Kinachoendelea Msumbiji, magaidi na Jeshi - Part 3

Kinachoendelea Msumbiji, magaidi na Jeshi - Part 3

Hiyo mbinu ya Winning hearts and Mind strategy ina fanikiwa vipi wakati jamii ina fahamu matatizo yote hayo yana sabibshwa na kikundi hicho ndio maana serikali imeingia vitani kuwaondoa
Kwenye picha pale inayohusu winning hearts and mind strategy kuna jamaa hapo kashika msahafu af kiunoni anabunduki anatoa Mahubiri huku wananchi wakimsikiliza kwa makini.

Hapo inaonesha ilitumika dini kurainisha mioyo ya hao raia.

Km unavyojua wenzetu linapokuja suala la dini akili zao huwa wanaachana nazo.
 
Baada ya kusoma makala yako mkuu maoni yangu ni haya;

kwanza nimeanza kuelewa chanzo cha hawa magaidi sababu si dini kama tunavyoaminishwa hii ni michezo michafu inayochezwa na baadhi ya serikali ili kujihakikishia wanabaki madarakani ila pia wanahodhi njia za kiuchumi.

hawa wanaoitwa magaidi kwa kisingizio cha dini ya uisilamu wanatumiwa tu kufanikisha malengo ya watu bahati mbaya dini ya uislam inajinasibu sana na vita vya kulinda imani na udhaifu huo unatumiwa vyema na hawa viongozi makatili..

nini tanzania ifanye?
kwa upande wetu tuendelee kuimalisha mifumo yetu ya ulinzi hasa ya ndani ila pia ni wakati wa sisi pia kudeal na hawa bwea wanaotuchukulia poa mimi naamini tunaweza kuwadhibiti vizuri tu kwa hali iliyopo msumbiji hakuna mwekezaji atakuja kuwekeza hapo mtwara kwenye gas yetu hii.. ila tunajua ni nani yupo behind this kwa hili ilipaswa na sisi tuwatekenye hawa wahuni hizi tabia zetu za kijamaa sometime zina tuumiza kama nchi.

leo hii wamejaa waamiaji haramu kila pembe ya nchi na kuna fununu wahamiaji kutoka nchi fulani wao wanajisogeza zaidi karibu na uongozi wanatafuta nini huko tushtuke.. naona walijaribu njia ya magaidi wakafail na wameona njia nyepesi kufikia lengo lao ni kupitia kujipenyeza kwenye uongozi tushtukeeee!

ikiwa SADC itafunga operation zake kule msumbiji na kuwaacha majeshi ya rwanda pekee tutegemee matatizo zaidi mimi naona tunazungukwa pande zote na adui huku sisi tukiwa mtu kati..

namaliza kwa kusema upande wangu naona kwa hiki kinachoendelea target kuu ni Tanzania kinachofanyika kwanza kwa sasa ni kudhoofisha mipaka yetu ambayo ilikuwa imara kwenye ulinzi wa nchi yetu.

kuna nchi inajikuta ni israel ya Africa sasa kabla tatizo halijawa kubwa na sisitunapaswa kuchukua hatu lasivyo tutakuja kushtuka tupo uchi. tutaishia kutupa taulo kwa aibu!
Hawa magaidi si waislamu?
 
