KINANA: Urais wa Samia sio wa Kikatiba, amepatikana kwa Uchaguzi

Hapo ccm penyewe hawataki kumsikia wala kumuona huyo mama, ukiachana na hao walamba asali!
 
Utata mtupu!
Mkuu, 'Tindo', mimi sioni utata wowote; maadam CCM walishawaona waTanzania kuwa ni watu wasiokataa lolote linalotoka kwao ( CCM.).

Ninakuhakikishia ikifika wakati hawawezi kamwe kuona aibu yoyote ya kusema lolote, kama anavyofanya kwenye taarifa iliyoletwa hapa kwenye mada hii tunayoijadili sasa hivi hapa.

Hebu jiulize, haya anayoyasema hapo juu kweli ni mambo ya kuwaambia watu walio na akili zao nzuri kichwani? Hata hivyo, kayasema haya ili iweje hasa? Anataka watu waelewe vipi na kwa faida gani?

Nchi yetu hii tumerudi nyuma sana katika kila jambo unalotaka kulichunguza kuona ufanisi upo wapi.
 
Kwa kule zanziba wamepokea kwa mikono miwili na miguu kabisa
 
Kwani Uchaguzi wenyewe haupo kikatiba? Hivi inakuwaje mtu mzima na akili zake anatoa boko kama hili? Kila kitu kipo kikatiba. Na anachopinga ni ukweli usiopingika. Uko wazi.
 

Huyo mwindaji haramu naye hata akipindisha maneno namna gani, ukweli utabaki pale pale kwamba urais wa Hangaya haukupatikana kwa mchakato wa uchaguzi. Kura alizopewa 2020 zilikuwa za nafasi ya VP. Hajawahi kuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwaomba wapigakura wamchague kuwa Rais wa JMT.

Mbona wabunge wa viti maalumu na wale wa kuteuliwa na Rais hatuoni shida kuwavika taji hilo (kuwatambua kwa chapa hiyo)?
 
Ok yote uliyosema ni sahihi, But she is still our president.
Huna unachoweza kubadili katika mamlaka yake
 
Aiseee

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Hii inaonyesha jinsi elimu yetu ilivyo duni. Hata kuchambua mambo kisomi ni shida! Katiba ipo inajieleza vizuri sana licha ya kuwa ni ya chama kimoja! Tatizo nililoona kwenye katiba yenyewe haikufafanua sifa za mgombea mwenza ili aweze kushika wadhifa wa rais kama aliyepo atafariki. Na kama hizo sifa hana anapaswa kushikilia kwa muda gani hadi uchaguzi mwingine ufanyike. Kwa maoni yangu SSH anapaswa kukalia hicho kiti kukamilisha ngwe ya pili ya Rais Magufuli. Kama ana sifa za kugombea urais 2025 achukue fomu agombee hiyo nafasi kwa kupigiwa kura na wananchi.
 
Ni wapi Samia aliwahi kuomba kura za Urais , mbona 2020 alikuwa anatuomba tumchague Magufuli ?

Kinana hawezi kuachwa akipotosha katiba ya nchi , hatutakubali .
 
Hapa kwa sisi vilaza wa siasa ni kama tunapigwa changa la macho.Kwa sisi vilaza tunajua Mama alichaguliwa na Mwendazake kama Makamu wa Kwanza wa Rais.Sasa sijui uchaguzi ulifanyika lini?
 
Komredi
 
Muda si mrefu ukivaa nguo za kijani utaanza kuzomewa labda ziandikwe Yanga.
 
Huyu mzee tokea uteuzibwa akina Makala na Nchimbi ni kama amepoteana kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…