Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.
Kwa hakika kabisa kwenye zile sauti Membe hajatenda kosa lolote la jinai wala la kinidhamu.
Labda harakati zake zingine au kama kuna sauti zingine hatukuwekewa hadharani.

Sasa huyu mzee Kinana kajua ana makosa tena makubwa tu ya kisheria, hawezi kujileta mtegoni kama mjinga.
Huwezi kusema raisi wa nchi kachanganyikiwa wakati wewe sio daktari wake, hata kama wewe ni daktari hupaswi kusema hadharani taarifa za mgonjwa bila utaratibu rasmi, sasa hiyo ni kwa mtu yeyote yule jiulize kwa mkuu wa nchi inakuwaje?

Kinana akijileta kaisha, atachukuliwa hatua za kisheria.
Nawaza kitoto zaidi wakubwa mnisaidie kutafakari.
Ndugu, Kinana hakuyasema hayo hadharani, yeye ndiye aliyedukuliwa na ikawekwa hadharani. Kwanza haki yake imedhulumiwa, na raisi alipisema kuna wataalamu walimuambia sauti zile ni zao, hapo alitudhihirishia kuwa serekali ndiyi ikiyomdukua.

Watu kutetana faragha ni moja ya maisha ya kawaida. Hapa aliyejitukana ni serekali yetu yenyewe kwa kudukua simu za watu na kuzifujisha kwa umma, alafu bila kujijua wakajitaja wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania kwa unafiki.

Asingeitwa mngesema akuitwa kujieleza, na pale barua za wito zilivyo chelewa mlisema wanaogopwa.
 
Jana tarehe 8/2/2020 ndiyo ilikuwa siku tuliyotangaziwa kuwa makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdrahman Kinana na Yusuph Makamba, watafika mbele ya Kamati ya maadili ya CCM, kuwahoji kwa vitendo vyao vinavyodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya Chama chao cha CCM

Umma wa watanzania walikuwa wametega masikio yao kwa hamu kubwa huko Dodoma kwenye jengo linalofahamika kama "white house" kilikotarajiwa kufanyika kikao hicho ili kujua mbivu na mbichi

Hata hivyo habari zilizotufikia ni kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM "wamegoma" kufika katika kikao hicho ili kuhojiwa.

Tetesi zipo nyingi zinazosemwa kuhusu sababu za makatibu hao wakuu wastaafu kutohudhuria kikao hicho, lakini sababu kuu inayotolewa ni hii ya makatibu hao wakuu kudaiwa kukitosa chama hicho na kuamua kujivua uanachama wa CCM

Ndipo hapo tunapomtaka Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole ajitokeze hadharani na kutujulisha ni nini kimejitokeza hadi kusababisha makatibu hao wakuu wastaafu "kugoma" kuitikia mwito wa Chama chao ili wahojiwe?

Nadhani Katibu mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole, atajitokeza hadharani na kulitolea ufafanuzi suala hili nyeti na lenye maslahi mapana kwa Taifa ili kupoza kiu ya mamilioni ya watanzania

Kama tetesi tunazozisikia mitaani kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM watakuwa wameamua kukitupa mkono chama hicho, kutokana na kutorodhika na mwenendo wa kibabe wa Jiwe, na kusahau juhudi kubwa waliyoifanya wao ya kuhangaika usiku na mchana, ili kuhakikisha wanamsimika yeye kuwa Mkuu wa nchi, basi tuhesabu kuwa chama hicho kikongwe kabisa barani Afrika, tunaelekea kukizika rasmi!
 
Polepole na akili yake atakuja kujibu tena bila tahadhari atatumia magazeti yake yote
Ndiyo maana Mkuu vipik2 tunamtaka Katibu Mwenezi wa CCM ajitokeze hadharani na kutueleza watanzania ni sababu zipi zilizofanya makatibu hao wakuu wastaafu wadharau kikao hicho muhimu cha maadili cha Chama chao na kukidharau na kutoweza kuhudhuria?
 
Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.

Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.

Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
 
Wameishaandika barua za kujivua uanachama CCM. Kwahiyo sio wana CCM na hawalazimiki kuhojiwa! Waliwahi kuwa Makatibu wakuu wa CCM na wanajua hadhabu ya kosa walilotenda ni nini. Hivyo wameamua kusepa wenyewe fasta! Hahhahaha
Lakini inakera sana......

