepo kule kiharakati za kusaka life.
Anadai wakati wanakimbia kwa miguu kutoka Mocimboa kuelekea Palma na ikumbukwe pako na urefu mkubwa mno na ikumbukwe tukio la utekaji mji lilianzia Mocimboa baada ya mawiki Kadhaa ikafata Palma.
Sasa kipindi wanakimbia ndani ya kundi Lao anadai walikuwemo na wanajeshi wa Mozambique wawili tena wakiwa full gwanda na bunduki zao maneno walokawa wanalalamika ni kuwa watapambanaje hali ya kuwa wako na miezi mitatu hawajapata mishahara yao.
 
Kuna baadhi nimeona huwa wanabeza utendaji wa kazi wa TISS kuwa wamezembea kwenye hii ishu ya Ugaidi Mozambique.
Sijajua wao walitaka taarifa ya kile wanachokibaini wakibandike magazetini ili wajue jamaa wako kazini...?
Alafu kwa mwenye akili ya Sawa sawa ataelewa ugumu na uzito wa kudili na vikundi vya kimkakati kama hivi pata picha wanaua nchi kama Russia au France ambamo kwa kiwango kikubwa interejensia zao ziko juu ila jamaa wanatoboa.
Mimi binafsi kwa miaka hii minne Sasa yaenda nikiri vyombo vyetu vinafanya kazi kubwa mno hadi maadhi ya miamala ya Mozambique to Tz imerejea kwa kiwango characters kuridhisha.
Msumbiji imekosea sana kuliacha eneo LA kaskazini kana kwamba ni nchi nyingine na hii itawagharimu na huu uingiaji wa RDF pako na viashiria vidogo kuisha kwa huu mgogoro
 
Sikiliza wewe, unaonekana bado unaishi miaka 100 iliyopita na enzi za kina Nyerere walioamini ukombozi wa bara la Africa, 2024 usalama wa nchi ni juu yako hakuna wa kusaidia na ukitoka usaidiwe utalipa na ndio kinachoendelea sasa, hizo mission zote unazoona ni biashara tupu na nchi husika inalipa gharama zote kuanzia vifaa mpaka mishahara ya wanajeshi, na nchi nyingi wanazitaka sana hizo mission na JWTZ ikiwemo, Rwanda hajaenda Msumbiji Kwa sababu anaipenda Msumbiji au Kenya anaipenda Haiti au Somalia, mission zote hizo motivation ni pesa, kutumia Wagner ni very expensive so kwanini usilipe kidogo Kwa jina la kulinda amani ili kuwadhibiti wabaya wako, na ndio mwanzo utaona mengi sana na hizi mission zitaongezeka sana
Mfano mission ya kupambana na ugaidi Somalia imeinufaisha Kenya?

Kenya imepoteza mapato kiasi gani kutokana na kukosa watalii. Ile hasara haileti justification ya kupokea hizo hela. Wanajeshi wangapi wamekufa, zana ngapi zimeteketea, mashambulizi mangapi ya kigaidi yametokea.

Unaielewa opportunity cost kweli, wewe unalinganisha mission ya kuzuia mapinduzi Anjouan au Haiti ikiisha imeisha dhidi ya mission ya kupambana na ugaidi ambao ukiwakimbiza wanatafuta kulipiza kisasi hata mtaani kwa raia. Unadhani gharama za kupambana na ugaidi ni zile za mafuta, silaha na mishahara tu? Nani alilipia shambulizi la Westgate, Garissa na mengine.

Hela za kulipia wanajeshi walinda amani (ambao hata 1000 hawafiki) unaona ni muhimu kuliko hela za makumi elfu ya watalii wanaokuja kwa amani. Kenya hapo mahoteli yalifungwa, flights zikapungua, NGOs na aid workers wakaondoka. Kama hata Msumbiji na umaskini wote inaweza dhamini mission ya Rwanda au Tanzania hiyo mission haiingizi hela nyingi kama unavyodhani, kwanza mapato yake hayaonekani. Utalii unaingiza hela nyingi sana bila consequences za milipuko ya kujitoa mhanga.

Ukiwaambia Msumbiji walipie hata 20% ya mapato yetu ya utalii hawawezi. Ila ukiingia uko kichwakichwa kwa dharau kama Kenya walivyoingia Somalia, mambo yakigeuka soon unapoteza hata 30% ya sekta ya utalii. Calculations
 
Back
Top Bottom