Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.
Hasira za mkizi ,bora wametambua ya kwamba muda umewatupa mkono
Mara nyingi niwaonapo wazee hawa huwa naikumbuka vita ya Kagera iliyomng'oa dikteta nduli fashisti Iddi Amini Dada pale Uganda.

Wakati huo nilikuwa nafanya kazi pale TRC Mwanza station......hakika niliwashuhudia wapiganaji wetu WAZALENDO wengi wakielekea vitani. Nasi tulitoa kila aina ya msaada uliohitajika ili kuwawezesha wapiganaji hawa.

Ndio maana siku mzee Lowassa alipotangaza kujiuzulu uwaziri mkuu sikushangaa kabisa.

Na hata nikisikia mzee Kinana na mwenzie Makamba wamestaafu siasa na kurudisha kadi za chama cha siasa kwa wamiliki wa kadi sitashangaa.

Kuchukua maamuzi magumu ni sehemu ya maisha ya mjeda popote pale duniani.

Nawatakia Dominika yenye Baraka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale wazee hata wakikataa kuhojiwa ni sawa tu.
Lakini wao nao wanawajibika kuwa kimya, kimsingi kwa umri wao inatosha sasa hawa ni kama Joka la kibisa hawana meno .
Nao wanajua ukimya wao ni usalama wao, vijana wao wanakubalika chamani na hawawezi kuwaharibia career wanaokuja.
Kwenda kuhojiwa ni kutolewa kifunguo kimawazo ili sasa nao watoe maoni
Ccm haiwezi kuwaadhibu wazee hawa ila kuweka sawa kuingia kwenye game kwa baraka zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vema wameamua kuondoka mapema kwani CCM inahitaji mabadiliko Makubwa Sana.
Uzee na Uzoefu usioenda na Uadilifu Ni hewa tu na hauna maslahi kwa Taifa letu.

Kama Wana Tuhuma zozote za Kijinai Basi nashauri Mamlaka Husika ziingie kazini.
Mwenyewe ukajibeba na familia yako ukidhani utapat teuzi, kafie mbele huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.

Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.

Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
Akili za makonda na babake haziwezi kuona hilo. Wao ni tutawakomesha,......tutawamaliza,....watatutambuwa,......... Bila kuangalia kuwa na wenzao ni binadamu wenye fikra.
 
Komredi Kinana kaona utoto kwenda, hata wakimpa adhabu ya kumfuta uanachama bado ni alama tosha ya CCM hata asipokuwa na kadi! Sio watu Kama Bashite,Kitila, Waitara, Bashiru, Pole pole ambao hata hadhi ya ushabiki wa chama hawana hata wakiwa na kadi!

Kwa Membe it's ok kwenda bado ana future ndani ya Chama. Nahisi soon Komredi Mangula ataomba kujiuzulu kupisha siasa za 'kihuni' ndani ya Chama.
 

Attachments

  • 2300404_Nimeikuta_from_archives__expressionless___Hebu_tupia_caption_hapa_.._ziwe_fupifupi_plz...jpg
    2300404_Nimeikuta_from_archives__expressionless___Hebu_tupia_caption_hapa_.._ziwe_fupifupi_plz...jpg
    31.7 KB · Views: 1
Atakuwa kaamua kupumuzika siasa.

Anamakandokando mengi sana huyu mzee.
Atulie tu.
 
L
Lakini kwa wakati huu ambapo Jiwe anakiendesha hiko chama kama vile anavyoiendesha familia yake ya mama Jesca, hakika safari hii ni lazima chama kitamfia mikononi mwake
Chadema na upinzani uko ktk hali mbaya. Sisiemu ya jpm inaimarika. Uthibitisho ni nyie bavicha hamlali mkiiombea mabaya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom