Ndiyo maana nikasema jambo linaweza likawa la umuhimu lakini lisiwe la kipaumbele kwa wakati uliyopo,ila ndiyo watu waanangali jinsi gani ya kuikomoa ccm na serikali yake.kama hilo litakua suluhisho la matatizo yetu yote kama watanzania na iondolewe. lakini madhara yake yanaweza kua makubwa sana kuliko faida.
Mkuu jamaa walivyokuwa wanaimba wimbo wao wa ccm ni ileile we ulidhani wanatania?Kama ni hivyo haya mapambano yake hayawezi kuwa endelevu, akimaliza muda wake ataondoka nayo! It shall have been some effort to futility!
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema kuondoa kinga ya Rais baada ya utawala wake ni hatari kwa usalama na demokrasia ya nchi.
Alisema kwa kuwa kila kiongozi hufanya maamuzi ya kisiasa ambayo wakati mwingine hayatimii, kuondolewa kwa kinga hiyo kunaweza kukaleta matatizo ya kisiasa kwa siku za mbele.
“Kuna mtu atakuja kung’ang’ania ikulu endapo atatambua kuwa yupo kwenye hatari ya kufikishwa mahakamani,” alisema Profesa Mukandala na akashauri zianzishwe taasisi makini na imara zitakazokuwa zinamshauri Rais juu ya maamuzi mbalimbali anayoyafanya akiwa madarakani.
Alisema hakuna haja ya kuwafikisha mahakamani viongozi wa ngazi hiyo, kama makosa yao yalitokana na mtazamo wa kisiasa na kukumbusha kuwa hata Rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere alishindwa kutekeleza mkakati wa kuanzisha Vijiji vya Ujamaa kama ulivyoratibiwa sawa na ilivyotokea kwenye Katiba Mpya kipindi cha Rais Kikwete.
we unadhani kwanini chuo kikuu chetu kumeporomoka ?Kama hii ndio namna ya profesa kufanya reasoning sijutii kamwe kutokufika chuo kikuu.
Yaani, Profesa Mukandala anaamini kuwa, rais akiondolewa kinga ndio atang'ang'ania madarakani lakini hakuweza kuona kuwa rais akiwekewa kinga anaweza pia kung'ang'ania madarakani kwa kuwa anajua hata jaribio lake likishindwa au kufanikiwa hatashitakiwa na yeyote yule?
Yaani, Profesa Mukandala anashauri zianzishwe taasisi imara na makini za kumshauri rais na bado haoni haja ya rais huyo huyo kubanwa kwa sheria fulani endapo atakataa kusikiliza ushauri wa taasisi hizo!!!
Yaani, Profesa Mukandala anaona kuwa 'kwa kuwa Mwalimu Nyerere alishindwa' basi kila rais ajaye naye anapata haki ya kushindwa na katika hili labda niulize: Mwalimu Nyerere ndio 'marking scheme' ya utendaji wa viongozi wetu wajao?
Hivi profesa anaweza kuainisha hatari za kiusalama na kidemokrasia zinazoikumba Marekani, South Africa na Brazil (kwa kutaja chache) kwa kuwa viongozi wao wa juu wanabanwa na sheria?
Ee Mungu tuhurumie!
lowasa na jk dugu moja wataendelea kuimba fisadi fisadi fisadi hakuna atakayekamatwa kati yao badala yake wezi wa kawaida ndo watakaa lupangoJK mjanja sana. Hakuna anayeweza kumuweka kati na kumsulubu.
Wataishia kuaibika wanaotaka kumshitaki JK.