Ni wazi kwa kitendo cha Mzee Kinana na Mzee Makamba makatibu wakuu wastaafu waliokuwa na mvuto mkubwa kuandika barua ya kujitoa CCM chama chetu kimekutana na dhoruba Kali sawa na kusambaratika.
Nini chanzo cha yote hayo? Bila kupepesa macho ni kitendo cha wao kuhoji kwa nini mtu anayejiita mwanaharakati mtetezi wa Rais Magufuli anawavunjia heshima na kuwatukana na haguswi? Jee anatumwa na Magufuli mwenyewe? Kwa sababu angekuwa hatumwi naye lazima ange shughulikiwa.
Baada ya hapo ndio misukosuko ya ajabu ikaanza.
Sasa jee kweli chama chetu kikongwe kama CCM ambacho kinaheshimika Afrika nzima na hasa kusini mwa Afrika kinaweza kweli kukubali kusambaratishwa na mjinga mmoja kama Musiba na maandiko na kauli zake kwa vile anabebwa?
Na kwa nini mwenyekiti wetu amezungukwa na watu waletao mtafaruku na jamii na hata kusababishia heshima ya chama kupotea naye haambiwi kitu kuhusu watu hao mfano RC Makonda?
Ukiangalia kwa makini tatizo hapa ni mwenyekiti, chama kinageuka kundi LA wahuni na misingi inapotea kabisa.
Kukubali wanachama waandamizi kukikimbia chama ni ujinga mkubwa bora kumtimua madarakani mwenyekiti anayekipoteza chama na kukivuruga. Naamini hata watangulizi wake wote katika hili la kina Kinana hawamuungi mkono na kacheza karata vibaya kabisa.
Kinana nakumbuka ndiye alikuwa Kampeni meneja wa Mkapa kipindi cha pili na JK vipindi vyote viwili jee huyo ndio wa kutumiwa Musiba awatukane?
JPM must go, na inaanzia julai katika kupeperusha Bendera uchaguzi mkuu 2020 then tutamtoa uenyekiti.
Sasa CCM inatakiwa itoke mikononi mwa wasio kijua chama na kurudi mikononi mwa wenyechama yaani wanachama
Sent using
Jamii Forums mobile app