KINANA: Urais wa Samia sio wa Kikatiba, amepatikana kwa Uchaguzi

Huyu ndio wanamwita mwalimu wa siasa labda mwalimu wa propaganda
 
Kinana hana usemi zaidi ya ku_ justify uhongo,
Si hamini kama kinana hajui utaratibu wa makamu wa Rais kuwa Rais,
Ingekuwa kuwa samia yupo hapo kikatiba basi baada ya Magufuli kufa tungerudia UCHAGUZI.....Ivyo basi Samia siyo Rais wa kuteuliwa kikatiba...
 
Katiba mbovu na hatari sana!!makamu anaweza shiriki njama za kumuua aliyeko madarakani ili achukue kijiti

Unataka katiba iitishe uchaguzi rais akifa? Si walioshindwa uchaguzi watafanya njama za kumuua aliyeko madarakani ili wajaribu tena kwenye uchaguzi mpya?
 
Kuna uwezekano mkubwa sana wanaojua kusoma na kuandika ni viongozi wetu tu.

Sisi wengine tunasubiri kusimuliwa tu kila kitu tena hatutakiwi kuuliza.

Kuuliza ni utovu wa nidhamu.
 
Ni rais wa katiba bhana. Mtu gani hana vision ya maana kwa nchi. Aende huko akapake miwanja na ma lip steak yake. Kuchukua tu urais anawatema wanamapinduzi na kuweka wapigaji. Anawasikiliza kina tonny blair maagent wa ubeberu na mabwana zake waliyomsapport kwenye enzi za ngo yake.
Sisi tumezoea siasa za jeuri kwa mabeberu na kutaka maendeleo ya usawa kiuchumi kwa raia. Samia kazi yake kutetea wapigaji tu.
Tumuombee atufikishe 2025 salama kisha wanachama wa chama cha mapinduzi watafute mwanamapinduzi kugombea urais.
 
Huo Ushahidi mbona hujawahi kuutoa hadharani? Ni kama hivyo, basi Mwambie Kinana kuwa mama yenu hakupata kuchaguliwa na sio Raisi kwa mjibu wa Katiba kama anavyodai.
 
Reactions: nao
Umesema kitu. Mangula was fair and true to the revolutionary principles of ccm. The current vice chairman is there to represent business interests .
 
Kwahiyo hapaswi kugombea tena urais 2025 kwani alishapita vipindi viwili akisaka kura?
Ndio nilipomsikiliza mtu anayedaiwa eti ndiye mjuzi wa Siasa nikasema kumbe ndiyo maana lichama na Serikali havina maono. Nilitegemea maelezo yake kuhusu hoja ya uraisi wa mama ingalimaliza kabisa mjadala badala yake ndio kwanza ameboronga na kujichanganya.
 
Ukwel ni kuwa Samia kapata Urais kwa sababu ya katiba! Zingine ni blahblah tu!
Sasa tunajiuliza Ni nani mkweli kati ya Kinana na Samia? Mama aliwahi kunukuliwa akiwaeleza wanawake wenzie kuwa yeye sio Raisi wa kuchaguliwa bali wa Katiba na hivi inabidi wanawake wampigie kura uchaguzi ujao ili awe Raisi wa kuchaguliwa na hao ndio watakuwa na Furaha ya kweli. Sasa Kinana Ni kama anarekebisha hiyo Kauli au anampa Tuition?
 
Kinana, aache kuwapotosha wananchi...anatakiwa atuambie tuko awamu ya ngapi? Kama ni awamu ya tano, Samia Suluhu Hassan ni Rais kwa mujibu wa kura alizopata Magufuli!

Kinana, wahenga walisema, you cant eat your cake and have it! Kama hii ni awamu ya sita kama inavyodaiwa, Samia Suluhu Hassan ni Rais kwa mujibu wa Katiba na si vinginevyo!
 
Ni kupoteza muda kufafanua mambo yanayoeleweka.

Mh. Rais Samia, ni Rais kwa mujibu wa katiba, na siyo kwa kupigiwa kura. Na hata wakati wa kampeni, hakuna inapoelezwa kwamba kama humtaki mgombea mwenza, usimpe kura mgombea wa Urais.

Anayoyaeleza Kinana kama yangekuwa sahihi, basi wakati wa upigaji kura kungekuwa na maeneo mawili ya kuweka kura yako, mgombea wa Urais na makamu wa Rais, na katiba ingetamka kuwa ili mgombea wa chama aweze kutangazwa kuwa Rais, ni lazima mgombea mwenyewe ashinde na mgombea mwenza ashinde, mmoja asiposhinda, wote wawili hawawezi kupitishwa kuwa viongozi wakuu wa nchi.

Mh. Rais Samia, kwa mujibu wa katiba yetu, ni Rais wetu halali. Kuuleza ukweli huu, kuna tatizo gani?

Kuhusu tamaduni za CCM kuwa Rais aliyepo madarakani, hatakiwi kushindanishwa na mwingine, sidhani kama ni jambo jema unapoongelea maendeleo ya demokrasia. Mila na desturi hii ya CCM, nadhani inatakiwa kuwekwa kwenye kundi la mila potofu.

Wanachama wanatakiwa kuwa huru kugombea, na wala haimaanishi kwamba jambo hilo ni kwa sababu watu hawamtaki Rais Samia, au Rais Samia hafai, bali ni kudumisha misingi ya demokrasia. Binafsi naamini, siyo kwa unafiki au upambe, Mh. Samia anafanya vizuri kuliko watu wengi ndani ya CCM wangepewa nafasi ya Urais.

Mh. Rais ana majukumu mazito kama Rais, tunamwombea ayatekeleze vyema ili watu wapige hatua za maendeleo. Mpaka sasa, naamini anafanya vizuri, na huenda akafanya vizuri zaidi mbeleni, lakini ni kosa kumjengea mazingira yatakayoashiria kuwa yupo kwenye nafasi hiyo kwa kuminya haki za kidemokrasia.

Huyu ni Rais wa kwanza Mama, tunataka aweke alama zitakazodumu katika Taifa letu. Alama mojawapo kubwa, aweke falsafa itakayoishi ya misingi ya kidemokrasia, misingi ambayo nchi Deikosa kwa muda mrefu.

Tuna Baba wa Taifa, tunamtafuta Baba au Mama wa demokrasia.
 
Kwa maelezo ya Kinana mwaka 2025 ndio mwisho wa huyu bibi bilionea
 
Lisu wako hawezi kuwa Rais mpaka tutakufa sote na wewe! That is stupid politician ever seen!
Naona Magufuli kafufuka...! Ulijaribu kumuua Lissu, ukatangulia wewe na bila shaka kwa hicho Kiingereza unaongea kutoka kuzimu! Nashauri waongeze kuni...
 
Naona Magufuli kafufuka...! Ulijaribu kumuua Lissu, ukatangulia wewe na bila shaka kwa hicho Kiingereza unaongea kutoka kuzimu! Nashauri waongeze kuni...
Huko kuzimu hata wewe na Lisu wako kunawasubiri! Ulivyo mshamba unashangaa mtu kufariki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…