Ivan Stepanov
JF-Expert Member
- Apr 22, 2023
- 6,799
- 22,209
Mpakani ni nje.au hujafika mipakani ukaona jinsi kulivyo??Broo! Je mlinzi hulinda akiwa ndani? Acha niishie hapo, wanaotaka kuelewa wameelewa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpakani ni nje.au hujafika mipakani ukaona jinsi kulivyo??Broo! Je mlinzi hulinda akiwa ndani? Acha niishie hapo, wanaotaka kuelewa wameelewa.
Nyie si mpo busy kusema mama anaupiga mwingi?Baada ya kusoma makala yako mkuu maoni yangu ni haya;
kwanza nimeanza kuelewa chanzo cha hawa magaidi sababu si dini kama tunavyoaminishwa hii ni michezo michafu inayochezwa na baadhi ya serikali ili kujihakikishia wanabaki madarakani ila pia wanahodhi njia za kiuchumi.
hawa wanaoitwa magaidi kwa kisingizio cha dini ya uisilamu wanatumiwa tu kufanikisha malengo ya watu bahati mbaya dini ya uislam inajinasibu sana na vita vya kulinda imani na udhaifu huo unatumiwa vyema na hawa viongozi makatili..
nini tanzania ifanye?
kwa upande wetu tuendelee kuimalisha mifumo yetu ya ulinzi hasa ya ndani ila pia ni wakati wa sisi pia kudeal na hawa bwea wanaotuchukulia poa mimi naamini tunaweza kuwadhibiti vizuri tu kwa hali iliyopo msumbiji hakuna mwekezaji atakuja kuwekeza hapo mtwara kwenye gas yetu hii.. ila tunajua ni nani yupo behind this kwa hili ilipaswa na sisi tuwatekenye hawa wahuni hizi tabia zetu za kijamaa sometime zina tuumiza kama nchi.
leo hii wamejaa waamiaji haramu kila pembe ya nchi na kuna fununu wahamiaji kutoka nchi fulani wao wanajisogeza zaidi karibu na uongozi wanatafuta nini huko tushtuke.. naona walijaribu njia ya magaidi wakafail na wameona njia nyepesi kufikia lengo lao ni kupitia kujipenyeza kwenye uongozi tushtukeeee!
ikiwa SADC itafunga operation zake kule msumbiji na kuwaacha majeshi ya rwanda pekee tutegemee matatizo zaidi mimi naona tunazungukwa pande zote na adui huku sisi tukiwa mtu kati..
namaliza kwa kusema upande wangu naona kwa hiki kinachoendelea target kuu ni Tanzania kinachofanyika kwanza kwa sasa ni kudhoofisha mipaka yetu ambayo ilikuwa imara kwenye ulinzi wa nchi yetu.
kuna nchi inajikuta ni israel ya Africa sasa kabla tatizo halijawa kubwa na sisitunapaswa kuchukua hatu lasivyo tutakuja kushtuka tupo uchi. tutaishia kutupa taulo kwa aibu!
SAsa hapo kosa lake ni lipi kaka? Maana kama Tanzania ingekua bado na ile diplomatic influence iliokuaga nayo miaka yoote, trust me Nyusi asingeshindwa kutu consult kwanza sisi kwa kuheshim mipaka yetu kabla hajaingiza jesho la nchi ambayo ana uhakika kabisa tunahasimiana nayo huko Drc.Rwanda hata usipomwomba anakuja kukuomba yeye mwenyewe. Rejelea sakata la Benini na mipaka yake ya Burkina Faso.
Hapa point ni moja tu mpaka kuiamini Sadc, Tanzania ana upper hand katika ushawish kuliko Rwanda when it comes to Drc issues.Ingalikuwa hivyo, Raisi wa DRC asingeomba majeshi ya MONUSCO na yale ya EACRF yaondoke katika nchi yake ili awakaribishe SADC ambayo Tanzania imo ndani yake kwakuwa anawaamini zaidi.
hii ni point ya msingi chief.Nikipongeze sana.
Tanzania ilipoteza fursa wa kuwa baba wa ulinzi na Usalama wa nchi za kusini mwa Afrika baada ya upigania uhuru ambao sehemu kubwa ulikuwa unaasisiwa Tanzania.
Exactly na mimi ndicho najaribu kukisema hapa kwa SteveMollelSasa Rwanda anachykua fursa hii kwa lengo la kujinufaisha.