Wao makatibu wakuu wastaafu wa CCM walimwandikia barua Msekwa, kuelezea kusikitishwa kwao na kitendo cha mwanachama mwenzao Musiba, kuwadhalalisha na kuwaita kuwa wanamkwamisha Rais Magufuli katika juhudi zake za kuwaletea maendeleo watanzania........

Badala ya Kamati hiyo ya maadili kumwita pia huyo anayeitwa Musiba ili kumhoji kuhusu tuhuma zake ili aeleze hao makatibu wakuu wastaafu wanakwamisha vipi juhudi za Rais katika kuleta maendeleo, badala yake wanawaita hao makatibu wakuu wastaafu ili wajibu tuhuma za sauti zao kuvuja ikidaiwa kuwa wanamkashifu Mheshimiwa Rais!

Ndiyo tatizo la huyu jamaa, kutaka kukiendesha hiko chama chake kwa ubabe, badala ya nguvu ya hoja
 
Busara hakuna, chama gani wazee kama hao Kinana na Makamba wahofie kutoa maoni yao? Kama watu wa hadhi ya kinana na makamba wawe na hofu ya kutoa maoni kuboresha utendaji wa serikali na chama, wananchi wa kawaida itakuwaje? Kuna watu wana USHAMBA sana wa madaraka! Hawathamini kabisa michango ya watu wengine!
 
Jana tarehe 8/2/2020 ndiyo ilikuwa siku tuliyotangaziwa kuwa makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdrahman Kinana na Yusuph Makamba, watafika mbele ya Kamati ya maadili ya CCM, kuwahoji kwa vitendo vyao vinavyodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya Chama chao cha CCM

Umma wa watanzania walikuwa wametega masikio yao kwa hamu kubwa huko Dodoma kwenye jengo linalofahamika kama "white house" kilikotarajiwa kufanyika kikao hicho ili kujua mbivu na mbichi

Hata hivyo habari zilizotufikia ni kuwa makatibu hao wakuu wastaafu wa CCM "wamegoma" kufika katika kikao hicho ili kuhojiwa.

Tetesi zipo nyingi zinazosemwa, kuhusu sababu za makatibu hao wakuu wastaafu kutohudhuria kikao hicho, miongoni mwake likiwa hili la kujivua uanachama wa CCM

Ndipo hapo tunapomtaka Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole ajitokeze hadharani na kutujulisha ni nini kimejitokeza hadi kusababisha makatibu hao wakuu wastaafu "kugoma" kuitikia mwito wa Chama chao ili wahojiwe?

Nadhani Katibu mwenszi wa CCM, Humphrey Polepole, atajitokeza hadharani na kulitolea ufafanuzi suala hili nyeti na lenye maslahi mapana kwa Taifa ili kupoza kiu ya mamilioni ya watanzania


MAKATIBU wakuu wastaafu wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wamejivua uanachama wa chama hicho.

Habari zilizoifikia SAUTI KUBWA zinasema Kinana na Makamba walijiondoa rasmi CCM kwa maandishi. Barua zao, kila mmoja na ya kwake, zilifikishwa ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM tarehe 7 Februari 2020.

Chanzo kinachoaminika kutoka CCM Makao Makuu kimeiambia SAUTI KUBWA: “Barua zao zimefika kwa nyakati tofauti, zimepokelewa. Lakini inaonekana kama walikuwa wameziandika muda mrefu baada ya kushauriana, maana zinafanana na zimewasilishwa siku moja. Taarifa hizi zilipofikishwa kwa Mzee (Rais John Magufuli) zilimvuruga kwa kweli.”

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ambacho hakitatajwa hapa, Rais Magufuli, baada ya kupokea ujumbe wa Kinana na Makamba kujivua uanachama, aliwaomba wazee wawili waandamizi – Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Spika Mstaafu Pius Msekwa – wamsaidie kuzungumza na akina Kinana ili kuwashawishi wabadili msimamo wao.

Hata hivyo, Kinana na Makamba wamegoma kusikiliza ushawishi wa mtu yeyote. Katika barua zao za kujiondoa CCM, kwa mujibu wa chanzo chetu, Kinana na Makamba waliambatanisha pia kadi zao za uanachama.

“Tayari wameturudishia kadi zetu, maana yake wao si wanachama wetu tena,” kimesema chanzo hicho.

Kinana na Makamba ni miongoni mwa makatibu wakuu wanaoheshimika katika CCM, wenye ushawishi, na ambao wametumikia nchi katika nyadhifa mbalimbali kuanzia jeshini hadi serikalini na kwenye chama.

Siku ambayo walikabidhi barua na kadi zao na kutangaza rasmi kujiondoa CCM, ndiyo siku walipotarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM iliyoagizwa na Rais Magufuli katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), ili wajieleze kuhusu waraka walioanidika kwa Baraza la Wazee la chama hicho wakilalamikia kubezwa na kudhalilishwa na mhuni mmoja anayetumia jina la rais kudhihaki na kushambulia wakosoaji wa rais na serikali.

Mbali na Kinana na Makamba, mwingine aliyeitwa kuhojiwa na kamati hiyo ni Bernard Membe, waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye aliunga mkono waraka wa wazee hao, na pia alidukuliwa akizungumza katika simu mambo ambayo hayakumfurahisha Rais Magufuli.

Yeye alikutana na kamati hiyo Mjini Dodoma Ijumaa tarehe 7, Februari 2020; na baada ya mahojiano alionekana mwenye kujiamini na mwenye furaha. Mmoja wa wajumbe walioshiriki mahojiano hayo amezungumza na SAUTI KUBWA kwa sharti la kutotajwa, akisema: “Tulijuta kumuita Membe. Kuna maswali amehoji na masuala amezungumza nasi hadi tukahisi yeye ndiye anayetuhoji. Ukweli ni kwamba chama chetu kinahitaji mabadiliko makubwa ya kimsingi, maana kuna shida mahali. Bwana mkubwa anatupelekesha, na watu jasiri wa kumwambia ukweli hawapo, tunaishia kuagizwa tu, hata kutenda mambo yaliyo kinyume cha misingi ya CCM. Membe ametukumbusha yote haya. Kwa kweli, sijui kinachoofuata.”

Hata hivyo, SAUTI KUBWA iliambiwa wiki iliyopita kuwa agizo la kamati kuwahoji wakongwe hao lilikuwa kama igizo tu, kwani Rais Magufuli na watu wake walishaamua kuwa Membe na Kinana wavuliwe uanachama, na Mzee Makamba apewe onyo kali.

Kwa Kinana na Makamba kujivua uanachama na kugoma kuhojiwa, wamewaza hatua mbili mbele ya Magufuli. Chama hakiwezi kuwahoji kwa kuwa wao hawafungwi tena na nidhamu wala maadili ya CCM kwa kuwa si wanachama CCM.

Ingawa barua zao zilipelekewa kimya kimya, na uongozi wa juu wa CCM umekuwa unahangaika kuzuia taarifa hizi kuvuja, zilivuja mapema mno; na kitendo chao cha kutofika mbele ya kamati kuhojiwa kimezua maswali na mjadala mpana ndani nanje ya CCM.

Baadhi ya wadau wa siasa za Tanzania wanasema inawezekana kitendo hiki kikawaingiza wote wawili, au mmoja wao, kwenye matata makubwa, kwani uongozi wa CCM ni wa visasi, unaweza kutaka kuwakomoa na kuwadhalilisha.

Profesa mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema: “Tusishangae sasa kusikia siku moja Kinana au Makamba wametiwa mbaroni na wanashitakiwa kwa utakatishaji fedha, maana hii ndiyo fimbo mpya ambayo inatumika kuumiza wanaotofautiana na watawala. Lakini iwapo watashitakiwa umma utajua kuwa sababu hasa si uhalifu wao bali ni hii barua yao na uamuzi wao.”

Kiongozo mmoja mwandamizi wa CCM ameiambia SAUTI KUBWA: “Kiukweli, Mzee Kinana na Mzee Makamba hawana cha kupoteza. Nadhani sisi ndio tuna cha kupoteza, maana ukisoma waraka unaowasababishia haya yote utagundua kuwa wao ni watetezi wa misingi ya chama chetu. Wanachotetea ndicho wanaCCM wote tunapaswa kutetea, lakini sasa tofauti iliyopo kati yetu na wao ni kwamba wao wameonyesha ujasiri ambao sisi hatuna. Wengi wetu tumebaki kutii maagizo ya bwana mkubwa, huku chama kinaporomoka!”

SAUTI KUBWA inatambua kuwa kuna mtifuano mkubwa ndani ya CCM ambao haujawahi kutokea tangu uwepo wa chama hicho, ingawa wanafanikiwa kuufunika kwa kutishana – kwa kutumia vuombo vya dola.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom