KINANA: Urais wa Samia sio wa Kikatiba, amepatikana kwa Uchaguzi

KINANA: Urais wa Samia sio wa Kikatiba, amepatikana kwa Uchaguzi

Unafikiri atasemaje? Kazi kutetea tumbo tu.
 
Tanzania kungekua na wasomi wenye akili timamu, huu ufafanuzi wa kinana ungetosha kumfanya raisi samia asigombee 2025, maana muda wake utakua umeisha.
 
Huo Ushahidi mbona hujawahi kuutoa hadharani? Ni kama hivyo, basi Mwambie Kinana kuwa mama yenu hakupata kuchaguliwa na sio Raisi kwa mjibu wa Katiba kama anavyodai.
Kama hujawahi kuona basi wewe hukupiga Kura mwaka 2020 na ulyawezekana wewe ni Mrundi. Watanzania wenye AKILI TIMAMU wanajuwa 2020 hakukuwa uchaguzi. Angalia tu setup/composition ya Bunge tulilonalo uniambie kama kweli tuliwachagua wale
 
Kinana mzee wetu kuna sehemu umechanganya kidogo naomba kurekebisha.

Makamu wa Raisi hapigiwi kura, ndio maana hata Mpango ni makamu wa Raisi na hajapiguwa kura

Kwa katiba yetu hii, imeqcha tafsiri rahisi tu kuwa Raisi sio lazima apigiwe kura na wananchi nakushinda uchaguzi. Mfano ni kwa Mpango, Leo ikitokea Mama Samia hayupo, mpango atakuwa Raisi.

Mzee wetu kinana ipo hivi, chochote kinachotokana na katiba ni Cha kikatiba. Magufuli, JK, mkapa wote pia walikuwa maraisi kikatiba kwa kuwa katiba ndio iliwaweka madarakani kwa kushinda uchaguzi.

Hivyo hata mama Samia ni raisi wa kikatiba.

#kazi inaendelea#
 
Kama hujawahi kuona basi wewe hukupiga Kura mwaka 2020 na ulyawezekana wewe ni Mrundi. Watanzania wenye AKILI TIMAMU wanajuwa 2020 hakukuwa uchaguzi. Angalia tu setup/composition ya Bunge tulilonalo uniambie kama kweli tuliwachagua wale
Hunaga akili
 
Nadhan katiba haimzuii Mpango ku ascend kwenye power kama ikitokea incapacitation yoyote...Kinana yuko kazini, na kayasema aliyoyasema kwenye viunga vya nyumbani na shughuli yenyewe ilikua ndo haswa sehemu ya kupakana mafuta...ila kwa katiba yetu ilivyo...Kazi namba moja ya makamu wa RAIS ni kuwa back up ya RAIS..na ndio maana RAIS akiteua Makamu kama ilivyotokea kwa Mpango...Bunge kwa niaba ya wananchi wanatakiwa wamdhibitishe/ wampigie Kura..
Kina Yuko kazini, fafanua kdg. Ana agenda gn behind?
 
Unataka katiba iitishe uchaguzi rais akifa? Si walioshindwa uchaguzi watafanya njama za kumuua aliyeko madarakani ili wajaribu tena kwenye uchaguzi mpya?
Aseeee, kauli ya kinana ijadiliwe Kwa mapana, icjekuwa wanaogopa uchaguzi wanataka wawe wanapokezana bila ridhaa ya wananchi.

Nyerere hukuliona hili!!!!!
 
Kina Yuko kazini, fafanua kdg. Ana agenda gn behind?
Alitoa kauli hiyo mjini unguja kwenye kongamano mahususi la kumpongeza RAIS wa jamhuri kwa Kazi kubwa na iliyotukuka anayowafanyia Watanzania Bila kupumzika....Kinana ni VC wa CCM, CCM ni chama cha siasa, na Kazi/lengo kubwa na namba moja ya chama chochote cha siasa ni kushinda chaguzi na kushika madaraka...kwa muundo wa CCM, Kinana ndio kiongozi fulltime wa kuhakikisha ilo linafanyika wakati Chairperson wake anaongoza Executive... ingekuwa soccer basi wawili Hawa ni striking partners...mmoja chamani na mwingine Serikalini...Kazi inaendelea...
 
Rais Samia ni wa Kikatiba iwe amechaguliwa moja kwa moja na wananchi au iwe kaingia madarakani baada ya Rais aliyekuwepo kufariki (kama ilivyo sasa) njia zote ni za Kikatiba,kama ingekuwa ameingia kwa mapinduzi hapo ndio tungesema sio rais wa Kikatiba.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ameweka wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hasasan ni Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amepatikana kwa mchakato wa uchaguzi mkuu kwa kupigiwa kura na wananchi.

Kinana ametoa ufafanuzi huo jana wakati akizungumza na wana CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kutekeleza vema Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020/2025.

“Nataka niseme na vizuri Watanzania wakajua tangu Rais Samia achukue uongozi wa taifa letu kuna kauli nimekuwa nikisikia baadhi ya kauli kwamba Rais Samia ni Rais wa Katiba. Kauli hii ina ukweli lakini haina ukweli.

“Inaukweli kweli kwasababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kila chama kitaweka mgombea na mgombe mwenza na Katiba inasema mgombea Mwenza na mgombea wanafasi moja ya kupiga kampeni ya chama chao na kila Chama kinapochagua Mgombea Mwenza,”amesema Kinana.
============

Amefafanua CCM hakimchagua mgombea mwenza kwa kucheza bahati nasibu ya kutumbukiza halafu tuangalie nani kapata nani kakosa bali wameweka sifa, kwa kuangalia uwezo, kukubalika , anafaa ,uwezo wa kufanya kampeni, , anaweza kuleta kura nyingi na mwisho wanajiuliza iwapo mgombea kwa sababu yoyote atakuwa hayupo au ameondoka madarakani je mgombea mwenza atamudu nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vigezo vyote hivyo vilipimwa kwa Samia.

“Anaweza ndio , ana mudu, ndio, anajua kazi yake ndio, anaweza kufanya kampeni ndio, anaweza kumsaidia mgombea na kuleta kura ndio. Mwisho iwapo mgombea kwasababu yoyote ataondoka madarakani kwa njia za kidunia au zake Mwenyezi mungu anaweza kuchukua nafasi hiyo wana CCM tukajiridhisha ndio anaweza.

“Kwa hiyo kwa wale wanaosema huyu ni Rais wa Katiba si kweli , Rais Samia Suluhu Hassan alipimwa kabla ya kupewa hiyo nafasi, bahati nzuri mimi nilikuwa Katibu Mkuu wa Chama, nilishiriki vikao vya awali mwaka 2015 na wengine walikuwepo kwenye vikao, hayo maswali yote tulupojiuliza tukasema anaweza ,ana mudu hiyo kazi, anaongeza kura, ana uzoefu, anakifahamu chama cha mapinduzi lakini kama anahitajika kuwa Rais anaweza.

“Sasa unaposema Rais Samia ni Rais wa Katiba hakuchaguliwa sio kweli lakini kubwa zaidi Rais anapopigiwa kura na mgombea mwenza anapigiwa kura na kabla haijafika muda wa kupiga kura iwapo mgombea mwenza Mwenyezi Mungu atamchukua uchaguzi utasimmamishwa.”

Ameongeza kwa kueleza “Kwa nini usimamishwe? Kama kweli yeye ni Rais tu wa Katiba tuendeee kupiga kura mambo yaishe .Mwaka 2005 tulikuwa na mgombea mwenza wa CHADEMA Jumbe Rajab Jumbe mwenyezi Mungu akamchukua , uchaguzi ulisimamishwa, kwanini ulismamishwa? Kwasababu na yeye ananafasi muhimu hawezi rais wan chi akapigiwa kura au mgombea akapigiwa kura kama mgombea mwenza hayupo.

“Wanasema Rais Samia ni Rais wa Katiba hawasemi kweli, Rais Samia ni Rais aliyetokana na mchakato wa uchaguzi , alipopigiwa kura Rais Magufuli na Samia alipigiwa kura hapo hapo kama rais aliyemtangulia angekuwa ameondoka madarakani kwa kujiuzulu au kwasababu nyingine yoyote angekuwa Rais lakini kwasababu za Mwenyezi Mungu Rais Samia amechukua dhamana.

“Kwanini basi uchaguzi wa Chadema mwaka 2005 ulisimamishwa? Kwasababu wote wawili wanatokana na utaratibu wa Katiba uliowekwa kwa hiyo Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wale wanaosema ni Rais wa Katiba wana ajenda yao, msiwasikilize. Kama hawajui au wanajifanya hawajui , nadhani sasa watajua, nilisema wanaosema Rais Samia ni wa Katiba hawasemi kweli na nimetoa maelezo.

“Sasa nitoe upande wa pili kweli ni Rais wa Katiba.Katiba inasema hivi kila Chama kitateua mgombea na mgombea mwenza, kwa hiyo kila Chama kinateua Mgombea na Mgombea Mwenza , Rais au mgombea anatokana na matakwa ya Katiba ya Jamhurii ya Muungano wa Tanzania.


