Kinana kuongea na mamlaka bodaboda wabebe abiria zaidi ya 1 (mshikaki)

Kinana kuongea na mamlaka bodaboda wabebe abiria zaidi ya 1 (mshikaki)

Hafai kabisa!
Huu ni ujuha kwenye siasa kaka yangu Kinana.

Kila siku askari wa usalama barabarani wanapambana kukomesha upakiaji wa mishikaki kwenye bodaboda.

Wewe kwa kutaka kupata wapiga kura unaamua kuwaruhusu hao bodaboda wabebe mishikaki?

Yaani unathamini kura kuliko uhai wa watanzania?
Kinana hapa umekengeuka.

Watanzania tuamke hawa ccm wamekusudia kutumaliza makusudi.
View attachment 2701108
afai
 
Wanajua wanawaongoza wapmbv na wajinga ,huoni hapo bodaboda wanashangilia

Ova
 
Nimeshangaa kuona na kusikia Kinana akiwaambia bodaboda kuwa ataiambia mamlaka ya usimamizi usalama barab

Una mtazamo gani juu ya kauli hii?.
Mungu utuhurumie hawa viongozi wetu kwakweli ni zaidi ya tunavyo fikiria, yaani kweli kuruhusu kuvunja sheria kwaajili ya manufaa ya wao kubaki madarakani? Kitaalamu hawaangalii wao wanaangalia wao kupata kupigiwa kura? Mungu awasamehe.
 
Hizo kauli zao,
Sometimes waweza fikiria kuwa hao jamaa ni wagonjwa…!
Kutunza ulimi ni hekima kubwa sana..
 
Hawa wazee naona wasiwe wanapewa vipaza sauti sasa
Kama ni ushauri wawe wanatoa kimya kimya kwenye vikao vyao vya ndani
 
Watanganyika tumieni akili hao wageni hawana uchungu na nyie hata mkifa
 
Wakati huo maeneo mengi Noah hazisajiliwi tena kubeba abiria kisa ajali ila zinabeba bila vibali na hivyo kuikosesha pesa mapato.
 
Nimeshangaa kuona na kusikia Kinana akiwaambia bodaboda kuwa ataiambia mamlaka ya usimamizi usalama barabarani waondie zuio la mishkaki yaani kubeba hadi abiria 3.

Sababu kuu anasema hii itaongeza kipato kwa waendesha boda boda.

Kibaya zaidi akasema kuwa...kuna shida gani kama abiria wenyewe wametaka kubebwa hadi watatu.

Huu sio uongozi kwani wote tunafahamu jinsi boda boda zinapoteza maisha ya watu wengi.

Kiongozi asiyejali maisha ya raia huyo ni muuaji

========

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amesema CCM inakwenda kuzungumza na Serikali kuangalia sheria ya kuzuia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda kuruhusia kubeba abiria zaidi ya mmoja (mshikaki)

Kinana amesema hayo wakati akipokelewa na Viongozi, Wanachama wa CCM na Wananchi wa Bariadi mkoa wa Simiyu, ikiwa ni mendelezo wa ziara yake ya kuangalia uhai wa chama, utekelezaji wa llani ya CCM na kuongea na Wananchi katika maeneo mbalimbali.

Una mtazamo gani juu ya kauli hii?.
si kinana wala mtoto wake SABRA anayepanda bodaboda so hajui kinachotokea huko barabarani shenzi huyu
 
Back
Top Bottom