Jana tarehe 8/2/2020 ndiyo ilikuwa siku tuliyotangaziwa kuwa makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdrahman Kinana na Yusuph Makamba, watafika mbele ya Kamati ya maadili ya CCM, kuwahoji kwa vitendo vyao vinavyodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya Chama chao cha CCM
Umma wa watanzania walikuwa wametega masikio yao kwa hamu kubwa huko Dodoma kwenye jengo linalofahamika kama "white house" kilikotarajiwa kufanyika kikao hicho ili kujua mbivu na mbichi
Hata hivyo habari zilizotufikia ni kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM "wamegoma" kufika katika kikao hicho ili kuhojiwa.
Tetesi zipo nyingi zinazosemwa kuhusu sababu za makatibu hao wakuu wastaafu kutohudhuria kikao hicho, lakini sababu kuu inayotolewa ni hii ya makatibu hao wakuu kudaiwa kukitosa chama hicho na kuamua kujivua uanachama wa CCM
Ndipo hapo tunapomtaka Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole ajitokeze hadharani na kutujulisha ni nini kimejitokeza hadi kusababisha makatibu hao wakuu wastaafu "kugoma" kuitikia mwito wa Chama chao ili wahojiwe?
Nadhani Katibu mwenszi wa CCM, Humphrey Polepole, atajitokeza hadharani na kulitolea ufafanuzi suala hili nyeti na lenye maslahi mapana kwa Taifa ili kupoza kiu ya mamilioni ya watanzania