“Mgombea mwenza ni matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano , kwa hiyo anateuliwa Samia kuwa mgombea mwenza ambaye baadae anakuwa Rais anatokana na matakwa ya Katiba kwa hiyo Rais Maguli ni Rais wa Katiba , unapendekezwa na chama chako, uakwenda kwa wananchi lakini hupigiwi kura peke yako unapigiwa na mgombea mwenza.

“Iwapo hayupo uchaguz unaahirishwa , kwa hiyo nimalize kwa kusema tukisema kwamba Rais Samia ni Rais wa Katiba husemi ukweli, Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.nchi ya Marekani Rais wa sasa ni Rais wa 46 , katika marais 46 waliowahi kufariki kabla ya muda wao walikuwa marais wa nane baadae wakachukua wagombea wenza ambao baadae wakaja kuwa marais,” alifafanua.

Aliongeza kuwa, pamoja na hayo nchini Marekani hawajawahi kuwaita Marais hao ni WA katiba, “lakini hapa Tanzania wanaotaka kukoroga mambo wanakwambia Rais Samia ni Rais wa Katiba.”

Katika hatua nyingine, Kinana alifafanua kuwa, katika kudhirisha sifa za uongozi wa Rais Samia ameweka alama kubwa za maendeleo katika kila mkoa wilaya na shehia nchi nzima.

“Yote haya ya mefanyika katika muda mfupi wa mwaka mmoja wa uongozi wake
fedha za maendeleo zimetokana na ukusanyaji mkubwa wa kodi kwa njia ya hiyari, fedha za misaada na mikopo zilikuja kotokana na kukubalika kwake duniani.

SHAKA ASEMA RAIS SAMIA,DK.MWINYI 2030

Kwa upande wake Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, tikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ameweka wazi kwamba kwa kazi nzuri anayoifanya Rais Samia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwatumikia na kuwaheshimisha Watanzania, kuiheshimisha Afrika na Dunia awataendelea kuwa madarakani hadi 2030.

Amesema kwa pamoja wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kusimamia maendeleo endelevu na kudumisha na kuimarisha muungano.

“Mitano kwa Rais Samia haina mjadala biashara imekwisha, kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu, Katiba yetu na utamaduni wetu huu mjadala haupo tena.Kama kuna mtu ana ndoto, hizo ndoto zikae pembeni Dk.Mwinyi tunamalizana 2030 , Chama hiki kina msingi na msingi wake mkuu ni Katiba, Kanuni na taratibu lakini kina utamaduni wake , hivyo viongozi hawa watatuvusha mpaka 2030 halafu ndio tunaangalia Katiba inasemaje.

JAMHURI
Huyu Al shaabab naye atuondolee ujangiri wake hapa
 
Kwa mantiki hiyo mama Samia hapaswi kugombea uchaguzi ujao!
Ngoja nisaidie kujibu ki'Kinana', kama inawezekana.

Awamu ya sita hii, itakuwa imetimiza miaka mitano hapo 2025; atakuwa kabakisha miaka mitano mingine, itimie kumi!
 
Poor reasoning from Kinana! Kama kweli Kinana anadhania zile Kura Uraisi wa Magufuli zilichangiwa na uwepo wa mama ni kwa nini wananchi hawampendi mama kiasi hicho wakati walimpigia? Hivi anaamini Toka moyoni mwaka 2015 na 2020 watu walimpigia Magufuli kwa sababu yuko na Samia? Ama kweli ukubwa wa Kamasi sio wingi wa Kamasi. Nilitarajia Kinana kwa jinsi anavyosifiwa kuwa na Akili angetumia hoja nzito sana hata za Kifalsafa kumaliza huu mjadala lakini naona ameongea kingumbaru fulani hivi. Eti Makamu Mwenyekiti! Kiongozi wa Chama ni Maono. Hakuna maono yasiyoendana na namna ya kuchambua na kujibu hoja vizuri.
Ukiona hivi ujue Uzee tayari, na vile alikuwa anaongea na mangumbaro menzake maccm
 
Ngoja nisaidie kujibu ki'Kinana', kama inawezekana.

Awamu ya sita hii, itakuwa imetimiza miaka mitano hapo 2025; atakuwa kabakisha miaka mitano mingine, itimie kumi!

Utata mtupu!
 
Mbona Samia mwenyewe alishakiri kuwa umemuangukia tu.

Sasa ikitokea nae akaenda kwa baba huyu Mpango hatakuwa Rais?

Maana hajapigiwa kura kadiri ya Kinana.
 
Back
Top Bottom