UMemaliza kila kitu mkuuKama hatadhibitiwa na Tanzania kwa haraka sana madhara ya utengenezaji wa vikundi vya kihaini kama anavyofanya DRC na sasa huebda Msumbiji atafanya Tz lengo lake ni kujipatia mali kutoka nchi hizo.
Kifupi PK must be quenched
Andiko kama hili kukosa hata views milioni Moja linaakisi upeo wa akili zetu tulivyo mabombonya!- Shambulizi la kigaidi mji wa Macomia mwezi jana.
- Oparesheni ya SADC na jeshi la Rwanda.
- Interest ya Kagame katika vita za wengine.
Wa kwanza kufika hapa Msumbiji ni jeshi la Rwanda. Kwa makubaliano ya siri yalowekwa na raisi wa Msumbiji, Felipe Nyusi, na raisi wa Rwanda, Paul Kagame, polisi 300 na wanajeshi 700 wanaingia nchini kuanzia tarehe 9 July, 2021.
View attachment 3008214
Kikosi hiki maalum kinaongozwa na jenerali Innocent Kabandana (pichani) kabla ya hapo baadae kuja kupandishwa cheo kuwa Lt. General kwa oparesheni kubwa yenye matunda hapa nchini Msumbiji.
View attachment 3008215
Siku sita baadae, tarehe 15 July, ndo' kikosi cha SADC kinaingia hapa. Kikosi hiki kina jumla ya wanajeshi 2,200 wengi wao wakitokea Afrika Kusini ambapo ndo' pia anatokea kamanda wa kikosi hiki cha SADC, jenerali Xolani Mankayi. (pichani)
View attachment 3008216
Kwa pamoja, makamanda hawa wawili, Innocent Kabandana (wa Rwanda) na Xolan Mankayi (wa SADC) wanashirikiana na kamanda mwenyeji, Cristovao Chume (pichani), kupanga misheni ya kupambana na magaidi wa Ansar al-sunna.
View attachment 3008217
Jeshi la Rwanda linakabidhiwa mji wa Palma na Mocimboa de Praia na lile la SADC linapewa miji kama vile Nangende, Mueda na Muidumbe.
View attachment 3008218
Kuanzia hapo, magaidi ya Ansar al-sunna yakaepuka kufanya mashambulizi makubwa kwenye miji mikubwa, badala yake wakawa wanashambulia kidogo na kukimbia (small hit-and-run raids), haswa vijiji vidogo visivyo na ulinzi ama kambi ndogo za jeshi zisizokuwa chini ya uangalizi.
Oktoba 2022, magaidi wanavamia maeneo mapya kabisa ambayo hayakuwahi kushambulia hapo kabla. Maeneo ya kusini mwa Cabo Delgado kama vile Namumo, Balama na Montepuez na sio tena kaskazini kama vile Palma na Mocimboa de Praia.
View attachment 3008219
Baadae magaidi wanakuja na mkakati maalum. Wakiendelea kushambulia kule kusini, wanafanya tukio kubwa kaskazini kwa kuvuka mpaka wa Tanzania na kushambulia vijiji vya Kitaya na Michenjele kule Mtwara.
Wanaharibu, kuteka na kuua.
Lengo lao kugawa 'attention' ya vikosi hivi vipya ndani ya Msumbiji, vigawanyike kuzingatia kaskazini na pia kusini mwa Cabo ili wapate mwanya wa udhaifu kushambulia zaidi.
View attachment 3008221
Bahati mbaya mpango huu hauzai matunda na mpaka kufikia ukomo wa mwaka 2022, oparesheni ya kuwadhibiti inafanikiwa kuwapunguza kwa idadi kubwa sana.
Ripoti ya UN Security Council inasema kati ya magaidi 2,500 mpaka 3,000 walipoteza maisha kwenye oparesheni hii.
Matokeo yake tunakuja kuuuona mwaka 2023 kama mwaka tulivu zaidi tofauti na miaka ya nyuma tangu pale 2017. Kwa sasa ni wastani wa matukio 11 kwa mwezi ukilinganisha na hapo 2022 kulipokuwa na wastani wa matukio 36 kwa mwezi.
View attachment 3008224
Ndani ya mwaka huu (2023), Ansar al-sunna wanabadili mbinu na kuanza kutumia 'winning hearts and minds' strategy. Mbinu ya kushinda na kuvutia mapenzi ya watu kwa kutembelea jamii maeneo ya Macomia na Mocimboa ili kufanya nao biashara na kuwaambia wao si watu wabaya.
Hivyo mambo yanatulia kidogo.
View attachment 3008226
Lakini kwenye kimya hiki, kinakuja kishindo kikubwa sasa kuanzia mwanzo wa mwaka 2024.
Mwaka unaanza kwa tabu.
Siku ya tarehe 21 January, magaidi wanashika kijiji cha Mucojo na kuweka sheria kali kwenye mavazi, haswa kwa wanawake, na wanapiga marufuku uuzwaji na unywaji wa pombe, lakini chini ya wiki mbili wanadhibitiwa na kuondoshwa.
View attachment 3008229
Wiki moja mbele, tarehe 31, wanashambulia msafara wa wanajeshi na kusababisha vifo vya wanajeshi wawili.
February 9, wanashambulia eneo la Mazeze na kuchoma makanisa yaliyokuwa yanahifadhi watu.
View attachment 3008230
Lakini kilele cha mwaka huu ni siku ile ya Ijumaa, tarehe 10 mwezi wa tano katika mji wa Macomia.
View attachment 3008232
Siku hiyo, kwenye majira ya alfajiri, magari yalobebelea wanaume zaidi ya mia mbili wenye silaha za moto, yanavamia Macomia kupitia magharibi (Xinavane), kusini (Bangala) na mashariki (Nanga) ili kuwakuta wanajeshi wa Msumbiji katikati.
View attachment 3008233
Swala la kufumba na kufumbua, mvua ya risasi inaanza kushuka kila kona.
Kujiokoa roho zao, watu wanakimbilia huko porini na mashambani.
View attachment 3008234
Simu inaita upesi kwa jeshi la Rwanda pamoja na la SADC kuwa Macomia hali ni tete na unahitajika msaada wa haraka sana.
Magari yalobeba wanajeshi wa RDF na SADC yanatoka mji wa Pemba, mji mkuu wa jimbo la Cabo Delgado, na kuanza safari ya kwenda kuokoa jahazi huko Macomia.
View attachment 3008236
Baada ya mapambano makali, mabwana wanazidiwa na kuondoka lakini baada ya dakika arobaini na kitu, wanarudi tena na mapambano yanazuka upya.
View attachment 3008237
Ni mpaka tarehe 12 May, baada ya siku mbili, ndipo jeshi la Msumbiji na washirika wake wanafanikiwa kuurejesha mji wa Macomia mikononi.
View attachment 3008238
Serikali ya Msumbiji, kwa ajenda wanayoijua wao wenyewe, wanaficha maswahibu yalotokea katika huu mji lakini shida huwezi kufumba macho na mdomo wa kila mtu.
Waliokuwapo wanasema waliona miili ya watu kuanzia kumi mpaka ishirini na tatu. Wanajeshi kadhaa waliuawa, maduka kadhaa yaliporwa na pia 'ambulance' moja ilibebwa.
View attachment 3008240
Hivyo kwa hali hii, tofauti kidogo na hapo nyuma, hatuwezi tukasema hali ni shwari hapa jimboni Cabo Delgado.
Sasa kwenye nyakati hizi za mashaka, 'members' wa SADC, hususani Afrika ya Kusini, Botswana na Lesotho, zinaondoa majeshi yao hapa nchini Msumbiji.
Kama haitoshi, oparesheni yenyewe ya SADC inatarajiwa kufikia mwisho rasmi tarehe 15 July mwaka huu.
View attachment 3008241
Just imagine.
Lakini ajabu upande wa pili, kwa wenzetu wa Rwanda, ambaye si hata mwanachama wa SADC, mambo ni kinyume kabisa na hawa wengine.
View attachment 3008242
Kwanza jeshi hili, kwa namna ya pekee, limejichimbia kwenye mioyo ya wanamsumbiji, wanajeshi wake wanaaminika zaidi ya wenyeji wao linapokuja kwenye swala la uadilifu na ufanisi.
Mara kadhaa, wanajeshi wa Msumbiji wanaleta shida kwa wananchi. Wanafanya uonevu. Wanaiba. Wananchi wanaita wanajeshi wa Rwanda kuja kuwatetea na kweli wanaupata msaada.
(pichani wananchi wa Msumbiji wakiwa wamebebelea picha za Kagame na Nyusi)
View attachment 3008243
Lakini pili, wakati wengine wanabeba mabegi kuondoka hapa nchini Msumbiji kama tulivyoona hapo juu, Rwanda ndo' kwanza anasogeza kiti chake apate kuketi vizuri.
Jenerali Karuretwa (pichani), kiongozi wa ushirikiano wa kijeshi kimataifa nchini Rwanda, anasema;
"Kuondoka kwa majeshi ya SADC nchini Msumbiji kunatufanya tuchukue hatua fulani ... tutawapa mafunzo wanajeshi wa Msumbiji ili kuyachukua maeneo yaliyoyoachwa na jeshi la SADC na pia tutaongeza idadi ya wanajeshi kucover maeneo zaidi."
View attachment 3008244
Mbali na fungu la pesa linalotoka Umoja wa Ulaya (EU) kwenda kwa Rwanda, jenerali Karuretwa anasema kuguswa kwa Rwanda katika oparesheni za kutunza amani ni matokeo ya mauaji ya kimbari, mwaka 1994.
Kama watunza amani wa Umoja wa Mataifa wasingeliwatelekeza, basi wangelinusurika na kikombe kile cha mauaji, hivyo wanaujua umuhimu wa kuitunza amani.
Ikumbukwe mbali na Msumbiji, Rwanda wana jeshi lao kule jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) tangu walipopeleka kikosi chao cha kwanza Januari, 2014 baada ya makubaliano ya Kagame na Raisi Faustine Touadera.
View attachment 3008245
Mpaka kufikia sasa wanajeshi wa Rwanda katika nchi hiyo ni zaidi ya alfu moja, wakiwa hapo kwa makubaliano rasmi ya kuisaidia nchi hii maskini barani Afrika kupambana na waasi wanaoitaka serikali kwa udi na uvumba.
View attachment 3008246
Achilia mbali hapo, tarehe 15 April 2023, Raisi Kagame anafunga safari mpaka nchi ya Benin kukutana na Raisi Patrice Talon ambaye katika kikao anamuahidi kumpatia msaada wa jeshi kupambana na magaidi wanaotokea mipaka ya kaskazini.
View attachment 3008247
Sasa yote haya Rwanda anayafanya kwa gharama ya kitu gani?
Ananufaika vipi na wanajeshi wake waliotapakaa Afrika kupambana na kifo uso kwa uso?
Bila ya shaka kuna mchezo Rwanda anaucheza na mchezo huo unamwingizia zaidi kuliko vile anavyopoteza. Na hii inamfanya autake mchezo zaidi na zaidi.
Kwenye mchezo huu, mbali na kocha mwenyewe bwana Kagame, kapteni si mwingine bali kampuni ya CRYSTAL VENTURES Ltd (CVL). Kampuni yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 500 za kimarekani.
View attachment 3008249
Kampuni hii iliyoanzishwa 1995, ni mkono wa kuume wa chama tawala hapa Rwanda (RPF) na inashikilia karibia kila nyendo ya kiuchumi katika nchi hii kwa kupitia makampuni yake madogo madogo yanayosimama kama matawi.
View attachment 3008251
Mkono wa kampuni hii unagusa kuanzia sekta ya kilimo, madini, ujenzi na hata ulinzi.
Kuanzia 2014, wawakilishi wa kampuni hii wanaambatana na serikali yao kwenda nchini Afrika ya kati, nchi ambayo Rwanda imepeleka wanajeshi wake kupambana na waasi, na tokea hapo wamekuwa wakifungamana na Afrika ya kati kwa makubaliano kadhaa.
Mojawapo ni lile la mwezi wa 9, 2021 ambapo tawi la CVL, Vogueroc, linaidhinishwa na serikali ya Afrika ya kati kufanya uvumbuzi wa migodi ya dhahabu na almasi nchini humo.
THERE'S NO FREE LUNCH.
Hata kule nchini Msumbiji mkondo ni huohuo.
Habari ni zilezile.
Mpaka muda huu unaposoma hapa, tayari makampuni matatu ya CVL; Macefield Ventures, NPD Ltd na Strofinare, yapo kwenye ardhi ya nchi hiyo kwa shughuli mbalimbali chini ya makubaliano ambayo wanayafahamu Felipe Nyusi na Kagame.
View attachment 3008256
Taratibu, shughuli za ujenzi na ulinzi binafsi katika nchi hii, vinaanza kuhodhiwa na makampuni ya Rwanda.
