johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Kwa hicho kinyesi chako cha Machame!Najua hapo unawashwa washwa baada ya kusikia Mwanaume ntakupanda next week
Tuliza Mshono
Sent from my Nokia 6.1 using Tapatalk
JAMBO ILI LIWE KASHFA ni lazima liwe la kweli. kama likiwa si la kweli inakuwa ni UZUSHI.ama UONGO.
Wakati Membe akitamba kuwa alienda mbele ya kamati ya maadili ya CCM kuwafunda na kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali, Kinana amegoma kufika mbele ya kamati hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Kinana ameona ni kama kudharauliwa kwa kuitwa kuhojiwa mambo ambayo kimsingi ni malalamiko aliyotoa kuhusu namna alivyokuwa akipakwa matope na mtu anayejiita Cyprian Musiba. Inaelezwa kuwa aliyetakiwa kuitwa ni Musiba na siyo Kinana.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ndani ya chama, Kinana jana ijumaa alitakiwa kuwepo mbele ya kamati hiyo ya maadili lakini alisubiriwa hadi jioni na hakuna taarifa yoyote rasmi iliyopatikana juu ya kutokuhudhuria kwake mbele ya kamati hiyo.
Aidha hakutuma ujumbe wowote wa udhuru kuelezea kuhusu yeye kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo kama ilivyopangwa.
Tusubiri tuone.
Mmmi nadhani Ccm wali chemka mahali, alie takiwa kuitwa kuhojiwa alikuwa ni Musiba na sio hao walio itwaJana tarehe 8/2/2020 ndiyo ilikuwa siku tuliyotangaziwa kuwa makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdrahman Kinana na Yusuph Makamba, watafika mbele ya Kamati ya maadili ya CCM, kuwahoji kwa vitendo vyao vinavyodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya Chama chao cha CCM
Umma wa watanzania walikuwa wametega masikio yao kwa hamu kubwa huko Dodoma kwenye jengo linalofahamika kama "white house" kilikotarajiwa kufanyika kikao hicho ili kujua mbivu na mbichi
Hata hivyo habari zilizotufikia ni kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM "wamegoma" kufika katika kikao hicho ili kuhojiwa.
Tetesi zipo nyingi zinazosemwa kuhusu sababu za makatibu hao wakuu wastaafu kutohudhuria kikao hicho, lakini sababu kuu inayotolewa ni hii ya makatibu hao wakuu kudaiwa kukitosa chama hicho na kuamua kujivua uanachama wa CCM
Ndipo hapo tunapomtaka Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole ajitokeze hadharani na kutujulisha ni nini kimejitokeza hadi kusababisha makatibu hao wakuu wastaafu "kugoma" kuitikia mwito wa Chama chao ili wahojiwe?
Nadhani Katibu mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole, atajitokeza hadharani na kulitolea ufafanuzi suala hili nyeti na lenye maslahi mapana kwa Taifa ili kupoza kiu ya mamilioni ya watanzania
Kama tetesi tunazozisikia mitaani kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM watakuwa wameamua kukitupa mkono chama hicho, kutokana na kutorodhika na mwenendo wa kibabe wa Jiwe, na kusahau juhudi kubwa waliyoifanya wao ya kuhangaika usiku na mchana, ili kuhakikisha wanamsimika yeye kuwa Mkuu wa nchi, basi tuhesabu kuwa chama hicho kikongwe kabisa barani Afrika, tunaelekea kukizika rasmi!
Kumuita Lowasa Captain ni u Maaluni
Ni kama vile umepanic!Hakuna mtu anayeweza kustaafu siasa kwa kurudisha kadi ya chama, bali mtu anarudisha kadi ya chama kama ishara ya kujitoa kwenye chama husika.
By the way hiyo story ya Iddi Amin hata haiendani na mada husika.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaaa.......!Naona CCM wameanza michezo yao mwaka wa uchaguzu huu.
Kama nimeelewa sawasawa, ni kwamba:sijakuelewa mkuu
Maji yameshakorogeka.Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.
Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.
Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
Samahani kuwaweka nini sentensi ya mwisho naomba usisitiza mpendwa katika ImmanSijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.
Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.
Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.