residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,348
- 15,205
Wazazi wanalipishwa kwani!?Na ndio huwa vichaka vya wakwepaji kodi.....
Non-Profit Organization haiko subjected to Tax payments.Maelezo mazuri lakini yana mapungufu. Kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali, sasa basi, ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.
Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara
Hatari sana, asiyejua anajifanya anajua kila kituSomething is very wrong somewhere in Tanzania.
Charity works are prohibited.
Investments are prohibited.
Sending money there is prohibited.
Tanzania is doomed.
Inaelekea umekariri au kukaririshwa kauli za wanasiasa. Hii ni shule iiyoanzishwa na mama raia wa Australia kusaidia watoto maskini kupata elimu. Watoto zaidi ya 2000 wa msingi na sekondari wanasoma, kuvalishwa na kulishwa bure, bila kulipa hata senti moja, vijana zaidi ya 300 kutoka kaya hizo hizo wanalipiwa karo na stipend kusoma vyuo vikuu na vyuo vya kati bila wazazi wao kugharimia. Sasa wewe unazungumza kodi gani. Yaani wananchi wa Australia wajitolee kusomesha Watanzania kupunguzia Serikali/TRA mzigo wa kugharimia elimu halafu Serikali iwatake wahisani wanaoisaidia kugharimia elimu kulipa kodi!Awamu hii hakuna janja janja ya kukwepa kodi, muda mnaotumia kwenye mitandao ya kijamii kutafuta huruma bora mtafute mwanasheria mzuri ili mpate haki yenu.
TRA nenda kwenye NGO watu wamejisajiri kama shirika linalojiendesha kwa misaada huku ni wanatumia kivuko hicho kukwepa kodi!
👍Maelezo mazuri lakini yana mapungufu. Kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali, sasa basi, ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.
Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara
Kama ni hivyo na sadaka zianze kukatwa kodiNa ndio huwa vichaka vya wakwepaji kodi.....
Kama ni jukumu la serikali yako wangesaidiwa na wazungu ambao wanatoa mabilioni ya fedha zao ili watoto wenu wasome bure????Elimu kwa Watanzania ni jukumu na kazi ya Serikali JMTZ na siyo Mzungu wa sijui Australia, kwani huko kwao hana matatizo ? ...
🤣🤣Elimu kwa Watanzania ni jukumu na kazi ya Serikali JMTZ na siyo Mzungu wa sijui Australia, kwani huko kwao hana matatizo ? ...
🤣🤣Kama ni jukumu la serikali yako wangesaidiwa na wazungu ambao wanatoa mabilioni ya fedha zao ili watoto wenu wasome bure????
Wewe kama sio mchawi basi ni mshirikina. Sijawai ona roho ya kichawi kama yako
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE
UTANGULIZII
1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana.
2. Shule hii inategemea misaada ya wahisani kwa asilimia 100 amabpo aslimia 90 inatoka kwa wahisani wa Australia.
3. Shule ina usajili wa wa shirika lisilo la kiserikali na ina jumla ya shule tatu zilizosajiliwa; Shule ya msingi (Na. AR. 02/7011), Shule ya Sekondari ya Wasichana (Na. S. 5243) and shule ya sekondari ya Bweni wavulana wa O-level na mchanganyiko A-level (Na. S. 4262). Shule ilipewa tamko kuwa ni shule ya ufadhili kupitia cheti S/Na. 53.
4. Shule inatoa ajira kwa zaidi ya watanzania 300 na wageni waajiriwa nane. Zaidi ya asilimia 60 ya uongozi wa Shule ni watanzania.
5. Shule pia inawasaidia wahitimu 326 kusoma elimu ya juu kwenye vyuo vikuu na vyuo vya kati vinginevyo.
6. Tarehe 3 Novemba 2020, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliondoa kiasi cha Shilingi za Kitanzania 500,000,000 kwenye akaunti za Shule.
7. Tarehe 4 Novemba, Mwenyekiti wa Bodi wa wafadhili wa Australia (amabao ndio wanaifadhili bajeti ya mwaka ya shule kwa asilimia 90) aliandika kutujulisha kuwa Bodi haitaweza tena kutuma fedha zozote kwenye shule maana hawawezi kutoa ufadhili kulipa kodi za TRA. Badala yake wanataka kufadhili elimu tu ya wanafunzi wa Kitanzania.
8. Kwa sababu hiyo, St Jude ina uwezo mdogo sana wa kifedha na haiwezi kujiendesha kama kawaida.
9. Bajeti ya shule kwa mwaka 2020 ni Shillingi za Kitanzania 12,682,710,722. Kila mwaka, shule inarudisha bajeti nzima kwenye uchumi wa Tanzania kwa kutumia asilimia 100 ya matumizi ndani ya Nchi. Kwa ufupi jedwali linatoa picha ya matumizi kwa baadhi ya maeneo muhimu sana kama ifuatavyo:
....... see attach for more
Nimekosa jibu la kukupa Mkuu.Awamu hii hakuna janja janja ya kukwepa kodi, muda mnaotumia kwenye mitandao ya kijamii kutafuta huruma bora mtafute mwanasheria mzuri ili mpate haki yenu.
TRA nenda kwenye NGO watu wamejisajili kama shirika linalojiendesha kwa misaada huku ni wanatumia kivuko hicho kukwepa kodi!