View attachment 3008257
Wataishia wapi na ingali wanazidi kujitanua hivi sasa wakiachwa peke yao na SADC?
Na nini hatma ya Ansar al-sunna mbele ya mabwana hawa wa Rwanda na sisi Tanzania tuliopakana nao?
Bila shaka tutalibakiza jeshi letu hapo Msumbiji, hata kama ni kwa gharama kubwa, lakini yatakayojiri huko mbeleni bado hatujajua.
Ngoja na tuone.
sio mimi mkuu ni mkuu SteveMollel huyo ndio mwenye uziStory ime-skip from part 1 to 3?part II sijaiona steveachi kama itakupendeza naomba pandisha link ya sehemu ya pili tuipitie.
Kwa mwendo hakuna kamanda, nakubaliana na wewe. Namchukia huyu jamaa lakini kwakwel anatumia akil sana.Hakuna wa kumzuia Kagame
Nyie endeleeni kuvunja matofari
Sure. Tanzania ilishindwa kubadilika kadiri dunia inavyobadilika huenda hadi sasa inawaza upigania uhuru, ilitakiwa ibadilike baada ya nchi hizi kuwa huru iwe mnufaika na wa kuaminiwa. Leo USA anatumia nguvu ili abaki world policeman. Liko tatizo . Na hii ndioutajua hatujui nini hasa hitaji la dunia kwa sasa, mfano tuna sera ya ujamaa lkn hatuuishi ujamaa wala miko yake. PK uko smart kwa ajili ya huo mkoa wa Rwanda, kwanini tusimfanyie counter na ku take over?Hapa point ni moja tu mpaka kuiamini Sadc, Tanzania ana upper hand katika ushawish kuliko Rwanda when it comes to Drc issues.
And the vice versa has applied on Mozambique matter, Tz kapoteza kabisa ule ushawishi aliopaswa kuwa nao. RWANDA wametupoka hii fursa. Tujijkize hapo, what ia going on???
Jesbi letu lina ueledi wa kutosha sana kuliko la PK hiyo ni uhakika wa zaidi 200% tatizo ni uongozi na malengo.Kwa mwendo hakuna kamanda, nakubaliana na wewe. Namchukia huyu jamaa lakini kwakwel anatumia akil sana.
Wakat wengine tuna deal na petty issues, yeye ana focus na big stuffs. Acha achanje mbuga ru, mpaka siku tunakuja kushtuka, tulisha chelewa kitambooo
SteveMollel usimsikilize huyu lete NONDO hizo tusimamishe mjengo hii bado haijaisha mpaka iisheAlisema hii Ni sehemu ya mwisho
Sawa.SteveMollel usimsikilize huyu lete NONDO hizo tusimamishe mjengo hii bado haijaisha mpaka iishe
I think you have a short-sighted mind.
Je, umeshawahi kujiuliza ni kwa Nini nchi yenye uchumi mkubwa kama Nigeria imeshindwa kulitokomeza kundi la Boko Haram licha ya kwamba nchi hiyo Ina Jeshi Kubwa Sana na lenye nguvu zaidi ukilinganisha na nchi nyingine yoyote ile kwenye ukanda huo wa Magharibi mwa Afrika???Do you know the reasons???
Mambo haya hayapendwi sana, mkuu. Sisi tunataka umbea wa mastaa.An
Andiko kama hili kukosa hata views milioni Moja linaakisi upeo wa akili zetu tulivyo mabombonya!
Kuondoka Kwa vikosi vya SADC msumbiji ni ombi la rais Nyusi na mkuu wao wa majeshi waliwaarifu jamaa waondoke na ukumbuke vikosi vya Rwanda wanaishi kama wafalme kule maana hakuna wanachokosa kuanzia posho nono, vifaa vya kisasa yaani hata wakiwa doria mtaani wanajeshi wa Rwanda wanavifaa vya kisasa na bora zaidi kuliko hata wanajeshi wetu, lazima kazi ifanyike kubwa na serikali ya msumbiji Kwa sasa imeshaanza kuwalipa wanajeshi wa Rwanda hadi mishahara Kwa siri, na achilia mbali makampuni hayo ya Rwanda lakini TOTAL wanaomba vikosi zaidi vikalinde uwekezaji wao lakini sharti viwe vikosi kutoka Rwanda tu