Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.
Acheni kumpa sifa MTU mpumbafu,mnamjadili sana Nate ndiyo atakacho
 
Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.

Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.

Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
Hivi Kachero si mjeda!!?
 
Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.

Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.

Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
Sahihi kabisa 👏👏👏
 
Wewe ulitakaje? Lakini si ni kweli walimkashifu Rais?
Kwani kuna watu ambao huwa faragha na wakaacha kuwateta wenzao? Nani aliwaambia waanike mambo ya faraghani? Ukinikuta ninakunya chooni utaenda kuitisha press na kutangaza wakati nilikuwa nimejisitiri? Kurusha zile audio lilikuwa kosa kubwa mnooooo!
 
aisee.. hiki chama kinaenda kumfia mtu kabala hata ya kumaliza muda wake, haiwezekani wazee wenye hadhi ya akina kinana ambao wameshiriki kwa kiasi kikubwa kuwaweka watu madarakani eti wakadhalilishwe na vikamati uchwara, ni bora wajivue tu kwani hamna namna!
Wewe chama hakina mtu mhimu, hayo yspo ndani ya chadema tu! Mbowee tuvushe! Huku ni chama tuvushee!

Kinanaa niz mkubwa kaua faru wetu wakutosha tu!
Kuna watu muhim nchi hii kuliko kinana.

Kuna makamanda, wakuu wa vikosi vya majeshi na wapigania nchi maarufu kuliko kinana na makamna.

Kinan ni jiziiii mkubwaa.

Walikuwepo wakawepo lakini walizima gafra sembuse kinan na makambaaa!!!
 
Rais wa nchi hateuliwi kwa kuandika vikaratasi na kuwaita vipofu wateue Rais wa nchi, JK alifanya kosa kubwa Sana ambalo analijutia Sana, Sasa jamaa anasema alisukumizwa tena hadharani
 
Vijana wa sasa wana la kujifunza.
CCM ikishakutumia ukachoka haina habari na wewe tena, utabezwa, utadharilishwa na kufanyiwa kila uovu.
Vijana mnaotumika na CCM mjitafakari na kuchukua hatua asubuhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana tarehe 8/2/2020 ndiyo ilikuwa siku tuliyotangaziwa kuwa makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdrahman Kinana na Yusuph Makamba, watafika mbele ya Kamati ya maadili ya CCM, kuwahoji kwa vitendo vyao vinavyodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya Chama chao cha CCM

Umma wa watanzania walikuwa wametega masikio yao kwa hamu kubwa huko Dodoma kwenye jengo linalofahamika kama "white house" kilikotarajiwa kufanyika kikao hicho ili kujua mbivu na mbichi

Hata hivyo habari zilizotufikia ni kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM "wamegoma" kufika katika kikao hicho ili kuhojiwa.

Tetesi zipo nyingi zinazosemwa kuhusu sababu za makatibu hao wakuu wastaafu kutohudhuria kikao hicho, lakini sababu kuu inayotolewa ni hii ya makatibu hao wakuu kudaiwa kukitosa chama hicho na kuamua kujivua uanachama wa CCM

Ndipo hapo tunapomtaka Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole ajitokeze hadharani na kutujulisha ni nini kimejitokeza hadi kusababisha makatibu hao wakuu wastaafu "kugoma" kuitikia mwito wa Chama chao ili wahojiwe?

Nadhani Katibu mwenszi wa CCM, Humphrey Polepole, atajitokeza hadharani na kulitolea ufafanuzi suala hili nyeti na lenye maslahi mapana kwa Taifa ili kupoza kiu ya mamilioni ya watanzania
Mtu ambaye si mwanachama wako hawezi kuja labda kama Ana wito wa polisi kuelewa mahakamani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom