Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Ogopa sana taifa ambalo lenye bora kiongozi na sio kiongozi bora. Rais wa Sri Lanka alikua bora kiongozi, yeye alikuwa anafanya mambo kuwafurahisha wananchi bila kuangalia madhara yake hapo mbeleni.
Alikuwa akikopa mikopo mikubwa isiyo na unafuu na kufanya mambo ambayo yameifanya Sri Lanka kuwa na deni kubwa mpaka kufikia hatua ya kushindwa kuhudumia wananchi wake.
Kwa sababu ya janga la COVID-19, mapato kutoka kwa watalii wa kigeni na pesa zinazotumwa kutoka nje zilishuka. Wanauchumi walionya kuwa Sri Lanka huenda isiweze kulipa deni lake la nje na wakahimiza serikali kuwasiliana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Baada ya kuchaguliwa mnamo 2019, Rais Gotabaya Rajapaksa alipunguza ushuru, ambayo ilinyima serikali mapato yanayohitajika sana.
Kama Rais ni vyema ukawa unafanya maamuzi huku ukiangalia muelekeo wa nchi yako. Na hapa ndiyo maana nasema Tanzania tushukuru kuwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwani mikopo inayochukuliwa ni ya nafuu na pia inatumika kwenye mambo muhimu ya maendeleo ya taifa huku ikiendelea kutengeneza fursa na kuweza kupata fedha za kurudishwa mikopo hiyo.
Mnaolalamika kuhusu tozo na ushuru, kumbukeni umuhimu wake katika kuiendesha serikali. Makusanyo ya tozo unaiongezea serikali kipato na kuiwezesha kulipa madeni.
Rais Samia Suluhu amekuwa akiweka wazi umuhimu wa tozo na kufafanua maana ya mikopo hiyo na namna inavyotumika.
Pia hapa tunaweza kuona dhahira umuhimu wa Rais kuwaachia watendaji wake kutekeleza majukumu yao na kujipunguzia majukumu. Rais Samia anafanya kazi zake, Waziri Mkuu naye anafanya majukumu yake, vivyo hivyo wasaidizi wote wa Rais mpaka wabunge.
Lakini kwa serikali ya Sri Lanka, Rais ndiye mkuu wa nchi, serikali na jeshi nchini Sri Lanka lakini anashiriki majukumu mengi ya kiutendaji na waziri mkuu, ambaye anaongoza chama tawala bungeni jambo linalofanya aingilie majukumu ambayo sio yake na kunyima viongozi kutekeleza kazi zao kwa ufasaha.
Wakati tukiiombea Sri Lanka, tukumbuke pia kumuombea Rais wetu na pia kumshukuru Mungu kwa kutupa kiongozi Bora na sio bora kiongozi.
Tanzania ni salama na Samia. KAZI IENDELEE