Kinachoendelea Msumbiji, magaidi na Jeshi - Part 3

Uliye
gemea Msumbiji wafanyaje mkuu! Magaidi Si watu wale!
 
Sio kila kitu ni hela, usalama wa taifa haulinganishwi na hizo dola elfu mbilimbili ambazo hazitoshi hata kufadhili kwa ukamilifu mission nzima. Unajua gharama za kuendesha mission na hasara zinazopatikana, landmines na IEDs zikiwekwa ardhini unajua ni gharama kiasi gani inatumika kulinda boots on ground kama kuwapa MRAPs? Au ndio yaleyale ya TPDF kwenda na Toyota double cabin kwenye warzone.

Opportunity cost inayotokana na ugaidi ni kubwa kuliko marupurupu yanayopatikana kwenye security missions za kiherehere na sifa za kijinga. Missions za kwenda ni kama za dhidi ya waasi na kulinda amani, ila hizi za kupambana na ugaidi ni hasara tupu.

Alafu inapendeza nchi kwenda mission ya mbali, sio Kenya ikakurupuka kwenda Somalia na Tanzania iende Msumbiji. Inafaa iwe ni Kenya iende Haiti, Tanzania ilivyoenda Comoro na angalau Rwanda ilivyo Msumbiji.

Alafu haya mambo hayaendeshwi kichwakichwa. Jeshi la Msumbiji lenyewe limegawanyika, wanasiasa hawataki vita iishe. Wewe Mtanzania unajiendesha kule kuchanganywa. Misaada hutolewa kwa serikali na jeshi lenye umoja, kama tulivyosaidia Namibia walikuwa na agenda moja na adui anajulikana. Sasa unaenda Msumbiji huelewi chanzo unaenda kutafuta sifa, unaiga Rwanda wakati hujui wao wamepanga nini na France kwa maslahi ya Total Energies.
 
Umechambua visuri.
Ni dhahiri Rwanda ina jeshi bora zaidi ya nchi yoyote kwa ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara.

Jeshi lenye ufanisi na kuaminika na mataifa mengi.
 
Angalau wewe kidogo umejitahidi kuelezea ukweli kwa kiasi fulani, kwa bahati mbaya sana kwamba Watu wengi humu mitandaoni wamekuwa wakitoa Maoni yao kwa kuzingatia hisia zao tu bila ya kujikita kwenye ukweli kuhusu Mgogoro wenyewe.
Wanaropoka ropoka tu maneno yasiyokuwa na ukweli wala hakuna uhakika. Mgogoro huo unaihusu nchi ya Msumbiji ambayo Ina majeshi yake ya ulinzi, lakini katika hali ya kustaajabisha Jeshi linalojadiliwa sana na wachangiaji wengi zaidi ni lile kutoka nchini Rwanda (yaani Jeshi la Rwanda na Rais wa huko Paul Kagame), badala ya kulijadili Jeshi la nchi ya Msumbiji na Utawala wake uliopo huko Msumbiji. Very sad in deed.
 
Sikiliza wewe, unaonekana bado unaishi miaka 100 iliyopita na enzi za kina Nyerere walioamini ukombozi wa bara la Africa, 2024 usalama wa nchi ni juu yako hakuna wa kusaidia na ukitoka usaidiwe utalipa na ndio kinachoendelea sasa, hizo mission zote unazoona ni biashara tupu na nchi husika inalipa gharama zote kuanzia vifaa mpaka mishahara ya wanajeshi, na nchi nyingi wanazitaka sana hizo mission na JWTZ ikiwemo, Rwanda hajaenda Msumbiji Kwa sababu anaipenda Msumbiji au Kenya anaipenda Haiti au Somalia, mission zote hizo motivation ni pesa, kutumia Wagner ni very expensive so kwanini usilipe kidogo Kwa jina la kulinda amani ili kuwadhibiti wabaya wako, na ndio mwanzo utaona mengi sana na hizi mission zitaongezeka sana
 
Kaka, kwanini usingefanya busara kidogo ukatupatia uzi ili tujifunze mengi ulonayo? Si mbaya ukatushirikisha your research.
 
Msumbiji ikitaka kukomesha ugaidi. Ni kukamata viongozi wote wa kiislamu wale wakubwa wote na kuwaweka ndani pasipo kujulikana siku yao ya kutoka.
Wajifunze Tanzania, walianza ugaidi wa kuchoma makanisa na kuwamwagia watu tindikali, ila walivyokamatwa magaidi yote ya UAMSHO, kuchomwa kwa makanisa pakakoma.
Tanzania ikawa amani
 
Migogoro kama huo wa huko Msumbiji siyo ya kuingilia kichwa kichwa, umakini na uangalifu mkubwa sana unapaswa kuzingatiwa wakati wote unapo-deal na Migogoro ya aina hiyo.
Aliyekuwa Rais wa Nigeria Bw. Buhari wakati wa kampeni za kugombea Urais alijitapa kwamba kutokana na uzoefu mkubwa alionao kwenye masuala ya medani' za Jeshi, angeweza kulitokomeza kabisa ndani ya muda mfupi usiozidi miezi sita Kundi la Wapiganaji la Boko Haram. Lakini alipoingia Ikulu akaja kugundua ukweli kwamba Boko Haram siyo kundi la Wapiganaji wa Jihad kwa 100% kama alivyokuwa akifikiri. Mbaya zaidi pia akagundua kwamba kundi hilo pia lina 'mkono wake' ndani ya Serikali ya Nigeria, hivyo, uwezekano wa kulitokomeza na kufutika kabisa haupo.
 
Hta usipoteze muda wako kumuelezea huyo mlokole njaa
Yeye anawaza ufunuo wa tiro na sidoni wakati wakati hata kula yake ni mashaka
 
'Vijana' wanalewa baa za Kawe, na kugombaniana malaya na civilian, wakilewa vibaka wanawaibia simu wanakwenda kambini kuita wenzao wake wawachape raia mtaa mzima, afisa mkubwa anafokezana na wahuni, wanajaa upepo na kumchoma kisu jeshi linaomboleza, .....
NIDHAMU, UBUNIFU NA KUJUTUMA vinalingana kama zama zile?
Hizi mambo za migogoro na ugaidi ni miradi kama ilivyo kilimo, viwanda, n.k.
Ili utoke kimaisha - kama jamii, hakikisha wenzako hawana utulivu ili wasieze kupanga na kutekeleza maendeleo, na unanufaika vilivyo na huko kukosekana utulivu; ndio michezo US anayowafanyia wapinzani wake, na jirani yetu - PK - amekuwa wakala wake mzuri. Mkenya nae kaelewa somo, amejaa, sisi je?
Kwa sasa bara la Afrika linagombaniwa kwelikweli - ni kigori - kama zile zama za 1880. Baada ya west kupoteza kule magharibi mwa Afrika, nguvu imeelekezwa ukanda huu, je tumejipanga kiulinzi na kunufaika?
 
Itawezekana vipi adui kuwa mmoja na wakati kuna taarifa zilisikika kuwa magaidi wakipigwa au wakiona wanazidiwa baada ya mapambano na vikosi SADC na FADM wanakimbilia eneo walipo jeshi la rwanda kupata msaada
 
KWA KUWEKA SAWA TAARIFA
SteveMollel.

Shambulizi la Ugaidi kubwa Tz kwa Mara ya kwanza kijiji cha Kitaya lilifanyika kipindi Cha kampeni za uchaguzi wa awamu ya pili ya JPM na baada ya kama wiki 3 mbele ndipo lilifanyika hapo Michenjele siku ya uchaguzi Mkuu.

Na taharuki haikuwa kama ulivyoilezea kwa kuwa wengi wa wananchi milio ya bunduki walitafsiri ni Askari polisi wanajaribu kutengeneza usalama kwenye chumba cha kupiga kura.
Na hata baadhi ya wale wapambe kindaki ndaki wa siasa zilipoanza kusikikwa wakaanza kuzomea kwa kusema
"HATOKI MTU........MNATAKA KUIBA KURA........."
Na mfano wa maneno kama hayo ila hali ilivyozidi ndipo walipobaini wale sio Askari polisi.........

Na haya yote yanajiri ni kipindi ambacho sio Jeshi la JWTz wala RDF Rwanda lililokawa limewasili Msumbiji.
kipindi hichi kulikuwa na Jeshi la Wagner likisaidiana na wenyeji na ufanisi wao bado ulikuwa ni changamoto na ilitokana na Jeshi LA Msumbiji kuwa na tabia za Jeshi la DRC kama walivyokalalamika Vecenaries wa WAGNER na zipo duru zinasema kuwa hata ushauri wa kuwaleta RDF ulitolewa na wao kumwambia Nyusi baada ya wao kuwaona mission inawapwaya ijapokuwa napo naona kama palishauriwa kimkakati.
Na kukuongezea chief tangu JW limevuka kule Mozambique magaidi walivuka awamu moja mwishoni mwishoni mwa uhai wa Mzee Baba na kilichokawakuta hawajajaribu tena kuigusa Tz kiliwaka haswaa mwaka wa nne sasa tunaishi kwa Amani.

Jambo la Mozambique ni mtambuka Kuna scenario zenye kushabihiana na ukweli ukiunganisha dots na mtu smart hawezi unganisha na Jambo la dini hata kwa 5% na kwa aina ya nchi kama ile si ya kuwaachia wenyewe Msumbiji hawatoboi.
Nidokeze kidogo na hapa nipaweke Sawa kwa SteveMollel kipindi Tukio la uvamizi wa Mocimboa tukio linajili palikuwepo na mwanafunzi wangu ile siku alikuwepo kule kiharakati za kusaka life.
Anadai wakati wanakimbia kwa miguu kutoka Mocimboa kuelekea Palma na ikumbukwe pako na urefu mkubwa mno na ikumbukwe tukio la utekaji mji lilianzia Mocimboa baada ya mawiki Kadhaa ikafata Palma.
Sasa kipindi wanakimbia ndani ya kundi Lao anadai walikuwemo na wanajeshi wa Mozambique wawili tena wakiwa full gwanda na bunduki zao maneno walokawa wanalalamika ni kuwa watapambanaje hali ya kuwa wako na miezi mitatu hawajapata mishahara yao.
 
Kuna baadhi nimeona huwa wanabeza utendaji wa kazi wa TISS kuwa wamezembea kwenye hii ishu ya Ugaidi Mozambique.
Sijajua wao walitaka taarifa ya kile wanachokibaini wakibandike magazetini ili wajue jamaa wako kazini...?
Alafu kwa mwenye akili ya Sawa sawa ataelewa ugumu na uzito wa kudili na vikundi vya kimkakati kama hivi pata picha wanaua nchi kama Russia au France ambamo kwa kiwango kikubwa interejensia zao ziko juu ila jamaa wanatoboa.
Mimi binafsi kwa miaka hii minne Sasa yaenda nikiri vyombo vyetu vinafanya kazi kubwa mno hadi maadhi ya miamala ya Mozambique to Tz imerejea kwa kiwango characters kuridhisha.
Msumbiji imekosea sana kuliacha eneo LA kaskazini kana kwamba ni nchi nyingine na hii itawagharimu na huu uingiaji wa RDF pako na viashiria vidogo kuisha kwa huu mgogoro
 
Mfano mission ya kupambana na ugaidi Somalia imeinufaisha Kenya?

Kenya imepoteza mapato kiasi gani kutokana na kukosa watalii. Ile hasara haileti justification ya kupokea hizo hela. Wanajeshi wangapi wamekufa, zana ngapi zimeteketea, mashambulizi mangapi ya kigaidi yametokea.

Unaielewa opportunity cost kweli, wewe unalinganisha mission ya kuzuia mapinduzi Anjouan au Haiti ikiisha imeisha dhidi ya mission ya kupambana na ugaidi ambao ukiwakimbiza wanatafuta kulipiza kisasi hata mtaani kwa raia. Unadhani gharama za kupambana na ugaidi ni zile za mafuta, silaha na mishahara tu? Nani alilipia shambulizi la Westgate, Garissa na mengine.

Hela za kulipia wanajeshi walinda amani (ambao hata 1000 hawafiki) unaona ni muhimu kuliko hela za makumi elfu ya watalii wanaokuja kwa amani. Kenya hapo mahoteli yalifungwa, flights zikapungua, NGOs na aid workers wakaondoka. Kama hata Msumbiji na umaskini wote inaweza dhamini mission ya Rwanda au Tanzania hiyo mission haiingizi hela nyingi kama unavyodhani, kwanza mapato yake hayaonekani. Utalii unaingiza hela nyingi sana bila consequences za milipuko ya kujitoa mhanga.

Ukiwaambia Msumbiji walipie hata 20% ya mapato yetu ya utalii hawawezi. Ila ukiingia uko kichwakichwa kwa dharau kama Kenya walivyoingia Somalia, mambo yakigeuka soon unapoteza hata 30% ya sekta ya utalii. Calculations
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…