Magonjwa Mtambuka
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 32,246
- 31,176
Tayari wameshapokelewa ufipa. Wanangoja kupitishwa kugombea urais. Nimeambiwa (na chanzo cha uhakika), kesho kutwa makamanda watatangaziwa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa kuwa demokrasia ilikuwa juu zaidi ya sasa, walizomewa, walitusiwa hata kupigwa, sio leo, ole wake umguse mwenye nguo zile, inamaana wewe ujapata ujumbe?Ni afadhali CCM ife izikwe kabisa kuliko kurudi kwenye CCM ya Makamba na Kinana; kuvaa jezi ya Yanga mtaani ilikuwa taabu sana enzi hizo. Siku hizi naziona nyingi tu.
Na kibaya zaidi malalamiko yao kuhusu kulalamikia kudhalilishwa kwao na huyo mtu anayeitwa Musiba, yakatupwaaisee.. hiki chama kinaenda kumfia mtu kabala hata ya kumaliza muda wake, haiwezekani wazee wenye hadhi ya akina kinana ambao wameshiriki kwa kiasi kikubwa kuwaweka watu madarakani eti wakadhalilishwe na vikamati uchwara, ni bora wajivue tu kwani hamna namna!
inauma sana, huku wakikumbuka wamemfanyia mtu kampeni mpaka leo hii yupo madarakani atokee muhuni tu na aanze kuwabeza, aisee...!Na kibaya zaidi malalamiko yao kuhusu kulalamikia kudhalilishwa kwao na huyo mtu anayeitwa Musiba, yakatupwa
Nashukuru niliwahi kushauri wasikubali kuhojiwa, ila wameenda hatua zaidi ya kujivua uanachama, si mbaya, nilisema ni vema wangewafuata na kuongea nao kungejenga zaidi! Sasa pole pole kweli umwite mzee Makamba, kisa madaraka! Naamini adabu ipo chini sana!Jana tarehe 8/2/2020 ndiyo ilikuwa siku tuliyotangaziwa kuwa makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdrahman Kinana na Yusuph Makamba, watafika mbele ya Kamati ya maadili ya CCM, kuwahoji kwa vitendo vyao vinavyodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya Chama chao cha CCM
Umma wa watanzania walikuwa wametega masikio yao kwa hamu kubwa huko Dodoma kwenye jengo linalofahamika kama "white house" kilikotarajiwa kufanyika kikao hicho ili kujua mbivu na mbichi
Hata hivyo habari zilizotufikia ni kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM "wamegoma" kufika katika kikao hicho ili kuhojiwa.
Tetesi zipo nyingi zinazosemwa, kuhusu sababu za makatibu hao wakuu wastaafu kutohudhuria kikao hicho, miongoni mwake likiwa hili la kujivua uanachama wa CCM
Ndipo hapo tunapomtaka Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole ajitokeze hadharani na kutujulisha ni nini kimejitokeza hadi kusababisha makatibu hao wakuu wastaafu "kugoma" kuitikia mwito wa Chama chao ili wahojiwe?
Nadhani Katibu mwenszi wa CCM, Humphrey Polepole, atajitokeza hadharani na kulitolea ufafanuzi suala hili nyeti na lenye maslahi mapana kwa Taifa ili kupoza kiu ya mamilioni ya watanzania
Wacha wafu wazikane wenyewe........Nashukuru niliwahi kushauri wasikubali kuhojiwa, ila wameenda hatua zaidi ya kujivua uanachama, si mbaya, nilisema ni vema wangewafuata na kuongea nao kungejenga zaidi! Sasa pole pole kweli umwite mzee Makamba, kisa madaraka! Naamini adabu ipo chini sana!
Ogopa sana kukaa meza kuu, ukiwa pale mawazo na akili yote yanakuambia kesho haipo na wewe ndio alpha na omega!FaizaFoxy,
Na sie wengine tunashangaa kuwa ni vipi leo hawa watu hawana heshima na staha kwa wazee wao?
Kinana ni muislam ila Makamba dini yake ni changanyikeni kama makande
Wakisema ukweli sio kumjashifu, Tofautisha ukweli na kashifaWewe ulitakaje? Lakini si ni kweli walimkashifu Rais?
Kabisa hawa na wazee na wamekifanyia chama mambo mengi sana hata kabla ya viongozi wa sasa kujiunga na chama leo watoto wanawaita wazee kwa kukosa adabu? hapa ndugu zangu wa CCM wamewakosea sana hawa wazee maana walishapumzika siasa na kubaki kama wanachama tu. Kwa hili ni CCM kuwaomba msamaha hawa wazee sio kinyume chake ni udhalilishaji wa hali ya juu kabisa hata mimi ningekuwa kati ya hawa wazee ningefanya the same.Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.
Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.
Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.