Ile Cabo Delgado na Niassa ni sehemu ya Tanganyika, Tanganyika ilipoteza hayo maeneo kutokana na vita ya dunia. Baadae ilitokea machafuko huko Msumbiji ikabidi Nyerere afanye jambo sasa hapo ndio ilikuwa nafasi nzuri ya kurudisha hayo maeneo. Ile kaskazini mwa Msumbiji ni sehemu halali ya Tanganyika.
Kuna baadhi nimeona huwa wanabeza utendaji wa kazi wa TISS kuwa wamezembea kwenye hii ishu ya Ugaidi Mozambique.
Sijajua wao walitaka taarifa ya kile wanachokibaini wakibandike magazetini ili wajue jamaa wako kazini...?
Alafu kwa mwenye akili ya Sawa sawa ataelewa ugumu na uzito wa kudili na vikundi vya kimkakati kama hivi pata picha wanaua nchi kama Russia au France ambamo kwa kiwango kikubwa interejensia zao ziko juu ila jamaa wanatoboa.
Mimi binafsi kwa miaka hii minne Sasa yaenda nikiri vyombo vyetu vinafanya kazi kubwa mno hadi maadhi ya miamala ya Mozambique to Tz imerejea kwa kiwango characters kuridhisha.
Msumbiji imekosea sana kuliacha eneo LA kaskazini kana kwamba ni nchi nyingine na hii itawagharimu na huu uingiaji wa RDF pako na viashiria vidogo kuisha kwa huu mgogoro
 
Mfano mission ya kupambana na ugaidi Somalia imeinufaisha Kenya?

Kenya imepoteza mapato kiasi gani kutokana na kukosa watalii. Ile hasara haileti justification ya kupokea hizo hela. Wanajeshi wangapi wamekufa, zana ngapi zimeteketea, mashambulizi mangapi ya kigaidi yametokea.

Unaielewa opportunity cost kweli, wewe unalinganisha mission ya kuzuia mapinduzi Anjouan au Haiti ikiisha imeisha dhidi ya mission ya kupambana na ugaidi ambao ukiwakimbiza wanatafuta kulipiza kisasi hata mtaani kwa raia. Unadhani gharama za kupambana na ugaidi ni zile za mafuta, silaha na mishahara tu? Nani alilipia shambulizi la Westgate, Garissa na mengine.

Hela za kulipia wanajeshi walinda amani (ambao hata 1000 hawafiki) unaona ni muhimu kuliko hela za makumi elfu ya watalii wanaokuja kwa amani. Kenya hapo mahoteli yalifungwa, flights zikapungua, NGOs na aid workers wakaondoka. Kama hata Msumbiji na umaskini wote inaweza dhamini mission ya Rwanda au Tanzania hiyo mission haiingizi hela nyingi kama unavyodhani, kwanza mapato yake hayaonekani. Utalii unaingiza hela nyingi sana bila consequences za milipuko ya kujitoa mhanga.

Ukiwaambia Msumbiji walipie hata 20% ya mapato yetu ya utalii hawawezi. Ila ukiingia uko kichwakichwa kwa dharau kama Kenya walivyoingia Somalia, mambo yakigeuka soon unapoteza hata 30% ya sekta ya utalii. Calculations
Watanzania wengi wanatoa Maoni yao kwa mihemko tu ya kisiasa kuhusiana na suala hili la Mgogoro wa huko Msumbiji bila ya kuzingatia ukweli, faida na hasara za Mgogoro wenyewe.
 
Mwaka fulani sikumbuki vizuri nadhani ni 2020 nikiwa maeneo ya Mbagala walipita JW wengi sana wakiwa kwenye magari yao na silaha nzito nzito kweli pamoja na vifaa vya kazi vikiwa vimefunikwa kwa maturubai wakielekea huko kusini. Watu wote tulibaki kutizama huo msafara, jamaa walikuwa wengi mno, nadhani ndio walio enda kuweka kambi huko mpakani mwa Msumbiji.
KWA KUWEKA SAWA TAARIFA
SteveMollel.

Shambulizi la Ugaidi kubwa Tz kwa Mara ya kwanza kijiji cha Kitaya lilifanyika kipindi Cha kampeni za uchaguzi wa awamu ya pili ya JPM na baada ya kama wiki 3 mbele ndipo lilifanyika hapo Michenjele siku ya uchaguzi Mkuu.

Na taharuki haikuwa kama ulivyoilezea kwa kuwa wengi wa wananchi milio ya bunduki walitafsiri ni Askari polisi wanajaribu kutengeneza usalama kwenye chumba cha kupiga kura.
Na hata baadhi ya wale wapambe kindaki ndaki wa siasa zilipoanza kusikikwa wakaanza kuzomea kwa kusema
"HATOKI MTU........MNATAKA KUIBA KURA........."
Na mfano wa maneno kama hayo ila hali ilivyozidi ndipo walipobaini wale sio Askari polisi.........

Na haya yote yanajiri ni kipindi ambacho sio Jeshi la JWTz wala RDF Rwanda lililokawa limewasili Msumbiji.
kipindi hichi kulikuwa na Jeshi la Wagner likisaidiana na wenyeji na ufanisi wao bado ulikuwa ni changamoto na ilitokana na Jeshi LA Msumbiji kuwa na tabia za Jeshi la DRC kama walivyokalalamika Vecenaries wa WAGNER na zipo duru zinasema kuwa hata ushauri wa kuwaleta RDF ulitolewa na wao kumwambia Nyusi baada ya wao kuwaona mission inawapwaya ijapokuwa napo naona kama palishauriwa kimkakati.
Na kukuongezea chief tangu JW limevuka kule Mozambique magaidi walivuka awamu moja mwishoni mwishoni mwa uhai wa Mzee Baba na kilichokawakuta hawajajaribu tena kuigusa Tz kiliwaka haswaa mwaka wa nne sasa tunaishi kwa Amani.

Jambo la Mozambique ni mtambuka Kuna scenario zenye kushabihiana na ukweli ukiunganisha dots na mtu smart hawezi unganisha na Jambo la dini hata kwa 5% na kwa aina ya nchi kama ile si ya kuwaachia wenyewe Msumbiji hawatoboi.
Nidokeze kidogo na hapa nipaweke Sawa kwa SteveMollel kipindi Tukio la uvamizi wa Mocimboa tukio linajili palikuwepo na mwanafunzi wangu ile siku alikuwepo kule kiharakati za kusaka life.
Anadai wakati wanakimbia kwa miguu kutoka Mocimboa kuelekea Palma na ikumbukwe pako na urefu mkubwa mno na ikumbukwe tukio la utekaji mji lilianzia Mocimboa baada ya mawiki Kadhaa ikafata Palma.
Sasa kipindi wanakimbia ndani ya kundi Lao anadai walikuwemo na wanajeshi wa Mozambique wawili tena wakiwa full gwanda na bunduki zao maneno walokawa wanalalamika ni kuwa watapambanaje hali ya kuwa wako na miezi mitatu hawajapata mishahara yao.
 
JW,TISS mnafanya kazi kubwa sanaa kutulinda heko kwenu.
Natamani Looting Departmentyo iwe hai kisawasawa. PK ameiwezesha RDF; Kwa sasa RDF ni kama mgambo kwa makampuni ya Wazungu. Kuna mageuzi makubwa sana ktk kupata na ulinzi wa rasilimali zao huku Afrika.
Kwa hali ilivyo Afrika inaweza kuwa bara la migogoro kwa karne nyingi mbele; na mataifa yenye rasilimali zaidi ndio yapo hatarini zaidi.
 
Nikipongeze sana.
Tanzania ilipoteza fursa wa kuwa baba wa ulinzi na Usalama wa nchi za kusini mwa Afrika baada ya upigania uhuru ambao sehemu kubwa ulikuwa unaasisiwa Tanzania. Iltakiwa ibadilike kuwa wafadhili wa wapigania uhuru na kuwa mshauri na mkoloni wa mambo ya kiulinzi ambayo yangeipeleka kunufaika na nchi hizi ambazo hazina umoja wa kitaifa au ukosefu wa uongozi.
Sasa Rwanda anachykua fursa hii kwa lengo la kujinufaisha. Kama hatadhibitiwa na Tanzania kwa haraka sana madhara ya utengenezaji wa vikundi vya kihaini kama anavyofanya DRC na sasa huebda Msumbiji atafanya Tz lengo lake ni kujipatia mali kutoka nchi hizo.
Kifupi PK must be quenched
Kuna sehemu historia imekupita. tanzania ilikuwa sehemu kubwa ya ukombozi nchi nyingi na wanaharakati ila kenya na ukibaraka wake alitumiwa sana kumuhujumu tanzania .kama utakumbuka kulishawai kutokea ugaidi kipindi tuan wasaidia south afrika kupata uhuru
 
Mwaka fulani sikumbuki vizuri nadhani ni 2020 nikiwa maeneo ya Mbagala walipita JW wengi sana wakiwa kwenye magari yao na silaha nzito nzito kweli pamoja na vifaa vya kazi vikiwa vimefunikwa kwa maturubai wakielekea huko kusini. Watu wote tulibaki kutizama huo msafara, jamaa walikuwa wengi mno, nadhani ndio walio enda kuweka kambi huko mpakani mwa Msumbiji.
Mzee sisi wengine bado tunaishi along Kilwa road mpaka leo, hayaa mambo wewe ulioyaona 2020 sis mpaka leo tunayaona.
Tunaona wakienda tunawaona wakirud. Tunawaona wakienda tena. Kwakifupi huko kusin kuko busy sanaa
 
Natamani Looting Department mayo iwe jai. PK ameiwezesha RDF; Kwa sasa RDF ni kama mgambo kwa makampuni ya Wazungu. Kuna mageuzi makubwa sana ktk kupata na ulinzi wa rasilimali zao huku Afrika.
Kwa hali ilivyo Afrika inaweza kuwa bara la migogoro kwa karne nyingi mbele; na mataifa yenye rasilimali zaidi ndio yapo hatarini zaidi.
Hapa nimelowa huwa napenda kuçhangia mada za migogoro zihusuzo mataifa mengine ila kwa nyumbani sipendi wala sitaki mabaya yatufike.

M naamini Tanzanians tuko very smart na hakuna wa kutuzidi EA. Kuanziaintelligence,mbinu,vifaa,morali kwa wanajeshi wetu Iko juu.
 
Mzee sisi wengine bado tunaishi along Kilwa road mpaka leo, hayaa mambo wewe ulioyaona 2020 sis mpaka leo tunayaona.
Tunaona wakienda tunawaona wakirud. Tunawaona wakienda tena. Kwakifupi huko kusin kuko busy sanaa
Mwezi March nilienda Mtwara kupitia Ruvuma ukifika Tunduru kuna ukaguzi wa vitambulisho na ukiwa unaingia au kutoka Mtwara kulikuwa na ukaguzi wa vitambulisho japo wenyeji walidai huwa inatokea Mara moja moja Kama kuna tishio la magaidi kuvuka boda.
 
Mwezi March nilienda Mtwara kupitia Ruvuma ukifika Tunduru kuna ukaguzi wa vitambulisho na ukiwa unaingia au kutoka Mtwara kulikuwa na ukaguzi wa vitambulisho japo wenyeji walidai huwa inatokea Mara moja moja Kama kuna tishio la magaidi kuvuka boda.
Tuko vizuri hakuna kucheka na kima yaaani mpaka natamani watumie machine zile za kuulia tembo( ikiingia kama sindao ila inapotokea inaacha uwanja).

Hakuna kuwaonea huruma kabisa.
 
Tuko vizuri hakuna kucheka na kima yaaani mpaka natamani watumie machine zile za kuulia tembo( ikiingia kama sindao ila inapotokea inaacha uwanja).

Hakuna kuwaonea huruma kabisa.
Hata wananchi nao wanapaswa kuwa wamoja kwenye mapambano ya namna hii wananchi wanapaswa kuwa jicho la kwanza hawa wahuni huwa wanajifcha kwenye jamii hasa sponsors wao
 
Back
Top Bottom