Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni sahihi maana wanakuja bungeni kulinda maslahi yao ya muungano.

Kimsingi hawapaswi pia kujadili masuala yasiyohusu muungano. Sema hii nchi imejaa uchawa sana.
 
Eti machifu. Hivi ccm wanataka nini kutoka machifu kama sio kutaka kuleta ukabila tu. Machifu jinsi wanapatikana nani anawachagua kama sio kutaka kuleta wababe au wanyonyaji wanaodai kutumikiwa na kusujudiwa. Tunakuombeni sana ccm na serikali yenu kuach kuendekeza uchifu. Kwa mara ya mwisho tuliwasikia wakitaka kutambuliwa kikatiba kwa hivyo bila shaka kutaka malipo toka bajeti ya taifa.
 
Kinana namkubali Sana. Kiujumla hapa amekiri Chama chake kimeshindwa Kwa hoja. Hata ukipima mzani wa hoja za vyama hivi utajua ipi ina uzito.
1.Katiba CCM inakubali katiba inahitajika na umesema Wananchi wanahitaji katiba. Kama Wananchi wanahitaji katiba Nani wa kuwaambia tena subirini? Au kuna kikundi kina nguvu kuliko Wananchi?
2.Uzanzibar wa Samia. Kwa hili ni Nape na papara zake aliyejikoroga lkn hata Kinana ameshindwa kujibu.
3.Majimbo na Idadi ya watu. Kwa hili amejikoroga tu. Anasema Idadi ya watu si hoja mwisho anasema si kigezo pekee. Hapa ina maana ni kigezo muhimu vinginevyo Tarafa ambazo ziko mbali na Idadi ndogo ya watu zingeshapewa hadhi ya Majimbo.
4.Alipojikoroga zaidi ni kwenye Uhuru WA kujieleza na mikutano ya hadhara. Serikali iliyozuia mikutano Kwa kutumia Polisi na Jeshi ni ya ACT?
 
Kinana katoa Siri Chadema mlitaka vyama vingine visihusishwe kwenye kikosi Kazi Cha Katiba mpya
Kwani ule mchakato wa katiba mpya ulioandsliwa na Jaji Warioba na CCM wakatia mpira kwapani uliandaliwa na Chadema? Ni watanzania wote bila kujali vyama, kusingizia Chadema ni kupotosha umma.
 
Bora wangekuwa wanamsema,Sasa wanamtukana.Hata Sasa akiamua kupiga marufuku maandamano hakuna wa kunyanyua mdomo.
 
Kinana hii siyo hisani ya samia ni katiba na mahitaji ya nyakatk

Ukifikiri hivyo ni sawa na kusema samia asingekuwa raisi kama wale wahuni wangekataa asiwe

Samia hana mamlaka kuzuia mikutana
Kama ambavyo wahuni hawana mamlaka kuzuia asiwe raisi
 
πŸ™„πŸ™„πŸ™„
 
Akisema au wakiamua kuuza Bandari itakuwaje ? Hata kama wanaweza na watafanya hivyo kwa ulaghai ila sio sawa...., Sababu unaweza kufanya ndivyo sivyo kwa wakati fulani haimaanishi usipofanya usifiwe kwa kutokufanya;...

Vilevile sababu unalipwa ufanye vyema haimaanishi usipofanya usisemwe sababu kuna mabaya zaidi ungeweza kuyafanya na haujayafanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…