Kinachoendelea Sri Lanka, Tanzania tushukuru kuwa na Rais Samia

Kinachoendelea Sri Lanka, Tanzania tushukuru kuwa na Rais Samia

Ogopa sana taifa ambalo lenye bora kiongozi na sio kiongozi bora. Rais wa Sri Lanka alikua bora kiongozi, yeye alikuwa anafanya mambo kuwafurahisha wananchi bila kuangalia madhara yake hapo mbelen...
Kipindi hiki wamejitokeza majuha wengi sana,maana walishaona kusifia Ni njia moja ya kupata uteuzi.
 
Ni lini nchi hii iliwahi kuwa kwenye hatari yoyote chini ya uongozi wa rais yeyote? punguza ushabiki!
Chini ya Mwendazake Nchinilokuwa kwenye balaa kubwa la kiuchumi..

Kama Takwimu hutaki kuzikubali huwezi tumia akili yako ndogo kufikiria kwamba kwa nini Mwendazake alizuia kutoa Takwimu za Uchumi tofauti na za kwake?

Huwezi hata kufikiria kidogo kwamba Rais Samia answezaje kisukuma sekta zote za Uchumi zikiwemo zile zilizotelrkezwa na Mwendazake kwa visingizio vya kujenga sgr kama ajira,salaries,kilimo,maji nk?
 
Ogopa sana taifa ambalo lenye bora kiongozi na sio kiongozi bora. Rais wa Sri Lanka alikua bora kiongozi, yeye alikuwa anafanya mambo kuwafurahisha wananchi bila kuangalia madhara yake hapo mbeleni...
Serious kwa madudu yote,anayofanya,unamsifia?

Hii ndio huwa tunaita stockolm syndrome,anayekutesa,unafikia point unakuwa unamuona kama mwema na anakupenda sana.

Ni kama mbakwaji,kumpenda mbakaji,
 
Samia anahamasisha ufisadi katika serikali yake,anapaswa ang'olewe fasta sana
 
Serious kwa madudu yote,anayofanya,unamsifia?

Hii ndio huwa tunaita stockolm syndrome,anayekutesa,unafikia point unakuwa unamuona kama mwema na anakupenda sana.

Ni kama mbakwaji,kumpenda mbakaji,
Si kweli unavyosema. Rais Samia anafanya kazi kubwa sana kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
 
Kwa mwendo huu ilikuwa lazma familia ikimbie Ikulu😂😂😂!

Bado zamu ya ile Miungu ya CCM utatu wa kikafiri, Msoga Jazz Band, Marope, Millet Mp
 
Wapi imeandikwa ni kosa kumsifia mtu anapofanya kazi nzuri? acheni chuki binafsi, mama anafanya kazi na huu ndio ukweli.
Tunatambua uko UVCCM na unatokea kaya yenye dhiki ila sometime kabla hujaandika utumbo hebu ona aibu kwa watu wazima walioko humu
 
Ogopa sana taifa ambalo lenye bora kiongozi na sio kiongozi bora. Rais wa Sri Lanka alikua bora kiongozi, yeye alikuwa anafanya mambo kuwafurahisha wananchi bila kuangalia madhara yake hapo mbeleni.

Alikua akikopa mikopo mikubwa isiyo na unafuu na kufanya mambo ambayo yameifanya Sri Lanka kuwa na deni kubwa mpaka kufikia hatua ya kushindwa kuhudumia wananchi wake.

Kwa sababu ya janga la COVID-19, mapato kutoka kwa watalii wa kigeni na pesa zinazotumwa kutoka nje zilishuka. Wanauchumi walionya kuwa Sri Lanka huenda isiweze kulipa deni lake la nje na wakahimiza serikali kuwasiliana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Baada ya kuchaguliwa mnamo 2019, Rais Gotabaya Rajapaksa alipunguza ushuru, ambayo ilinyima serikali mapato yanayohitajika sana.

Kama Rais ni vyema ukawa unafanya maamuzi huku ukiangalia muelekeo wa nchi yako. Na hapa ndiyo maana nasema Tanzania tushukuru kuwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwani mikopo inayochukuliwa ni ya nafuu na pia inatumika kwenye mambo muhimu ya maendeleo ya taifa huku ikiendelea kutengeneza fursa na kuweza kupata fedha za kurudishwa mikopo hiyo.

Mnaolalamika kuhusu tozo na ushuru, kumbukeni umuhimu wake katika kuiendesha serikali. Makusanyo ya tozo unaiongezea serikali kipato na kuiwezesha kulipa madeni.

Rais Samia Suluhu amekuwa akiweka wazi umuhimu wa tozo na kufafanua maana ya mikopo hiyo na namna inavyotumika.

Pia hapa tunaweza kuona dhahira umuhimu wa Rais kuwaachia watendaji wake kutekeleza majukumu yao na kujipunguzia majukumu. Rais Samia anafanya kazi zake, Waziri Mkuu naye anafanya majukumu yake, vivyo hivyo wasaidizi wote wa Rais mpaka wabunge.

Lakini kwa serikali ya Sri Lanka, Rais ndiye mkuu wa nchi, serikali na jeshi nchini Sri Lanka lakini anashiriki majukumu mengi ya kiutendaji na waziri mkuu, ambaye anaongoza chama tawala bungeni jambo linalofanya aingilie majukumu ambayo sio yake na kunyima viongozi kutekeleza kazi zao kwa ufasaha.

Wakati tukiiombea Sri Lanka, tukumbuke pia kumuombea Rais wetu na pia kumshukuru Mungu kwa kutupa kiongozi Bora na sio bora kiongozi.

Tanzania ni salama na Samia. KAZI IENDELEE
Hv mizombi kama hii isiyojielewa huwa inatokea wp!!!?
limevaa ushungu utafikiri kichwa cha jogoo
kumbaf kabisa!
 
Tunatambua uko UVCCM na unatokea kaya yenye dhiki ila sometime kabla hujaandika utumbo hebu ona aibu kwa watu wazima walioko humu
Shida yenu mnadhani kila anayesifia anatokea chama tawala.
 
Umefail kushawishi watu ili wakuelewe kuwa mama ako anafanya kazi nzr, watu hawakuelewi na hawatakuelewa labda uje na mada ingine
 
Nipigeni maweni mpendavyo lkn yule bwana angelikuwepo mapema sana angelisha tusrilanka. God is great
 
Back
Top Bottom