Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.
Wakati Membe akitamba kuwa alienda mbele ya kamati ya maadili ya CCM kuwafunda na kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali, Kinana amegoma kufika mbele ya kamati hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Kinana ameona ni kama kudharauliwa kwa kuitwa kuhojiwa mambo ambayo kimsingi ni malalamiko aliyotoa kuhusu namna alivyokuwa akipakwa matope na mtu anayejiita Cyprian Musiba. Inaelezwa kuwa aliyetakiwa kuitwa ni Musiba na siyo Kinana.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ndani ya chama, Kinana jana ijumaa alitakiwa kuwepo mbele ya kamati hiyo ya maadili lakini alisubiriwa hadi jioni na hakuna taarifa yoyote rasmi iliyopatikana juu ya kutokuhudhuria kwake mbele ya kamati hiyo.

Aidha hakutuma ujumbe wowote wa udhuru kuelezea kuhusu yeye kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo kama ilivyopangwa.

Tusubiri tuone.
FB_IMG_1581233838628.jpg
 
Hakuna mtu anayeweza kustaafu siasa kwa kurudisha kadi ya chama, bali mtu anarudisha kadi ya chama kama ishara ya kujitoa kwenye chama husika.

By the way hiyo story ya Iddi Amin hata haiendani na mada husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm ni chama cha kigaidi ndo maana viongozi na wanachama wanahubiri kuua watz huku wakiiharibu nchi vibaya kiuchumu na ushirikiano kimataifa huku wakiifanya chato nchi kamili
 
Jana tarehe 8/2/2020 ndiyo ilikuwa siku tuliyotangaziwa kuwa makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdrahman Kinana na Yusuph Makamba, watafika mbele ya Kamati ya maadili ya CCM, kuwahoji kwa vitendo vyao vinavyodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya Chama chao cha CCM

Umma wa watanzania walikuwa wametega masikio yao kwa hamu kubwa huko Dodoma kwenye jengo linalofahamika kama "white house" kilikotarajiwa kufanyika kikao hicho ili kujua mbivu na mbichi

Hata hivyo habari zilizotufikia ni kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM "wamegoma" kufika katika kikao hicho ili kuhojiwa.

Tetesi zipo nyingi zinazosemwa kuhusu sababu za makatibu hao wakuu wastaafu kutohudhuria kikao hicho, lakini sababu kuu inayotolewa ni hii ya makatibu hao wakuu kudaiwa kukitosa chama hicho na kuamua kujivua uanachama wa CCM

Ndipo hapo tunapomtaka Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole ajitokeze hadharani na kutujulisha ni nini kimejitokeza hadi kusababisha makatibu hao wakuu wastaafu "kugoma" kuitikia mwito wa Chama chao ili wahojiwe?

Nadhani Katibu mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole, atajitokeza hadharani na kulitolea ufafanuzi suala hili nyeti na lenye maslahi mapana kwa Taifa ili kupoza kiu ya mamilioni ya watanzania

Kama tetesi tunazozisikia mitaani kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM watakuwa wameamua kukitupa mkono chama hicho, kutokana na kutorodhika na mwenendo wa kibabe wa Jiwe, na kusahau juhudi kubwa waliyoifanya wao ya kuhangaika usiku na mchana, ili kuhakikisha wanamsimika yeye kuwa Mkuu wa nchi, basi tuhesabu kuwa chama hicho kikongwe kabisa barani Afrika, tunaelekea kukizika rasmi!
Mmmi nadhani Ccm wali chemka mahali, alie takiwa kuitwa kuhojiwa alikuwa ni Musiba na sio hao walio itwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Musiba aliitwa lini? Bravo to Comrade Kanali Kinana.
 
Amenituma nikamuwakilishe,nitatokea kikaangoni si muda mrefu
 
Kiongozi tuliyenaye Jiwe ambaye anapenda kuabudiwa kwa kuombwa msamaha hata na watu ambao hawajamkosea hana tofauti na akina Adolf Hitler na Benito Mussolini.

Hawa akina Abrahman Kinana na Yusuf Makamba walipaswa wawe washauri wake na siyo kushauriwa na Pole Pole na Bashiru Ally au Makonda. Hata waliyoyaongea kwenye simu alizowarekodi kijinai bado ni ushauri mzuri wa kukijenga chama, Mwenyekiti wa CCM kama angekuwa na akili nzuri angechukulia mawazo ya wale wazee positively kuliko kuwadhalilisha kwa kuyaanika na kutaka wamuombe msamaha.

Hili likiendelea usijeshangaa siku nyingine ikatokea akamdhalilisha JK na Mkapa.

Huyu Jiwe ni Dikteta tu sawa na Hitler na Mussolini:
 
sijakuelewa mkuu
Kama nimeelewa sawasawa, ni kwamba:

Mwenyekiti amewafokea Polepole, Bashiru na wajumbe wa kamati, lakini zaidi amefokewa Polepole kwa kuhidlsiwa kuwa ndiye aliyevujisha siri.

Kinana na Makamba wameandika barua za kujiondoa kwenye chama kwa maana ya kustaafu siasa. Kamati baada ya kupilokea barua zao ikawaomba kuwa wasiliseme jambo hilo kwa umma, nao wakawaambia kuwa, na wao (wajumbe wa kamati) wasiseme juu ya jambo hilo.

Cha kushangaza baada ya muda mfupi, jambo tayari limetoka na watu wanajua. Mwenyekiti amechukia, na kuwafokea sana Polepole na Bashiru, kiasi cha bwana Bashiru kuondoka ofisini na kwenda kupumzika.

Hivi ndivyo nilivyoelewa.
 
Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.

Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.

Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
Maji yameshakorogeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.

Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.

Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
Samahani kuwaweka nini sentensi ya mwisho naomba usisitiza mpendwa katika Imman
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom